Tetesi: Ndege mbili zapotea Kilwa

Status
Not open for further replies.

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,169
Kuna taarifa zilizothibitishwa na Mamlaka ya usafiri wa Anga Nchini (TCAA) kuwa ndege mbili ndogo zimepotea wilayani Kilwa.
Moja ya ndege hizo, iliyokuwa inatoka Dar kwenda Kilwa ilikuwa na watu 17 ndani yake na nyingine iliyokuwa inatoka Kilwa kuja Dar ilikuwa na watu wanne.
Ndege moja ya South Afrika iliyokuwa inatoka Dar kuelekea Msumbiji imeripoti kuyaona mabaki ya ndege katika moja ya vuisiwa vidogo eneo la Kilwa. Ndege mbili za jeshi zimeshatumwa kwenda kufuatilia hali hiyo
 
..........................................................................................????????
 
Any fisadi inside ? Please God let some of them to be inside !
 
Kuna Taarifa Kwamba Kuna Ndege Mbili, Moja Ya Abiria Na Ingine Ndog, Zimepotea Lro Asubuhi. Taarifa Zaidi Baadae

Macinkus
 
Kuna watu wameokoka lakini kadhaa wengine wamefariki. Identities zao bado hazijawekwa wazi
 
Ooh God!Leo tena ndege zimepotea?Hizi hitilafu zinatokea tu ndege zikiwa angani?Mbona hali ya hatari sasa
 
Tunatanguliza Pole kwanza kwa wale wote waliopoteza maisha na majeruhi tunawaombea ili mungu awaongeze na kuwapa Afya njema na kuwaponya Majeraha hayo
 
Pole kwa wafiwa.

Lakini pia inatakiwa ndege ndogo zote Tanzania zifanyiwe uchunguzi wa kina inawezekana kuna matatizo ya kiufundi. Haiwezekani ndege mbili zote zikapotea siku moja. Labda tutafute kingine tena zilitengenezwa wapi? na lini? na zilinunuliwa lini?
 
Nadhani niliwahi kuona kwenye Discovery Channel Mayday ndege mbili zilizokuwa zinaenda opposite direction kukutana kwenye altitude moja, na I guess U can predict what has happened in Kilwa is almost identical yaani ajali ya kugongana kwa ndege hewani.

Tusubiri taarifa zaidi.
 
nyingi ya ndege ndogo zilizopo bongo zimezeeka sana,kama yalivyo magari mengi pale Dar(mitumba) na mabasi yetu (malori chesis),je radar yetu ni mpya au nayo used?,vipi leseni na service zake nani anajua?

Eeee Mungu tusaidie walalahoi na ajali hizi.
 
Waungwana poleni kwa mshituko uliotupata.
Kilichotokea ni kuwa TCAA, SUMATRA na wadau wengine walikuwa waafanya MAZOEZI kuona utayari wao wa kushughulikia matatizo ya ajali za ndege.
ILIKUWA NI MAZOEZI TU, HAKUNA AJALI YA KWELI ILIYOTOKEEA kwa mujibuw a taarifa ya TCAA ya hivi punde.
Tangu asubuhi zilipopatikana habari hizi nimekuwa nikiwasiliana na wafanyakazi wa TCAA na wao walikuwa hawajui kuwa ilikuwa ni ajali ya kupanga.
Kwa mujibu wa Taarifa ya mama Munyagi, Mkurugenzi wa TCAA, zoezi hilo ni kwa mujibuw a ICAO regulations.
Hivyo tutulize mioyo, hakuna ajali iliyotokea
 
mmmh ......haya bwana ....wengine tulikuwa tushaanza kuvuta vitabu vya sala tena!
 
hii ilikuwa ajali ya ndege ya kugushi. yaani yalikuwa mazoezi yaliyopangwa tu.

macinkus
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom