Tetesi za usajili majuu

hantouch

Senior Member
May 7, 2014
155
225
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemwambia wakala wake Jorge Mendes kufanikisha uhamisho wake kurejea Manchester United (Sun).

Manchester United watawapa Real Madrid David de Gea, 26, pamoja na pauni milioni 183, ili kumsajili Cristiano Ronaldo, 32 pamoja na Alvaro Morata, 24 (Tuttosport).

Manchester United itawapa Real Madrid David de Gea pamoja na pauni milioni 175 kumchukua Ronaldo, na pia watamfuatilia Alvaro Morata katika mkataba mwingine tofauti (Daily Mirror).

Iwapo De Gea atakwenda Real Madrid, Manchester United watamfuatilia kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 18 (Calciomercato)

Tetesi za soka Jumapili 18/06/2017Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 17.06.2017

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hamtaki Ronaldo kwa sababu anahisi kiwango chake kimeanza kushuka (Diario Gol).

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amempigia simu Ronaldo kujaribu kumshawishi asiondoke Madrid (Marca).

AC Milan huenda wakaamua kumfuatilia kipa wa Manchester City Joe Hart, 30, iwapo kipa wao Donnarumma ataondoka (Daily Express).

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amekuwa akivutia timu mbalimbali nchini Spain, Italia, Uturuki na Marekani pamoja na China, lakini Rooney pia huenda akaamua kubakia Old Trafford (Times).

Wayne Rooney anashikilia rekodi ya kuifungia England mabao mengi zaidi, mabao 53 katika mechi 119

Chelsea wataongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro, 26, pamoja na kiungo Tiemoue Bakayoko, 22 (Guardian).

Kiungo wa Italy Marco Verratti, 24, anataka kuondoka Paris Saint Germain kwenda Barcelona (Gazzetta dello Sport).

Liverpool bado wapo kwenye mazungumzo na Roma kuhusu uhamisho wa winga Mohamed Salah, 25, lakini hawataki kulipa pauni milioni 35 wanazotaka klabu hiyo ya Seria A (Sky Sports).

Cristiano Ronaldo hakulipa kodiCristiano Ronaldo aandika historia kufikia magoli 100

Everton watafikisha pauni milioni 60 za usajili wiki hii watakapokamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Malaga, Sandro Ramirez, 21 (Daily Star).

Southampton wanataka kumsajili beki wa kimataifa wa Austria, Kevin Wimmer, 24, lakini wanataka Tottenham kupunguza bei ya pauni milioni 20 (Daily Mirror).

Leicester City wanafikiria kutoa dau la pili kumtaka beki Jonny Evans, 29 kutoka West Brom (Daily Telegraph).

Chelsea wanataka kuongeza dau kufikia pauni milioni 60 kumsajili beki wa Juventus Alex Sandro (Daily Express).

Manchester United wamempa 'ofa'ya mkataba mkubwa zaidi Blaise Matuidi, kuliko aliokuwa nao sasa PSG (PSG United).


Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 44 kumsajili winga wa Sporting Lisbon Gelson Martins (A Bola).

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang huenda akaungana na meneja wake wa zamani Jurgen Klopp, Liverpool (Le Parisien).

Barcelona watatumia kifungu cha kumnunua tena Gerard Deulefeu kwa kutoa pauni milioni 10.5 kwa Everton (Times).

Marco Asensio huenda akaomba kuondoka Real Madrid iwapo timu hiyo itasajili wachezaji watakaomuweka 'benchi', huku Arsenal, Liverpool na Juventus wakiwa wamemuuliza kiungo huyo mshambuliaji (Diario Gol).

captionBeki wa Brazil Alex Sandro

Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 26.3 kumsajili kiungo wa Barcelona Arda Turan (AMK).

Mshambuliaji wa Arsenal Takuma Asano, 22,atabakia kucheza kwa mkopo Stuttgart msimu ujao kwa sababu hawezi kurejea Emirates kwa kuwa hajatimiza vigezo vya kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza (Daily Express).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara tu zitakapothibitishwa.

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka wote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom