Tetesi: Waandamanaji wa deci wala mkong'oto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tetesi: Waandamanaji wa deci wala mkong'oto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ByaseL, Jun 17, 2009.

 1. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Habari kutoka Mahakama ya Kisutu ni kwamba wale waadamanaji wa DECI waoshinikiza serikali iharakishe kesi ya mabosi wa DECI wamepata kipigo toka kwa FFU. Mwenye taarifa za undani zaidi atufahamishe.
   
 2. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Jamani tuhabarisheni mliopo eneo la tukio kama kweli wana "Dance" wamepokea mkong'oto kutoka kwa FFU, maana hasara waliyopata kwa mbegu zao kuoza inatosha sana! Sidhani kama wanastahili kipigo tena kutoka kwa jeshi lililozoea kupiga "ramri"!!
   
 3. C

  Chaka Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Jamani wenye taarifa tuhabarisheni. Asubuhi niliona defender mbili zikiwa zimebeba hao FFU ndani yake pamoja na gari yenye maji ya kuwasha maeneo ya Nyerere Road. Please tuhabarisheni wenye taarifa.
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wapate tu mkong'oto kwani wanataka kuleta vurugu wakati sheria inafanya kazi yake,mahakama ndio itadhibitisha kama kweli walipanda mbegu na kwa utaratibu gani.
   
 5. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #5
  Jun 17, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Well, kwa mujibu wa taarifa ya habari ya saa saba mchana, iliyorushwa na TBC1, wanachama wachache wa DECI waliokuwa wakitumia haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni yao, nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo mchana, wamekamatwa na askari polisi kwa kile kinachoitwa "kuandamana" au "kukusanyika" bila kibali cha Polisi.

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amenukuliwa akisema kwamba pamoja na kuwapo kwa demokrasia nchini hapa, watu hao wanatambulika "kuandamana" kinyume cha sheria, kwa kuwa hairuhusiwi wao kukusanyika na kutoa maoni wakati kesi inaendelea Mahakamani, kwa kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wameingilia "uhuru" wa Mahakama, kwa "kushinikiza" hatua fulani zichukuliwe na Mahakama.

  Binafsi ninamshangaa Kova, kwa kuwa anaongea kana kwamba anaelewa vema mipaka iliyoainishwa na Katiba. Wanachama wa DECI, ambao ni Raia wa Tanzania, walikuwa na kila haki ya kukusanyika pale na kutoa maoni yao, kwani kwa upande wao, wanaamini kwamba hawakutendewa haki kwa viongozi wa DECI kukamatwa na kuwekwa ndani, kwa madai kwamba "wameendesha upatu kinyume cha sheria".

  Kesi hii ni (ingawa watu hawajajua umuhimu wake...) muhimu sana, kwani, hatima yake, iwapo viongozi hao wanne wa DECI watatiwa hatiani na kuhukumiwa kwenda jela, kesi nyingine ya msingi itazuka, ambayo Serikali itadai kwamba, kwa kuwa viongozi hao ambao wamepatikana na hatia na hivyo kufungwa gerezani walikusanya hizo fedha kinyume cha sheria, Serikali inakuwa na uhuru wa kutaifisha pesa hizo bila kujali nani atakayeathirika, kwa kuwa zilikusanywa kinyume cha sheria.

  Kuna tetesi kwamba Serikali (soma CCM) inajiandaa kutumia fedha hizo, takriban Shs. Bilioni 15, ambazo ziko kwenye akaunti mbali mbali za DECI, ambazo ni mali ya wanachama wa DECI, kwa ajili ya kuendeshea kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Kama kwa kupitia kesi inayowakabili viongozi wa DECI watafanikiwa kuzitaifisha pesa hizo, na kuzipeleka kwenye kampeni, basi huo ndio utakaokuwa mwiba utakaowapa jipu la kukizika rasmi Chama Cha Mapinduzi. Tayari wanachama wa DECI wameshaanza kampeni rasmi dhidi ya CCM, kwani mpaka leo hakuna taarifa yoyote juu ya pesa hizo.

  Narudi kusema, kama nilivyosema hapo awali: DECI haikufanya kosa, ila iliwasaidia Watanzania kujikwamua kiuchumi. Anayesema kwamba DECI ni "ponzi scheme" au mfumo wowote ule wa kitapeli aje na ushahidi kamili wa, (a) DECI inaendeshwaje na (b) ukiukwaji wa sheria uko wapi?

  Serikali, mpaka sasa, haijafafanua kosa lililotendwa na viongozi wa DECI ni lipi. Nimesoma miswada yote ya Sheria inayohusu Taasisi za Kifedha na Kibenki pamoja na Benki Kuu, sijaona sehemu yoyote inayozungumzia "Collective Investment Scheme" kama Benki Kuu ilivyoainisha kwenye madai yake dhidi ya DECI, kwamba DECI iliendesha "Collective Investment Scheme" (ndio upatu?) bila uhalali wa kisheria.

  Huu ni ufisadi tu kwa namna nyingine. DECI ilikuwa inawawezesha Watanzania kufunguka macho na kuachana na taasisi za kibenki ZA KIFISADI zinazowatoza raia wake RIBA KUBWA na kuwageuza kuwa WATUMWA wa kuwazalishia fedha lukuki kupitia mikopo.

  Kazi kwetu!

  ./Mwana wa Haki
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Umesema vizuri mwanahaki lakini tatizo la wadanganyika wengi ni wepesi wa kusahau. Unakuta kiongozi yule yule awaliyempa madaraka na akashindwa kuwatumikia kwa miaka mitano, akishaona uchaguzi umefika anakwenda kuwagawia khanga, kofia, vitenge, t-shirts halafu wanapewa wali au pilau basi kwisha kazi, watu wanaanza kuimba nyimbo za kumtukuza.Au mtu anadanganyika anauza shahada yake kwa shilingi 1000 au 2000.Hii ni aibu sana kwa kweli.Kama wadanganyika wakiwa makini kidogo tu, mwaka 2010 baada ya uchaguzi CCM watakuwa kwenye benchi la vyama vya upinzani. Ni suala la umakini kidogo tu kwa wadanganyika, kwa sababu ni mambo mengi sana ambayo serikali za ccm zimekuwa zikiyafanya ambayo yanadhihirisha kwamba wamechoka kuongoza, wanahitaji kufanyiwa substitution, ni bahati mbaya tu kwamba kocha(wadanganyika) hajakuwa na maamuzi ya kumpeleka benchi ccm.
  Lakini tusichoke iko siku mambo yatanyooka tu.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Aaaaaaaaargh
  Tanzania inachosha sana
  Tujitahidi kuwaelimisakina KOVA kwamba Uhuru si kama wanavyoutafsiri wao.
  Wasidhani kwamba nafasi walizo nazo ni sawa na miungu watu.

  Aaaaargh akili imenitoka kidogo hapo.
  ngoja nikale kahawa labda nitatulia kidogo
   
Loading...