TEUZI: Rais Samia amteua Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi, Sophia Mjema kuwa RC Shinyanga

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Wadau maoni yenu please Jaji za Zenji anafit kuja Tz? Maana zamani hata wakuu wa mikoa znz walikuwa wanateuliwa na Rais wa JMT baada ya mabadiliko ya katiba ta SMZ madaraka ya uteuzi wakawa chini ya Rais wa ZNZ na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, sasa kumtoa Jaji aliteuliwa na Rais wa SMZ sio kuingilia Mamlaka ya SMZ?

IMG-20211008-WA0051.jpg
 
Kesi ya uhujumu uchumi / ugaidi namba 16 /2021 ya Mbowe na wenzie 3

Jaji M. Siyani ataachiwa asikilize kesi ya Mbowe na wenzie 3 mpaka mwisho au ndiyo kesi atapangiwa jaji mpya?

Toka maktaba:

6 Sept 2021
Mahakama Kuu
Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
Dar es Salaam, Tanzania

Wakili Peter Kibatala azungumza baada ya Jaji Luvanda kujiengua



Habari kubwa iliyojitokeza Leo ni Jaji Luvanda ajitoa kesi ya Mbowe na wenzake.

Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya Ugaidi, amejitoa kusikikiza kesi hiyo.

Sababu ya kujitoa katika kesi hiyo ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuieleza mahakama hiyo kuwa yeye na washtakiwa wenzake watatu hawana imani na Jaji huyo katika kutenda haki dhidi ya kesi yao.

Kesi imehairishwa mpaka jaji mwingine atakapopatikana. Pia awali Jaji Elinaza Benjamin Luvanda alikataa kutoa uamuzi wake leo juu ya mapingamizi ya upande wa utetetezi mpaka atapopata hansard / kumbukumbu za majadiliano ya Bunge kuhusu sheria ya ugaidi.

Wote walikubaliana kuwa kesi hii ina masilahi mapana kwa umma wote waliopo ndani ya Mahakama na nje.

Hoja 3 za upande za upande wa utetezi zilikuwa zinashambulia madhaifu na kasoro ya hati ya mashtaka. Hoja ya kwanza ilikubaliwa na jaji wakati hoja ya pili ilikubaliwa kwa nusu yake na jaji wakati hoja ya tatu ya kutupiliwa mbali au kufutwa kesi, jaji aliikataa.

Na kwa msingi huo mtuhumiwa Freeman Mbowe kwa niaba ya wenzake akasimama na kusema hawana imani na Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuendelea kusikiliza kesi hiyo, na mheshimiwa Jaji E.B Luvanda akaafiki ombi hilo na kujiengua kusikiliza kesi hii.
Source : Mwananchi Digital



Kutoka maktaba :

10 September 2021
MAHAKAMA KUU DIVISHENI MAALUM KUSIKILIZA KESI YA FREEMAN MBOWE NA WENZIWE 3, MFULULIZO KUANZIA TAREHE 15 SEPTEMBER 2021



Jaji Mustapher Siyani ameanza jukumu lake na kupanga kuanza kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi / ugaidi namba 16 /2021 ya Mbowe na wenzie 3 ambao kwa pamoja wa wakabiliwa na tuhuma za ugaidi kwa mujibu wa upande wa mashtaka wa serikali.

Mahakama hiyo chini ya jaji Mustapher Siyani imekubali pia ombi la upande wa utetezi unaoongozwa na wakili Peter Kibatala kuwa upande wa utetezi una mashahidi wake kadhaa na kuiomba Mahakama Kuu kuwa miongoni mwao mashahidi hao, wapo mashahidi 4 walindwe na Mahakama wasitangazwe anuani zao wala majina yao kwa kuhofia kufuatwa na vyombo vya serikali.
 
Huu uteuzi wa Siyani umekuja kimkakati au ni mpango uliokuwepo?

Hasa wakati huu ambao hukumu ya kesi ndogo ilikuwa inasubiriwa tar 19.10.2021, Siyani akiwa kama muhusika mkuu kwenye kesi iliyojaa siasa kama ile napata mashaka.

Nilimkubali sana alivyosikiliza kesi ndogo ya Mbowe, alikuwa kama refarii haswa, upande mmoja ukiweka objection anauliza upande wa pili wanaonaje.

Then wakijibu anarudi kwa upande wa waliotoa objection kama wanakubaliana na hoja ya upande wa pili, wakikataa, jaji anaangalia sheria inasemaje, then anaupa haki upande unaostahili kesi inaendelea kusikilizwa.

Sijui kama wataipangia kesi jaji mwingine, if yes, napata ukakasi na huu uteuzi kama sio wa kimkakati, kumuondoa huyu aliekuwa anaenda na sheria/haki halafu wamrudishe kama yule wa mwanzo kuwafundisha jamhuri nini cha kufanya, fingers crossed.
 
Hii ya Jaji Makungu imekaeje,amepanda cheo au kashushwa.au maandalizi ya kuwa jaji mkuu
Zanzibar Mahakama inaishia Mahakama kuu tu, hivyo Jaji Makungu alikuwa Jaji Mkuu wa Mahakama kuu ya zanz, na mahakama zililo chini, suala la mahakama ya rufaa ambayo ndio iliyo juu kabisa ni suala la Muungano hivyo ni sawa kuteuliwa huku, rejea inaweza kufanywa kwa Jaji Ramadhani ambaye kabla yakuwa Jaji Mkuu huku alikuwa Jaji Mkuu zanzibar baadaye akateuliwa kuja kuwa Jaji Rufaa.
 
Miaka mingi nyuma, majina ya viongozi wengi yalikuwa maarufu kwa wananchi, siku hizi mimi kuwajua hata mawaziri tu ni shida, yaani mpaka afanye mambo ya kiki ndo nimjue, sijui kama ndo ilivyo kwa wengine!
 
Pongezi kwa wateule wote, lkn pongezi nyingi sana Kwa Jaji Mustafa Siyani kuwa Jaji Kiongozi Mpya wa Mahakama.
Hakika ataijenga Mahakama vizuri zaidi.
ajenge usawa ktk mhimili wa mahakama, umoja, upendo na Haki kuanzia ndani ya watumishi wa Mahakama wenyewe na kwa wananchi wote.
 
Kheri yao wateuliwaji......Namuona dada sofia mjema kaongezewa ugali wake
 
Back
Top Bottom