Tetesi: Wmbo "AHMADA UMELEWA" wa Bi Kidude unajambo?

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Kuna tetesi huku mitaani kuwa wimbo wa "Ahmada umelewa" wa Bi Kidude amemwimba rais mstaafu wa vile visiwa vya karafuu. Tetesi hizi zinasema huyo mheshimiwa sana wa ule ukoo unaojulikana sana visiwani na nje ya visiwa alimwita huyo ajuza(kikongwe) katika kasri lake linalolindwa na manjagu, akamshauri aache pombe kwani inampunguzia heshima yake haswa vituko anavyofanya akilewa. Maana alisikia hako kabibi kanawakera watu kwa jinsi alivyo-cha-pombe.

Kibibi huyo baada ya kuambia hayo, kwakuwa anafahamu kuwa mshauri wake huyo ni cha pombe naye, akakakusudia na kisha kuitimiza azma yake ya kutunga songi hilo.

Hii ndiyo sababu wimbo huo haupigwi kunakovisiwa vya karafuu.

Naomba kujua zaidi.....
 
mkuu,

mambo makubwa hayo, tembelea hapa, ujifurahishe

Tujulishe utakapopata jibu la tetesi hizo.

kama ni kweli hizo tetesi basi, namvulia kofia ajuza huyo.
 
Last edited by a moderator:
Nasema ni kweli! Amini usiamini kama mwulize masele.

Makofia, sijakupata mkuu.
Unamaanisha Masele chapombe wa MIZENGWE? Au unamaanishamwingine?
Je! Unataka kutuambia naye alipigwa mkwara na huyo mheshimiwa ama Bi Kidude alimmegea ishu ya huo wimbo Masele ? Au Masele alikuwepo wakati jambo hili linatukia?

Habari hii nzito, nithibitishie zaidi ili tusije amini jambo kumbe ni uzushi tu.
 
Mh! Niliskia ule wimbo umefungiwa usipigwe Zanzibar kwa sababu hilo jina ni la mtu flani mkubwa.
Hilo ni la kweli kabisa.
Ila kuhusu hilo jina la Am'mada ni la rais mstaafu sina hakika ila serikali ya Zenji imesema huo wimbo usipigwe kwa sababu ni jina la kiongozi flani so ni kumzalilisha kama utaendelea kupigwa.
Ikumbukwe hata ule wimbo wa Bata ulioimbwa na kundi hilo hilo nao umepigwa marufuku.
 
Mkuu Ndiba nimekusoma.
Lakini lisilopingika kuwa msanii anaweza tumia jina bandia ili ujumbe wake ufike vizuri. Nyuma ya pazia ukufikiria ndipo utajua jina hilo linamanisha nini. Hebu tujikumbushe zile tungo za zamani na majina yaliyotumika, mf Kalubandika, Mwanameka, Moshi katika "usimchezee chatu", nahodha katika "Mv mapenzi" n.k.
Pia katika tungo za kisasa tunaona Mjomba katika "Salamu zangu" wa Irene Sanga (akimshirikisha Mrisho Mpoto na Elidadi Msangi).

Tuko pamoja....ninachotafuta ni ukweli katika utunzi.
 
Kuna tetesi huku mitaani kuwa wimbo wa "Ahmada umelewa" wa Bi Kidude amemwimba rais mstaafu wa vile visiwa vya karafuu. Tetesi hizi zinasema huyo mheshimiwa sana wa ule ukoo unaojulikana sana visiwani na nje ya visiwa alimwita huyo ajuza(kikongwe) katika kasri lake linalolindwa na manjagu, akamshauri aache pombe kwani inampunguzia heshima yake haswa vituko anavyofanya akilewa. Maana alisikia hako kabibi kanawakera watu kwa jinsi alivyo-cha-pombe.

Kibibi huyo baada ya kuambia hayo, kwakuwa anafahamu kuwa mshauri wake huyo ni cha pombe naye, akakakusudia na kisha kuitimiza azma yake ya kutunga songi hilo.

Hii ndiyo sababu wimbo huo haupigwi kunakovisiwa vya karafuu.

Naomba kujua zaidi.....

Umechemsha, huo wimbo si wa bi kidude, ameshirikishwa tu ndugu yangu. Huu wimbo ni wa Offside trick mazee
 
sijui kwa nini simpendi huyu bibi.

Una roho mbaya na ni asili ya kabila lenu kujiona na kudharau binadamu wenzako. nawe pia hupendwi pamoja unajiona mrembo...
Ulaaniwe ili nawe usipendwe zaidi ya usivompenda huyu ajuza!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu kwa hilo sikuungi mkono kabisa!!
punguza jazba,mweleweshe kwa lugha nyepesi
 
Una roho mbaya na ni asili ya kabila lenu kujiona na kudharau binadamu wenzako. nawe pia hupendwi pamoja unajiona mrembo...
Ulaaniwe ili nawe usipendwe zaidi ya usivompenda huyu ajuza!!!!!!!!!!!!!

hata wewe sikupendi . hata ukinilaani dua la kuku halimkuti mwewe . your very right kabila letu halina ma bibi kama huyu anayechoma fegi na kukukata mauno .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom