Mi pia nimesikia habari hizi kuwa Mpendazoe alikua kamwacha Makongoro kura 80 lakini Mako kakimbia na masanduku. Sasa habari hizi si rasmi ni vizuri wenye taarifa watupe kwa kina kuliko kuandika tu "Ni kweli"
Mtu aliyekuwa akishiriki zoezi la kuhesabu kura (ni afisa mtendaji wa kata) alinitonya jana kuwa mpaka wanawasilisha masanduku ya kura kwenye kituo cha majumuisho, 'Mzee wa Nyantare' alikuwa kagaragazwa.
Ishu ya Mpendazoe na Makongoro kudakwa sio utata...
Ni kweli, hata Wapo Radio wameripoti asubuhi moja kwa moja toka Buguruni kuwa Makongoro alishashindwa, na alikuwa polisi akihojiwa kwa kukwapua mabox ya kura, (ambayo awali mtendaji alishasema 'yalipotea') na ukweli wamesema baadaye Mtendaji na polisi waliyaweka ktk tax ili yapelekwe tena Shule ya msingi Buguruni kwa majumuisho tena ila kwa Masharti ya kutomruhusu mtu yeyote kuingia ktk hiyo tax, mawakala wakagoma (wakijua kuwa ndani ya tax kulikuwa na kura zilizokwishapigwa walizotaka kujaza ndani ya mabox), ndipo walipogoma tax haikuenda. Hadi saa 2:00 asubuhi, mtangazaji wa Wapo alisema polisi haijakubali kutoa ufafanuzi wa Makongoro, hatua zilizochukuliwa na Mabox faki yamefanywaje...
Habari ndio hiyoo.....Ukombozi unakandamizwa na mafidhuli...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.