TEUZI: Rais Samia amteua Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi, Sophia Mjema kuwa RC Shinyanga

CJ ni Muislam
JK ni Muislam
Msajili Wa Mahakama Tz ni Muislam

Mkuu acha kuendekeza udini, usiangalie nafasi za hao wateule 3 au 4 tu halafu ukahitimisha.
Mimi ni mkiristu lkn naweza kukwambia kuwa ukiangalia kiuhalisia ktk mhimili wa Mahakama wakristu ndio wengi zaidi, angalia idadi ya Majaji, Wasajili, Watendaji, Mahakimu n.k, viongozi na ambao sio viongozi.
Mimi napenda sana uwiano ktk nafasi ZA uongozi wa nchi yetu kama anavyo fanya Rais Samia maana Uwiano huimarisha umoja Na mshikamano wa Taifa letu.
Taifa letu haliwezi kujengwa Na watu wa aina moja tu bali watanzania wote.
Kazi iendelee.
Mungu azidi kumbariki Rais wetu mpendwa Samia.
Anatuongoza vyema sana
 
Wadau maoni yenu please Jaji za Zenji anafit kuja Tz? Maana zamani hata wakuu wa mikoa znz walikuwa wanateuliwa na Rais wa JMT baada ya mabadiliko ya katiba ta SMZ madaraka ya uteuzi wakawa chini ya Rais wa ZNZ na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, sasa kumtoa Jaji aliteuliwa na Rais wa SMZ sio kuingilia Mamlaka ya SMZ?

View attachment 1968490
Kumekucha ni Siri nyuma yake ya uteuzi huu?

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
CJ ni Muislam
JK ni Muislam
Msajili Wa Mahakama Tz ni Muislam
jamani tuacheni hizi mbishe,

tumuhukumu kwa vigezo vyake

angechukuliwa mtu from no where bila vigezo tungekua na haki ya kuhoji,

lakini hawa wote wanaoteuliwa ni watu waliokwiva kwelikweli, wajuvi kwelikweli

hawajapendelewa.
 
Wadau maoni yenu please Jaji za Zenji anafit kuja Tz? Maana zamani hata wakuu wa mikoa znz walikuwa wanateuliwa na Rais wa JMT baada ya mabadiliko ya katiba ta SMZ madaraka ya uteuzi wakawa chini ya Rais wa ZNZ na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, sasa kumtoa Jaji aliteuliwa na Rais wa SMZ sio kuingilia Mamlaka ya SMZ?

View attachment 1968490
Uteuzi wa kimkakati
 
Samia amekwishasema kuwa anataka mahakama itende haki. Mnataka amteue mtu dhulumati kama maganga awe jaji kiongozi?
 
Huu uteuzi wa Siyani umekuja kimkakati au ni mpango uliokuwepo?

Hasa wakati huu ambao hukumu ya kesi ndogo ilikuwa inasubiriwa tar 19.10.2021, Siyani akiwa kama muhusika mkuu kwenye kesi iliyojaa siasa kama ile napata mashaka.

Nilimkubali sana alivyosikiliza kesi ndogo ya Mbowe, alikuwa kama refarii haswa, upande mmoja ukiweka objection anauliza upande wa pili wanaonaje.

Then wakijibu anarudi kwa upande wa waliotoa objection kama wanakubaliana na hoja ya upande wa pili, wakikataa, jaji anaangalia sheria inasemaje, then anaupa haki upande unaostahili kesi inaendelea kusikilizwa.

Sijui kama wataipangia kesi jaji mwingine, if yes, napata ukakasi na huu uteuzi kama sio wa kimkakati, kumuondoa huyu aliekuwa anaenda na sheria/haki halafu wamrudishe kama yule wa mwanzo kuwafundisha jamhuri nini cha kufanya, fingers crossed.
Huu uteuzi una mashaka mengi. Naiona rushwa ya cheo ikitamalaki
 
Tusubiri labda tarehe 19/10/2021 ndio tutapata majibu kamili, sasa hivi ni ubashiri tu.
 
Haya maandishi ya kizungu wananchi wengi hatuyaelewi.
Baada ya Uteuzi wa Jaji Kiongozi Mpya Siyani Wakishirikiana na Mtendaji Mkuu wa Mahakamq Prof: Elisante wananchi tunaimani kuwa sasa Matumizi ya Lugha ya Kiswahili katika kutoa haki za wananchi kuanzia Mahakama za Wilaya hadi Mahakama za Rufaa yataharakishwa kwa masilahi ya wananchi wa Tanzania.

kiSwahili hakijitoshelezi katika taaluma nyingi. Bado mapema sana kuanza hatua hiyo kubwa.

Hata lugha ya French na English wamekopa sana maneno ya Sayansi, utabibu, sheria n.k kutoka lugha ya kigiriki na kilatini ili kufikisha ujumbe wa kitaaluma bila kupotosha dhima ya ujumbe ynaokusudiwa.

Sababu ya waFaransa na Waingereza kukopa maneno kibao ni baada ya wao kujitathmini na kutambua mfano lugha ya French ni kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe wa kimapenzi inaongoza. Huku lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya kuandika mashairi na michezo ya kuigiza inaongoza.
French is a Romance language.
Sasa lugha ya kiSwahili tufanye tathmini inaongoza katika kuwasilisha na kutumika katika nini kuliganisha na lugha zingine za kibantu labda inaongoza katika kueneza dini na kuimba lakini inapokuja suala la taaluma ipo nyuma sana hivyo ijipange kukopa na kutohoa maneno ya kitaaluma toka ktk lugha za kigiriki, kilatini, kiarabu, kiEnglish, kifaransa n.k ili tusije kuwa tunapotoka ktk kuwakilisha elimu na maana husika za kitaaluma.
 
Tukimsikiliza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu tunapata picha kuwa majukumu ya jaji kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania ni nafasi ya kiutawala na kiutendaji zaidi kuhakikisha Mahakama zinapata waajiriwa wa kutosha, vitendea kazi, kutatua changamoto zinazojitokeza, kufukuzia bajeti na stahili za wafanyakazi kama mahakimu wafawidhi, majaji n.k

Hivyo jaji Kiongozi kutumika mahakamani kusikiliza kesi, kwa Jaji Kiongozi itakuwa ngumu maana yupo zaidi kusimamia taasisi kama msaidizi na mshauri wa Jaji Mkuu

27 Jan 2020
JAJI KIONGOZI ELIEZER MBUKI FELESHI " HAKUNA URASIMU KUFUNGUA MASHAURI, UNAWEZA KUSIKILWA SIKU HIYO HIYO"

Uongozi wa mahakama umezungumza na wanahabari kwa lengo la kueleze mafanikio ya muhimili huo muhimu ambapo pamoja na mambo ya kupunguza idadi za kesi ambazo hazijapagiwa kusikilizwa, umetangaza mpango wa kujengwa kwa jengo la mahakama kuu Dodoma. Jaji Kiongozi Eliezer Mbuki Feleshi aliwapa wanahabari wasaa wakuuliza maswali ambayo pengine yanahitaji majibu ya kina.
Source : Global TV online
Mbona kwenye kesi ya mauaji ya akina Zombe na wenzake kesi alisikiliza jaji kiongozi wa wakati huo (jina limenitoka)?
 
Back
Top Bottom