Tetesi za Soka Ulaya Leo Jumanne 28.06.2016

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Chelsea wanajiandaa kuingia katika mbio za kumwania kiungo wa Roma Axel Witsel, 27, ambaye yuko Ufaransa na timu yake ya taifa ya Ubelgiji katika Euro 2016 (Daily Mail)

Barcelona huenda wakamnyatia beki wa Arsenal Hector Bellerin, 21, baada ya Dani Alves kuondona Barca na kwenda Juventus (London Evening Standard)

Crystal Palace wamekubaliana ada ya uhamisho ya pauni milioni 31.6 ya kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Mitchy Batshuayi, 22, anayechezea Marseille (Guardian)

Manchester City huenda wakawazidi kete Manchester United na Benfica katika kumsajili winga Marlos Moreno, 19, anayeichezea Atletic Nacional ya Colombia kwa pauni milioni 8 (Daily Mail)

Real Madrid wanapanga kumtoa mshambuliaji wake Jese, 23, kwa mkopo msimu ujao, licha ya mchezaji huyo kusakwa na Chelsea na Manchester United kwa mkataba wa kudumu (AS)

Meneja wa Hull City Steve Bruce anafikiria kumsajili mshambuliaji kutoka Paraguay anayecheza Augsburg Raul Bobadilla, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 5 (Daily Mirror)

Leicester City wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo Nampalys Mendy, 24, kwa pauni milioni 13, kutoka Nice (Leicester Mercury)

Zlatan Ibrahimovic, 34, atafanya vipimo vya afya Old Trafford wiki ijayo kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja (Sky Sports)

Beki wa Chelsea Baba Rahman, 21, anasakwa na Lazio ambao tayari wametoa dau la pauni milioni 13 kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana aliyenunuliwa na Chelsea msimu uliopita kwa pauni milioni 21.7 (Daily Mirror)

Napoli wamekubaliana maslahi binafsi na Hector Herrera, 26, anayesakwa na Liverpool, lakini klabu hiyo ya Italia bado haijakubaliana na Porto ada ya uhamisho wa kiungo huyo (Tutto Mercatto)

Arsenal wamepanda dau kumtaka mshambuliaji Gabriel Barbosa, 19, ambaye kifungu chake cha uhamisho ni pauni milioni 40, katika klabu yake ya Santos ya Brazil (ESPN Brazil)

Meneja wa Everton Ronald Koeman anajiandaa kumsajili kipa Maarten Stekelenburg, 33, ambaye alikuwa Southampton msimu uliopita kwa mkopo akitokea Fulham (Liverpool Echo).

13566964_772601419543989_4592892084924387779_n.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom