Tetesi: Nini kina msibu Former IGP Mahita...??

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
30
Kuna tetesi kwamba Mahita yupo kwenye jela ndogo (jela ya nyumbani) kwa sababu yupo chini ya uangalizi kwa kuwa alishirikiana na baadhi ya RPC na kina Zombe na kusupport mitandao ya majambazi hapa nchini wakati wa utawala wake.

Mpashaji wa habari hizi anasema Bwana Zombe na mahita walishirikiana na mtanado wa majambazi kuiba baadhi ya mali za wakazi wa Dar na mikoani.

Mtoa habari huyo alisema kesi zote za ujambazi za uvamizi wa mabank na taasisi nyingine za fedha hapa nchini kwanzia 1997 hadi 2005 yeye na bwana Zombe walipata mgao. Pia mtoa habari huyo anasema baadhi ya account zake zilizoko nchini na nje ya nchi zinachunguzwa.

Mtoa habari huyo alipata kiburi zaidi wakati taarifa za ufisadi zilipokuwa zinamfikia na yeye akaongeza kasi ya kuchota kupitia mtandao wake ili kama ataondoka madarakani aweze kuwa na chochote na kama wanasiasa walivyokuwa wanafanya.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kutaka kusafisha fedha haramu alizokuwa nazo aliamua kujenga msikiti mjini morogoro ambao ndio chanzo ch uchunguzi unaoendelea kujua alipata wapi hela za kujenga msikiti, kununua ranchi, kununua baadhi ya nyumba dar n.k wakati mshahara wake na marupurupu yake hayawezi kufikia gharama alizotumia.

Pia mtoaji nyeti hizo alisema Zombe amecooperate vizuri na wachunguzi hao na kutoa nyeti za jinsi mtandao huo ulivyokuwa unafanya kazi kuanzia ujambazi, uchapaji wa hela feki, utoaji wa hati za kusafiria, madawa ya kulevya, n.k

Msiniulize sources but will keep on posting as I get information
 
nimeweka kwenye tetesi kwa sababu maaalum nitaomba ihamishwe muda muafaka ukifika
 
Bowbow..haishangazi huyo alianza ufisadi siku nyingi tangu akiwa RPC kilimanjaro inasemekana ndio muanzilishi wa "CHURA" kule horiri...
 
hapana hii sio tetesi ila ni UDAKU........samahani lakini ni mtazamo wangu sitaki malumbano
 
Bowbow..haishangazi huyo alianza ufisadi siku nyingi tangu akiwa RPC kilimanjaro inasemekana ndio muanzilishi wa "CHURA" kule horiri...

Wakati wa beer za stella hatoi....kutokea kenya hahahahahaha
 
.........Alionekana siku ya Muungano..au alipewa kibali maalum???hao RPC's vipi mbona wapo tu pale Makao Makuu Polisi?wamepewa ma desk wanasoma magazeti tuu??
 
Tutasikia mengi sana maana pia kuna Ma -RPC ambao hadi leo wako mikoani lakini walikuwa ndiyo wajasiriamali wake au vitendea kazi vyake. Na inasemekana kulikuwa na tofauti fulani kati yake na huyu IGP wa sasa Said Mwema na ndiyo kisa akatolewa U-RPC Mbeya na kupelekwa Interpol Kenya, wenye data mwageni zaidi.
 
hao walikuwa noma hata watu wao wakiiba warehouse/godown kubwa walikuwa wanakipewa escot ya king'ora.Huyo bwana Mahita alikuwa na yard ya magari ya wizi ambayo polisi wakikusanya magari ya wizi kutoka kwa wezi yalikuwa yanarudi kwake inakuwa kama ndio mwenye nayo.
Thats the story
 
Kuna taarifa kwamba baadhi ya Askari wasomi enzi za Mahita ikiwa walionekana kuwa ni challenge kwake basi adhabu yao ilikuwa ni kuwapeleka mbali na Dar kama vile Mtwara, Lindi ambako kwa namna fulani watajuta kutofautiana nae.
 
bowbow, kazi nzuri sana mazee.unajua huyu jamaa wakati wa utawala wake, haki ya mnyonge ilikuwa ngumu sana.nakumbuka alikuwa na kijana wake anamuita chiko(RPC kilimanjaro).walikuwa marafiki sana mpaka nikawa na wasiwasi na urafiki wao.kipindi chake ndio muda ambao asikari walikuwa wanakodisha silaha kwa majambazi,bank zinaibiwa, raia wasio husika wanakamatwa kwa uonezi.
wakuu huyu jamaa anautajiri usiosemekana,tembeleeni moro mjionee wenyewe hekalu zake na ile anayoishi kule forest hili.
ni vizuri huyu jamaa ashughulikiwe ili iwe fundisho kwa viongozi wengine wenye tabia kama yake.
mwanza ndio balaa, raia wanauliwa na kuteswa ndani ya nchi yao.fatilieni yanayotokea ndani ya ziwa victoria, sio kwamba RPC wa mwanza hajui lakini ndio hivyo.............
 
Bowbow umefanya kazi nzuri saana huyu jamaa wananchi walisha anza kumsahau.Ule msikiti wa MORO ni mkubwa sana sijui kama kweli alijengea mshahara wake au masurufu sidhani.Alafu ilisemekana jamaa anamiliki ZAHANATI sijui wapi huko walikuwa wanalinda FFU alafu jamaa nasikia ana nyumba kila mkoa na MA-RPC ndo wakusanyaji wa kodi ana mashamba balaa na ilisemekana alikuwa anatumia MA-RPC kukusanya mazao mikoani huku achilia mafungu ya wafanyabiashara wanayo toa ili kulindwa si mnajua tena wafanyabiashara nao kwa dili chafu ndo wenyewe kwa hiyo RPC anapoozwa na kiasi kingine kinakusanywa kwa ajili ya mzee IGP dah jamaa huyu nae ana CENT kibao.Inabidi iundwe tume.Hii habari si tetesi ni ukweli ukitaka kujua kama una rafiki yako AFANDE basi muulize atakupa full stroy wala si UDAKU ni tru story jamaa kachuma sana.
 
Yote tisa, kumi ni kitendo cha kuwajengea Hoteli wafanyakazi wake wanaokwenda shambani ambapo baada ya kazi ngumu hujiburudisha kwa mvinyo safi huku wakifaidi kazi ya Sir Godi ya kuumba warembo wanaoishi jirani na Shamba lake lililopo kando ya Barabara ya Dom-Moro.
 
Huyu jamaa namiliki mtaa mzima pale Gongolamboto; tena mtaa wenyewe umepewa jina lake.

Kule Morogoro mjini ametoa michango mingi sana kwenye shughuli za kijamii akijaribu kutafuta ubunge mwaka 2005 lakini sisiemu wakamfisadi akatupwa nje.
 
Kuna tetesi kwamba Mahita yupo kwenye jela ndogo (jela ya nyumbani) kwa sababu yupo chini ya uangalizi......
Does anyone really think this former IGP is daft enough to accept anything near this? Hivi kuna sheria inayomzuia mtu kutoka ndani kwake? As far as I know, anaweza kuzuiwa kusafiri tu vinginevyo huu ni uonevu na kinyume na haki za binadamu.
Having said that, lawama zote za madudu yote ya Mahita anayestahili kubebeshwa ni Mkapa. Mkapa ndiye aliyemteua kwa kigezo tu cha uwezo wake wa kuwathibiti wapinzani, esp. Mrema, japokuwa kulikuwa na watu wengine ndani ya jeshi la polisi waliokuwa na uwezo kuliko Mahita. Alikuwa anajua maskendo yote ya Mahita lakini hakuchukua hatua zozote.
 
Hata Kwenye Mazishi Ya Brother Dito Alikuwepo.

Sasa Kifungo Gani Cha Ndani Hicho? Au Unakusudia Ndani Ya Nchi Asitoke Nje Ya Nchi?
 
kikwete aanza kumchunguza huyu fisadi marijini kwanza na utoe ukumu tumeshachokana kuchunguza watu hakuna kinachoendelea
 
Huyu jamaa hata haya majambo hakuwa nyuma!

Mahita: Soo lake laibuliwa tena upya
2008-05-12 18:44:18
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Baada ya kuwa kimya kwa kitambo sasa, hatimaye lile soo la kudaiwa kutelekeza mtoto linalomkabili aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bwana Omar Mahita limeibuliwa upya tena.

Kwa mtaji huo, soo hilo litaanza kuunguruma kortini kesho.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Alasiri imezipata toka katika mahakama ya wilaya Kinondoni ambako shauri hilo la madai limepelekwa, ni kwamba litaanza kusikilizwa baada ya pande zote mbili kukubali kuwa lisikilizwe na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya.

Awali, kesi hiyo ilikuwa kwa Hakimu Mkazi Kisutu kabla ya kufutwa mbele ya Hakimu Pellagia Khadaye aliyemtaka mdai kufungua kesi yake kwa Hakimu wa Wilaya.

Kabla ya hapo, wakili wa mdaiwa Mahita, Bw. Charles Semigalawe, aliwasilisha madai ya kupinga kesi hiyo kusiklilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ambapo baada ya kuahirishwa mara kadhaa, hatimaye makubaliano ya pande zote yalifikiwa na sasa kesi hiyo itaanza kuunguruma kwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kesho, kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Katika kesi hiyo, mdai ni Bi. Rehema Shaaban, anayeeleza kuwa wakati alipokuwa mtumishi wa ndani wa Bw. Mahita, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi wake huyo (Mahita) na hatimaye akapata ujauzito.

Anadai kuwa baada ya hapo, Bw. Mahita alimtaka arejee kwao Kondoa na kwamba atakuwa akimpa matunzo.

Ilidaiwa zaidi kuwa baada ya kuwa kwao, mdaiwa Mahita alikiuka makubaliano yao na hivyo Rehema na mwanae wa kiume wakakosa matunzo.

Kutokana na kutelekezwa huko, Bi. Rehema anaiomba mahakama imuamuru Bw. Mahita amtambue mtoto aliyemtelekeza kuwa ni wake na pia, alipe fidia kadhaa ikiwa ni pamoja na kulipia matunzo ya mtoto toka alipomzaa hadi pale mahakama itakapotoa hukumu ya shauri hilo.

SOURCE: Alasiri
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom