Tetesi, Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja kaachia ngazi??

Haya yashatimia sasa WALETENI akina JULIO na KIBADENI.....nyie viongozi ni MAMLUKI wa KANDAMBILI FC......mnatuharibia timu
 
bora , nimefurahi alivyojiondoa kuliko kubaki na aibu



mayanja namkubali kuliko omog
mayanja ni kocha mpambanaji sana
 
Huyu jamaa ndiye alikuwa muhimu pale kwenye bench lao la ufundi! Sare na mtibwa imewachanganya sana! Hata hivyo wana bahati sana isingekuwa goli lao dk ya 95 wangefukuzana wote!
 
Kocha Jackson Mayanja ameamua kuachana na klabu ya Simba na kurejea kwao Uganda.

Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo yake binafsi.

“Ni matatizo ya kifamilia lakini suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa,” alisema.

Lakini habari kutoka Simba zimeeleza kuwa sasa wako katika hatua za mwisho kuvunja mkataba wake baada ya kukubaliana naye kutokana na uamuzi wake huo.

Muungwana Blog
Duu hiki kifaa kinaondoka! Ikumbukwe kuwa Kocha Mayanja ndiye aliyeibadili Simba kwenye uchezaji mpaka ikaachana na kutoa sare mfululizo zaidi ya michezo minne. Kama ni kweli hili ni pigo kwa Wanachama na Washabiki wa Simba. Bora angeondoka Joseph Omog kwa kweli.
 
Ukweli kuhusu Mayanja kafukuzwa Simba

Wednesday , 18th Oct , 2017
Na Elbogast Myaluko
Kocha msaidizi wa Simba Mganda Jackson Mayanja amekanusha taarifa za kutimuliwa ambazo zinasambaa nchini na kudai kuwa si za kweli kwani hana taarifa yoyote rasmi kutoka kwa uongozi.


MAYANJA%201.jpg

Mayanja amesema hajui taarifa hizo zinatoka wapi kwasababu sio za kweli na yeye anaendelea na kazi kama kawaida. “Sijafukuzwa naendelea na kazi yangu kama kawaida”, amesema Mayanja.

Aidha Mayanja amesema hakuwepo nchini kwa siku kadhaa zilizopita kwasababu alisafiri kwenda kwao Uganda ambako alikuwa na mambo ya kifamilia na tayari ameshayamaliza na amerejea kuendelea na kazi.

“Nilienda nyumbani Uganda mara moja kulikuwa na matatizo ya kifamilia sio kwamba nimefukuzwa, ndio mana nimerejea kuendelea na kazi yangu na uongozi wa klabu haujanipa taarifa yoyote, sasa sijui hizo taarifa zimetoka wapi”, ameongeza Mayanja.
 
Ukweli kuhusu Mayanja kafukuzwa Simba

Wednesday , 18th Oct , 2017
Na Elbogast Myaluko
Kocha msaidizi wa Simba Mganda Jackson Mayanja amekanusha taarifa za kutimuliwa ambazo zinasambaa nchini na kudai kuwa si za kweli kwani hana taarifa yoyote rasmi kutoka kwa uongozi.


MAYANJA%201.jpg

Mayanja amesema hajui taarifa hizo zinatoka wapi kwasababu sio za kweli na yeye anaendelea na kazi kama kawaida. “Sijafukuzwa naendelea na kazi yangu kama kawaida”, amesema Mayanja.

Aidha Mayanja amesema hakuwepo nchini kwa siku kadhaa zilizopita kwasababu alisafiri kwenda kwao Uganda ambako alikuwa na mambo ya kifamilia na tayari ameshayamaliza na amerejea kuendelea na kazi.

“Nilienda nyumbani Uganda mara moja kulikuwa na matatizo ya kifamilia sio kwamba nimefukuzwa, ndio mana nimerejea kuendelea na kazi yangu na uongozi wa klabu haujanipa taarifa yoyote, sasa sijui hizo taarifa zimetoka wapi”, ameongeza Mayanja.
Afadhali kama sio kweli!
 
Wala sijashtuka maana nilijua tu lazima kocha wa simba mmojawapo au wote (ni suala la muda tu) kung'atuka
 
GENTAMYCINE hana hizi taarifa?

Leo nasema ukweli na ' nafyatuka ' hivyo kama wana Simba Sports wenzangu ' mtanichukia ' sawa / powa ila sitobakisha kitu kwakuwa sipendagi Ujinga na Unafiki.

Sijawahi kuona Wapenzi wa Mpira ' Mapopoma / Wapumbavu ' duniani kama baadhi ambao wanapatikana katika Klabu yangu ya Simba. Hizi chokochoko zote nimeanza kusizikia Kitambo sana na kilichosababisha yote haya ni Kitendo cha Makocha Omog na Mayanja kutomkubali Nahodha wa zamani wa Simba SC Kiungo mkabaji Jonas Gerald Mkude kwakuwa wao ' Kiufundi ' waliona kwa sasa haendani na mfumo wao isipokuwa kuna mechi fulani fulani tu wangekuwa wanamtumia kutokana na uwezo wake.

Kilichofuata hapo ni Kitendo cha Mkude ambaye kiukweli ana ' Marafiki / Washkaji ' wengi ndani ya Simba SC na ambao pia wana ' ushawishi ' mkubwa kwa Uongozi kuwalalamikia na kuwachochea wamchukie Kocha Omog na mwenzake Mayanja kwakuwa tu wanamweka ' benchi ' huku akidai kuwa wana ' chuki ' nae binafsi.

Baada ya Wanasimba fulani fulani ambao ni ' Wapumbavu / Mapopoma ' kabisa kuona kwamba Mkude hachezeshwi wakaanza kumuonyesha Omog na Mayanja chuki za waziwazi huku baadhi ya Viongozi wa Simba SC na wa Kamati ya Usajili wakianza kumuingilia katika upangaji wa Timu na hadi kumtishia kuwa watamfukuza hali ambayo ilianza hata kuathiri ' Saikolojia ' ya Makocha hao wawili ambao Mimi kama Mwanamichezo, Mdau mzuri tu wa Michezo hasa Soka na pia Mchezaji wa Soka wa Kiwango changu bado sijaona tatizo lao lolote la Kiufundishaji au hata upangaji wa Kikosi.

Mishabiki ' Mipopoma ' ya Simba inamlaumu Omog lakini hapo hapo wakiwa wamesahau kwamba 90% ya Kikosi cha sasa cha Simba SC hakusajili Yeye Omog bali ameletewa na Viongozi wa Simba SC ambao hujifanya pia kama ndiyo sehemu ya Benchi la Ufundi la Simba na hata Wachezaji wengi waliosajiliwa Simba SC hawakuwa ' chaguo ' la Kocha Omog ila ilikuwa tu ni ' Sifa ' za Viongozi hao na ' Viherehere ' vyao.

Hivi kama kweli Wewe unaujua mpira hasa Simba SC ilikuwa ni ya Kusajili Wachezaji hawa Watatu ambao ni Pancha / Wagonjwa kama Shomari Kapombe, John Bocco na Said Dunda? Hivi kulikuwa na haja gani ya kuachana na Kipa aliyetusaidia kabisa Daniel Agyei na ambaye alikuwa akifanya vyema tu kama angebaki na kuwa pamoja na Aishi Manula kungekuwa mafanikio makubwa katika hiyo nafasi?

Kwa ' Utaalam ' wangu mkubwa wa Mpira Simba SC ilihitaji tu Wachezaji Wawili muhimu hasa Emanuel Okwi na Haruna Niyonzima na siyo ' Lundo ' la Wachezaji ambalo Kamati nzima ya Usajili ilitujazia ambayo sasa hao hao ' Magalacha ' ndiyo wamekuwa ni sehemu ya ' mgawanyiko ' mkubwa ndani ya Wachezaji wa Simba SC hadi sasa kumekuwa na ' mgawanyiko ' mkubwa baina yao hali ambayo ' Kiufundi ' ni tatizo kubwa.

Hivi kulikuwa na haja gani Simba SC kuachana na Mshambuliaji ambaye Mimi naamini alitusaidia na angetusaidia sana kama angeendelea kubaki Fredrick Blagnon na kuendelea na Mshambuliaji wa ' hovyo hovyo ' Laudit Mavugo? Fredrick Blagnon alikuwa ana uwezo wa kupambana na hadi kuwatisha Mabeki na kuogoa kupanda mbele tofauti ya Laudit Mavugo ambaye ' anazunguka zunguka ' tu utafikiri inzi kabeba ' Kinyesi ' cha chooni sasa anafurahia.

Sishangai ndiyo maana hata Beki wa Yanga na Rafiki yangu mkubwa ndani ya Yanga Kelvin Patrick Yondani kila mara amekuwa akisema kuwa katika kila mechi za Simba na Yanga huwa akiona Simba imempanga Laudit Mavugo huwa anafurahi mno na anakuwa hana wasiwasi kwani huwa anampiga mkwara / biti na kumfanyia vitendo vya ' Kisela ' hadi Mavugo anamuogopa na kila mara anamuamkia tu ' Shikamoo Kaka ' na anaishia tu kutoka mchezoni na kucheza vibaya.

Tunajua kwamba Uongozi na hasa Kamati ya Usajili ya Simba SC haiwataki akina Omog na Mayanja kwakuwa ' Makocha ' hao hawataki kupangiwa Kikosi hali ambayo imekuwa ni ' Kero ' kwa hao Watu wa Kamati ya Usajili ya Simba ambayo baadhi ya Wajumbe wake huwa wanakuwa na Wachezaji wao wanaotaka / wanaolazimisha wapangwe ili wawe wanakula nao 10% ya Posho na Mishahara yao hivyo ' misimamo ' ya hawa Makocha Kwao imekuwa ni ' Kipingamizi ' kikubwa na wakaanza kuunda ' zengwe ' ili Wanachama / Mashabiki / Wapenzi wawachukie.

Ilifika muda hadi hao hao Wajumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba SC baada ya kuona Kocha Omog na Mayanja bado wamekomaa na wanaonyesha ' Ueledi ' wao ( Professionalism ) wakaanza sasa ' Kuwashawishi ' Wachezaji ' Waandamizi ' wacheze chini ya Kiwango ili Timu isipate matokeo mazuri kisha Mashabiki wakasirike na wawakatae hao Makocha na wao wapate ' Kisingizio ' cha ' Kuwafukuza ' na hatimaye wawalete Makocha wao ambao ' watawatawala ' kisha watakuwa wanawashinikiza ili wawapange Wachezaji wao wa 10% na hatimaye maisha yaende.

Mpira uko Ulaya na Latin America tu Afrika na hasa Tanzania kuna Ujinga / Ungumbaru na Upumbavu / Upopoma mtupu!

GENTAMYCINE ni kama Bahari ambayo siku zote huwa haikai na Uchafu. Mwanamume tayari nimeshatema ' Nyongo ' yangu.

Nimemaliza.
 
Kuna jamaa humu siku ingine anajifanya mshabiki mkubwa wa Yanga siku ingine ni mshabiki wa mikia. Siku ingine akiamka ovyo anakuwa mnyarwanda siku ingine Mtz yaani km wimbo wa Jay Mo mvua na jua.
 
Kuna jamaa humu siku ingine anajifanya mshabiki mkubwa wa Yanga siku ingine ni mshabiki wa mikia. Siku ingine akiamka ovyo anakuwa mnyarwanda siku ingine Mtz yaani km wimbo wa Jay Mo mvua na jua.
:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D Nimecheka sana...
 
Back
Top Bottom