Tetesi za Matokeo ya NECTA kidato cha nne 2012 [Kabla Hayajatoka]

Status
Not open for further replies.
Matokeo ya kidato cha nne kwa mitihani iliyofanyika October mwaka jana yanakaribia kutoka. Katika matokeo hayo ambayo vikao vyake vya mwisho ndio vinafanyika,ufaulu umnaonekana kushuka.Nyaraka zinaonesha kuwa Shule za Seminari,kama ilivyo ada,zinaoongoza.Baadhi ya Shule za Serikali zinajikongoja ingawa ufaulu katika Shule zetu za Kata ni wa utata mtupu.

Matokeo hayo ambayo nimefanikiwa kuyachungulia kiintelijensia yanaonesha kuwa wanafunzi wa Sayansi ndio waliofaulu zaidi ya wale wa masomo ya Sanaa. Wasichana,katika ufaulu wa kitaifa,wameng'ara kuliko wavulana. Hali katika Shule zetu za Serikali hasa za Kata si nzuri hata kidogo. Yakitoka,hapatatosha!

Matokeo hayo yanatarajiwa kutangazwa muda wowote hasa kuanzia tarehe 1/2/2013.

ANGALIZO: Siwezi kutaja kwa majina Shule za kwanza na za mwisho na wanafunzi wa namna hiyo kwakuwa matokeo rasmi hutangazwa na Serikali.

We mwongo mbona mpaka leo date 7 hayajatangazwa?
 
Eti ni kweli matokeo yanatoka leo? Na yanaweza kutoka saa ngapi? Naomba mniambie kama mnajua.:A S cry:Wengine tushachanganyikiwa.
 
Eti ni kweli matokeo yanatoka leo? Na yanaweza kutoka saa ngapi? Naomba mniambie kama mnajua.:A S cry:Wengine tushachanganyikiwa.
Sasa kama umechanganyikiwa matokeo yatakusaidia nini?Maana sehemu unayotakiwa kuwepo saa hizi ni milembe.
 
Nipo hapa katika ukumbi na katibu ndo anatueleza hayo matokeo so nimeamua kuwapasha japo kidogo,asilimia 50.02 ya watahiniwa wamefaulu, shule za binafsi zang'ara na za vipaji maalumu.

Top ten ina shule za St. Francis, Marian, Feza boys, St. Joseph Millenium, Abbey, St.Mary Goreth, Kandoto girls, Mzumbe, Kibaha, Ilboru na wanafunzi bora ni Mary A . Ndona(St. Francis), Rebecca Nsingwe (Marian), Joseph Ulapi(Mzumbe), Ismail Kandeya(Arusha day), Martin Kaimbo(Kibaha)

...ntazid kuwajuza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom