Tetesi: Viongozi UKAWA kukutana na wananchi viwanja vya Mnazi Mmoja

Status
Not open for further replies.

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Kuna taarifa nimepenyezewa na mtu kuwa viongozi wa ukawa muda mfupi ujao watakuwa viwanja vya mnazi mmoja kuzungumza na wananchu,

Kama kuna mwenye uhakika na taarifa hii atujuze tuanze kujongea maeneo hayo
 
Kama ningekuwa na uwezo wa kuwashauri UKAWA, ningewashari wakubali matokeo.

Huwezi kuoa siku hiyo hiyo na kutarajia kupata mtoto siku hiyo hiyo na kumwandikisha shule siku hiyo hiyo. Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha, EL amewasaidia kuongeza idadi ya % ya kura za Urais huenda hata wabunge wa viti maalum wataongezeka, hiki sio kitendo cha kubezwa, ndege aliyeko mkononi ni bora zaidi aliyeko juu ya mti.

Kitendo cha UKAWA kuungana katika uchaguzi huu kimewapatia nguvu na wamefanya vizuri sana ikilinganishwa na chaguzi zilizopita.

Hata hivyo, imeshuhudiwa muungano huu kutoheshimiwa miongoni mwao wenyewe kiasi cha kusimamisha wagombea wawili kutoka vyama shirika kitu ambacho kimewachanganya baadhi ya wapiga kura kutoamini kama kweli ni muungano wenye tija, na wengine kuchanganya kura na kusababisha wagombea kushindwa; Katika hali kama hii, UKAWA wanapaswa kuchukua changamoto zilizojitokeza na kuanza kuzifanyia kazi kuanzia leo ikiwa ni pamoja na kuimarisha Muungano wao kwa malengo maalum.

Kitendo cha kugomea matokeo hakitakuwa na tija kwa sababu Rais akishatangazwa ataanza kutumia ngivu zake za Urais nao kuendelea kulalamika bila kuhudumia wapiga kaura wao kama ilivyotokea mwaka 2010 walivyogoma kutomtambua Mhe. JK, lakini mbona JK amekuwa Rai hadi leo.
 
Hahaa mim ntaenda endapo watoto wa kingunge mbowe mbatia mdee[najua hana mtoto huyu alete ndugu zake] sumaye na lowassa pamoja na mkewe hapo na mm ntajongea paleeee mnazi mmojaaa
 
Hawa watu WA ukawa wanafikiri kila mtanzania yupo upande wao majinga sn kuna watu hawana vyama tena ni wengi sn hebu watuachie Aman yt

Itafika time wanachi wenyewe ndio watapambana na hili group la ukawa Sasa cjui itakuwaje? Hapo ikifikia.
 
viongozi wanasahu kama kuna Mungu jamani mimi yangu macho ila sijui kama nitapiga tena kura kwasababu watu wanafikiri nchi ya kwao ila nchi ni ya watanzani kiukweli tanzani hakuna democracy nimechoka namuachia Munguu
 
nani aende kupigwa virungu huko

Wake na Watoto wa Lowasa,Kingnge,Mbowe,Mbatia,Sumaye,Mnyika na viongozi wengine watakuwepo? Au watakuwepo watoto wa walalahoi tu ili likitokea la kutokea watoto wa walalahoi waumie wakati watoto wao wako salama majumbani au ulaya?
 
hAO VIONGOZI WA UKAWA WAJE NA WATOTO WAO NA NDUGU ZAO PIA WASIJE KUWAPONZA WATOTO WA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI WAO KIKINUKA WANASEPA ZAO ULAYA.
 
Nafikiri ni wakati wa house arrest kwa hawa watu wanaotaka kufanya uhaini! Demokrasia imechukua mkondo wake, nini madai yenu ya msingi?

Kwamba Zanzibar uchaguzi usirudiwe au mmeibiwa kura? Hadi sasa hamna ushahidi wowote wa chochote!

Lubuva anajua kuwa kura za NEC Zanzibar ni halali, na kwa bahati mbaya Zanzibar haiendeshi muungano na bara haiwezi kuingilia serikali ya mapinduzi!

Mgogoro wa Zanzibar kuingiliwa na kikwete ni mgogoro mkubwa sana wa kikatiba kuliko huo wa NEC na ZEC! Rumours huwa haziongozi nchi, kama Lubuva akifuta matokeo then uchunguzi ukionesha kuwa mwenyekiti wa ZEC alirubuniwa na smz lubuva yeye anasema nini?

Acheni unyumbu fununu haziwezi kutengeu shughuli halali za JMT! Kaskazini vs Tanzania we unafikiri nani atashinda?
 
Natazama TV hapa nikimuona Mbowe,Sumaye,Lowassa na family zao pale mnazi mmoja naibuka sasa hivi hapo,lakini kutaka sisi tupambane na polisi haiwezekani hiyo
 
Nafikiri ni wakati wa house arrest kwa hawa watu wanaotaka kufanya uhaini!
Demokrasia imechukua mkondo wake, nini madai yenu ya msingi?
Kwamba Zanzibar uchaguzi usirudiwe au mmeibiwa kura?
Hadi sasa hamna ushahidi wowote wa chochote!
Lubuva anajua kuwa kura za NEC Zanzibar ni halali, na kwa bahati mbaya Zanzibar haiendeshi muungano na bara haiwezi kuingilia serikali ya mapinduzi!
Mgogoro wa Zanzibar kuingiliwa na kikwete ni mgogoro mkubwa sana wa kikatiba kuliko huo wa NEC na ZEC! Rumours huwa haziongozi nchi, kama Lubuva akifuta matokeo then uchunguzi ukionesha kuwa mwenyekiti wa ZEC alirubuniwa na smz lubuva yeye anasema nini? Acheni unyumbu fununu haziwezi kutengeu shughuli halali za JMT!
Kaskazini vs Tanzania we unafikiri nani atashinda?

Shikamoo
 
Nafikiri ICC nao wapo.

Wasidhani kuwa ICC wanashughulika na wakuu wa serikalini tu, mtu yeyote anayeleta vurugu zinazoweza kusababisha maafa anakuwa subject wa kushtakiwa ICC Uholanzi.

Mpata dakika hii hao kina Lowasa wameshindwa kuonyesha hata jimbo moja ambalo kura zilizotajwa na Tume ya Uchaguzi zinatofautiana na zile zilizowekwa signature na mawakala.

Halafu wanasema wameibiwa, kivipi? Kosa ni polisi kuwakamata wale vijana walioandaliwa kuchakachua matokeo. Yaani ukizuiwa kuiba unalalamika umeibiwa wewe.

Shame on them.
 
Umenena vyema,wasitusemee mioyo kama kwenda tutaenda kwa sababu n cc na c wao
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom