Tetesi, Watu wagombea maiti hadi kuchapana makonde.

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Kuna taarifa nimezipata muda mfupi uliopita kwamba kuna kabila fulani wanagombania maiti pale Muhimbili kuhusu aidha azikwe hapa Dar au asafirishwe kwenda Mkoani.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari, ni kwamba makundi hayo mawili yamefikia hatua ya kuchapana makonde hapo hapo Muhimbili wakati wakisubiri kuaga mwili wa merehemu na hadi sasa imeamuliwa mwili wa marehemu upelekwe mahakamani ili haki ipatikane.

Nimeelezwa kwamba vyombo vya habari kama ITV na TBC wapo pale pamoja na kundi la Ze Komedi.

Mwenye habari kamili tafadhali atujuze.
 
Mzee wewe ndio ulikuwa kwenye tukio ungetafuta haphapo info za kutosha kuja kutujuza
 
kashaija bana...

wewe ndio una habari, halafu tena unaomba habari

haya bana...
 
kashaija bana...

wewe ndio una habari, halafu tena unaomba habari

haya bana...

Hapana wakuu, mimi sikuwa hapo. Niko Bagamoyo, ila kuna jamaa yangu nilimpigia kuongea naye mambo mengine ndo akanambia habari hiyo, alikuwa anatokea hapo kupeleka mtoto hosp. Hakuwa na habari kamili.
 
poa poa mkuu... ngoja tukilizie, maana mwaka wa uchaguzi huu, kila kitu tunaogopa
 
Hivi watu wanaona ufahari gani kugombea maiti!!!! kuzikwa ni kuzikwa tu ingekuwa mimi ndio hakimu ningeamuru huo mwili wapewe wanafunzi muhimbili wafanyie mafunzo ama wangetunga sheria kuwa kundi ama watu watakao gombania maiti dawa ni kutoa kwenye vyuo vya madaktari ili wanafunzi wafanyie mafunzo sodhani kam hilo jambo la kugombania maiti lingekuwapo....
 
Ukiona hivyo ujue kinachogombaniwa si maiti bali ni burial permit make atakayeichukua ndo atapata uwezo wa kuprocess mirathi, watu wajanja hapo washalenga kwa manati mali za marehemu, stuka!
 
Hiyo taarifa nimeiona ITV. Shauri linaenda mahakamani kuamuliwa mwili ukibaki motuary. It is crazy!
 
Hao wanamatatizo ya akili kwani maiti akizikwa dar,moshi,pwani,musoma au kokote kule kundi la watu linapopataka huyo maiti haozi au ataendelea kupiga story wanadamu tubadilike
 
Back
Top Bottom