Gutapaka
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 283
- 218
Hivi ni kwa nini tunasinzia kihasi hiki kama taifa? Tunafahamu watu kama maafisa elimu wa mkoa, wilaya wanatakiwa kuwa na walau shahada moja au zaidi, lakini mtu anaye waongoza eti ajue kusoma na kuandika tu(Elimu ya msingi) hili si balaa!
Halafu tunapigana kuwa nchi yenye uchumi wa kati ikiwa bado mifumo yetu inabakana kwa kushindwa kutoa thawabu za elimu.
Nchi za wenzetu jambo la kuwa mkuu wa wilaya au mkoa ama waziri sio la mchezo mchezo, kipao mbele cha kwanza taaluma, cha pili uchumi ili wananchi wasiibiwe kwa uroho wa mali.
Lakini hapa ni vihoja tupu, mi nafikiri kama kuna dhamira ya kupambana na ubadhilifu ni lazima katiba ibadilike kwa kutoa sifa stahiki za teuzi mbalimbali kama vile mawaziri, kwanza waombe, kama wana taaluma, pia uchumi wao uanzie milioni kumi na tano za tanzania, ili kupunguza utitili wa wanasiasa katika mambo ya kitaaluma.