Rais Magufuli kutembelea Temeke zazua taharuki, barabara zaanza kutengenezwa usiku na mchana

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,888
Tetesi za Raisi Magufuli kutembelea Temeke zazua taharuki barabara zaanza kutengenezwa usiku na mchana nyingi zilikuwa mbovu na midimbwi kibao nimepita leo Tandika nikashangaa nikaambiwa kuna tetesi Rais atatembelea Temeke.

Watendaji ofisini hawaonekani wanashinda site kusimamia kazi.

Raisi Magufuli shikamoo.
 
Natamani akitua tuu aondoke na yule mtaalam aliye kuwa ana bishana na Dc Gondwe kama mchumba wake. Nilijisikia vibaya sana alivyo kuwa ana jibizana na Dc. Hana heshima kabisa.

Natamani angeingia ang aza Sabaya au Kennan unge kuta ndio ana malizi amalizia masaa yake 48. Na kazi sio wilayani kwake tena.
 
Kwahio inteligensia yake ilikuwa haijamfahamisha kwamba haya mambo Tanzania yapo ? Hapo hakuna wa kupewa heko ni kwamba wote in one way or another kuna walakini.

Na kutengeneza vitu usiku na mchana ndio kufuja kodi zetu sababu ufanisi utatokea wapi kwa vitu vya haraka haraka?

Hii nchi kila mtu Msanii.
 
Hewa hiyo tunamshukru Yehova kwani inatumika kama kings kuzuia ugonjwa mapumuzi legekege so kwauchafu rule, msimu Wa Maembe inzi ananenepa hapi anakutishia si kwa mvumo ule nyuki anasubiri
Tegeta looo sijawahi ona soko chafu ka la tegeta hivi lile dambo sokoni hampati kipindupindu
 
Unasifia ujinga, badala atengeneze mifumo imara ya kusimamia uwajibikaji, kila kitu kinasubiri mpaka yeye aende, halafu nyie wajinga mnabaki kuleta propaganda za kitoto kuwa rais kurudisha uwajibikaji kwenye ofisi za umma. Kwahiyo sehemu ambazo rais hatatembelea ni sawa kuendelea kuwa na matatizo?
 
Huko tegeta hakuna mtendaji, diwani au mbunge wa ccm? Maana hao ndio waliiba kura kwa kujifanya wananchi wamewachagua kisa wao ni battery. Sasa battery hizijachanganywa na magunzi, mbona haziwaki
hilo tatizo liko toka kipindi chadena wameshika jimbo
 
Maybe my understanding is shallow,
But kwa mimi hili si jambo la kufurahia na kutoa heko,
Ni jambo la kusikitisha sana tena SANA.
Yaani baada ya 5 years still kuwe na ishu za kazi za kushtukizana kisa flani anakuja wakati ilbidi by now tuwe na mfumo unaoeleweka hata mtu asipoenda eneo hilo kazi ziwe znafanyika kwa efficiency kama kawa
 
Mwaka 1963, nikiwa kwenye msafara wa mwalimu, tulitemveoea shamba darasa kwenye kijiji fulani huko kusini, shamba lilikua limenawili sana, basi mwalimu akashika mche mmoja wa mhindi, kuvuta kidogo tu mhindi ukachomoka, kumbe lile lilikua shamba fake,mahindi yaling'olewa sehemu na kuja kupandikizwa hapo, kwa ajili tu ya ziara ya rais.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom