Tetesi: Mkosi wa Simba ni laana za rambirambi za Mafisango! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tetesi: Mkosi wa Simba ni laana za rambirambi za Mafisango!

Discussion in 'Sports' started by Mdakuzi, Jul 30, 2012.

 1. Mdakuzi

  Mdakuzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,748
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Mashabiki wengi wa soka walishangazwa na uwezo mdogo uliooneshwa na klabu ya soka ya Simba na kujikuta wakitolewa mapema katika michuano ya kombe la Kagame huku ikidhalilishwa na klabu ya Azam FC.
  Kwa kipindi kirefu sasa, mashabiki wa soka nchini wamekuwa wakiilalamikia Simba kwa kutofikisha rambirambi ilizokusanya kwa ajili ya aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo marehemu Patrice Mafisango aliyefariki dunia kwa ajali ya gari.
  Lakini mpaka sasa hakuna kiongozi yeyote wa Simba aliyejitokeza hadharani kueleza kiasi kilichopatikana cha rambirambi hizo huku wakiendelea kuwa nazo bila kuzifikisha kwa familia ya mchezaji huyo.
  Hali hii imefanya wadau wa soka kudai kuwa, mkosi iliyoupata Simba hivi karibuni unatokana na kuchikichia rambirambi hizo bila kutoa maelezo yoyote.
  Kwani ijulikane kwamba, Simba ilishasajili wachezaji kadhaa kwa pesa nyingi kweli, kisha ikalazimika kuwaacha ndani ya siku chache kutokana na kiwango kibovu walichoonesha kwenye michuano ya Kagame.
   
Loading...