Tetesi za soka Jumapili 18/06/2017

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Real Madrid wamesema timu itakayomtaka Ronado italazimika kulipa pauni milioni 350.
Real wana matumaini kuwa bei hiyo huenda ikawakatisha tamaa Paris Saint Germain na Manchester United zinazomtaka Ronaldo (Mail on Sunday).

Lakini washauri wa Ronaldo wanasema ada ya pauni milioni 131 itatosha kumsajili mchezaji huyo ambaye anataka "changamoto mpya" (Sunday Telegraph). Chelsea wameibuka na kusema wanamtaka Cristiano Ronaldo, huku mmiliki Roman Abramovic akisema yuko tayari kuvunja rekodi ya dunia ya usajili (Sunday Express).

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amemuambia Ronaldo kuwa hatomzuia iwapo anataka kuondoka Spain (Marca). Ronaldo atabakia Real Madrid iwapo klabu hiyo itakubali kumlipia kodi anayotuhumiwa kudaiwa ya pauni milioni 13 (Sunday Mirror).

Paris St-Germain wanajiandaa kumfanya Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji aghali zaidi duniani, baada ya kusikia kuwa anataka kuondoka Madrid (Don Balon). Manchester City nao wamewasiliana na Cristiano Ronaldo baada ya kusikia kuwa anataka kuondoka Real Madrid (Don Balon).

Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa kulia wa Juventus Dani Alves, 34 (Guardian).
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola pia anataka kumsajili beki wa kulia wa Tottenham Kyle Walker 27 (Sun).

Bayern Munich wana matumaini ya kuwapiku City kumsajili Kyle Walker, wakipanga kumpa mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki (Sunday Express). Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa winga kutoka Misri, anayechezea Roma Mohamed Salah, 25 (Mail on Sunday).

Meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique huenda akachukua nafasi ya Antonio Conte, ingawa Chelsea hawataki Conte aondoke (Sunday Telegraph). Chelsea wana matumaini kuwa Antonio Conte atasaini mkataba mpya mwanzo wa msimu ujao na kubakia 'darajani' (Times).

Chelsea huenda pia wakatibua mipango ya Manchester United, kwa kutoa dau la pauni milioni 70 kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata 24 (Sunday Mirror).
Tottenham huenda wakataka kumsajili beki wa kati wa Manchester United Chris Smalling, 27 (Sun).

Arsenal watawazidi kete Everton katika kumsajili mchezaji wa kimataifa kutoka Norway Sander Berge, 19, anayecheza klabu moja na Mbwana Samatta, Genk (Sunday Mirror).

Mshambuliaji wa Malaga, Sandro Ramirez, 21, amefanya vipimo vya afya na anakaribia kusaini mkataba wa pauni milioni 5 kujiunga na Everton (AS). Liverpool bado wanafikiria kumsajili winga wa Sporting Lisbon, Gelson Martins, 22, ambaye klabu yake ya Ureno inasema ana thamani ya pauni milioni 44 (A Bola).

Everton wanataka kupanda dau la pauni milioni 16 kumtaka mshambuliaji wa AC Milan M'Baye Niang aliyecheza kwa mkopo Watford msimu uliopita (Daily Star). Everton watalazimika kulipa pauni milioni 40 iwapo wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji Gylfi Sigurdsson, 27 kutoka Swansea (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Bournemouth Joshua King amesema alishtushwa na taarifa zinazomhusisha na kuhamia Tottenham, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway wamesema hana mpango wa kuondoka (Bournemouth Echo).

Wakala wa Willy Caballero amesema kipa huyo wa zamani ameitwa Newcastle lakini mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City hana uhakika wa kwenda "kwenye baridi" (Evening Chronicle).

Southampton wanataka kuteua meneja mpya ndani ya siku 10 zijazo kabla ya mechi za kuanza kwa msimu Juni 29, huku Frank de Boer na Mauricio Pellegrino wakitajwa kuwania nafasi hiyo (Daily Echo).

Meneja mkuu wa klabu ya Juventus Beppe Morata amesema klabu hiyo ina wajibu wa kufikiria kumsajili kipa mwenye kipaji wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 18, kama itawezekana, na pia amethibitisha kuwa wanakaribia kukamilisha usajili wa Douglas Costa, 26 kutoka Bayern Munich (ESPN).

Rais wa Real Sociedad Jokin Aperribay amesema klabu hiyo inataka kumsajili winga wa Manchester United Adnan Jazuja, 22 (Manchester Evening News). Kiungo wa Arsenal Alex Oxlade Chamberlain, 23, anazidi kughadhabishwa na mwendo wa taratibu kuhuzu mazungumzo ya mkataba wake mpya Emirates (Mail on Sunday).

Bayern Munish wameshtushwa na mshahara mkubwa anaodai Alexis Sanchez, na wanahisi anajaribu kulazimisha kwenda Manchester City (Daily Mirror).

Manchester United wameanza mazungumzo na Lyon kutaka kumsajili mshambuliaji Alexandre Lacazette, iwapo watashindwa kumpata Alvaro Morata. Lyon wanataka pauni milioni 50 kumuuza Alexandre Lacazette, huku Arsenal wakiongoza mbio za kumsajili, lakini Manchester United, Chelsea, Borussia Dortmund, Liverpool na Atletico Madrid nao wana nusanusa (L'Equipe).

Lyon wapo kwenye mazungumzo ya kina kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Bertrand Traore, kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo Jean-Michel Aulas (Goal.com).

Barcelona wameanza mazungumzo na PSG ya uwezekano wa kumsajili Marco Verratti (Gazzetta dello Sport). Roma nao wamejiunga katika mbio za kumsajili beki wa Manchester United Matteo darmian (Corriere dello Sport).

Habari zilizothibitishwa tutakufahamisha mara zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.

bbc swahili
 
bbc swahili[/QUOTE

Kwa Wenger itabaki kuwa tetesi hadi mwisho
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom