Elections 2010 TETESI: Eti wabunge wa CHADEMA wamegoma kuchukua milioni 90 za kununua gari

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Wakuu,hizi taarifa ni za kweli?:Kwamba wabunge wetu wa Chadema wameziktaa sh milioni 90 walizopangiwa kuchukua ili kila mmoja anunue gari.Wabunge wamefikia hatua hiyo ili kuonesha uzalendo walionao kwa Taifa ,kwamba hawawezi kuchukua kitita hicho ili hali ya uchumi wa nchi yetu ni mbofu mbofu.

Kwa mjibu wa taaarifa hizo ni kuwa wabunge hao wanataka angalau wapate sh milioni 40 au 50 kila mmoja na zilizobaki zitumike kwenye maendeleo ya elimi,afya nk

nimefuraishwa na hatua hiyo ya wabunge wa CHADEMA,ni wazalendo sana tofauti na wenzao wa CCM waliokwisha chukua fedha zao

Wakuu hizi ni tetesi nimezisikia mitaani mimi mwenyeewe wapenzi wa chadema wakifurahia hatua hiyo
 
Utakuwa uongo tu labda mimi sijui maana ya kuzikataa, kwamtu mwenye akili hawezi kuzikataa pesa hizo ila unaweza kubadilisha matumizi....
 
Tetesi hazina mantiki. Zile pesa hawapewi, wanakopeshwa kisha zinakatwa kwenye mishahara na posho zao. Kwa hiyo si Chadema tu, yeyote asiyetaka kukopa hajazi fomu za mikopo, hivyo atakuwa analipwa mishahara yake yate na posho bila makato, na akifika mwisho mafao yake hupewa kamili. Wanaojaza fomu hizo wanapewa pesa hizo lkn mwishowe hulia na kusaga meno wakati mafao na mishahara yao vinapokatwa.
 
Signature yako inaweza kuwa ndio jibu

Kwa Tanzania Masuala ya Uongo yanaaminiwa sana kuliko Masuala ya Ukweli !
 
Mimi nafikiri walipashwa kuzikataa zote hakuna kuchukua hata centi moja. hatukuwatuma kwenda kununua magari tuliwatuma kwenda kutetea maslahi ya watanzania. Huu ni upumbavu wa kupeana magari bila mpango. Mbona wenzao nchi zilizoendelea hawafanyi ujinga huu kwa nini Tz. ambayo ni nchi maskini kupita mipaka watawala wanagawana pesa kama njugu wakati hospitali hazina dawa mashuleni hakuna walimu wala madawati sasa huu ni uwendawazimu au ndio kulogwa.. Chadema Chadema achananeni na hiyo hongo ya wazi wazi mkipokea watawamaliza bungeni
 
Nawashauri wabunge wa Chadema kuwa wazipokee hizo 90M halafu hizo wanazofikiri hawazihitaji (40M), wazipeleke kila mmoja kwenye jimbo lake kwa ajili ya maendeleo. Mkiziacha, mafisadi watazifisadi kama ilivyo kawaida yao.
 
Mimi nafikiri walipashwa kuzikataa zote hakuna kuchukua hata centi moja. hatukuwatuma kwenda kununua magari tuliwatuma kwenda kutetea maslahi ya watanzania. Huu ni upumbavu wa kupeana magari bila mpango. Mbona wenzao nchi zilizoendelea hawafanyi ujinga huu kwa nini Tz. ambayo ni nchi maskini kupita mipaka watawala wanagawana pesa kama njugu wakati hospitali hazina dawa mashuleni hakuna walimu wala madawati sasa huu ni uwendawazimu au ndio kulogwa.. Chadema Chadema achananeni na hiyo hongo ya wazi wazi mkipokea watawamaliza bungeni
Wanaweza kuzikataa lakini huenda haitakuwa na maana yoyote kwa vile fungu hilo limeshatengwa na serikali, na hata kama wakizikataa hazitarudi hazina, badala yake zitaliwa na watu wengine tu huko Bungeni. Ni muhimu wazichukue tu hata kama wanaona ubaya wake. Ni mpaka pale watakakuwa na uwezo wa kubadilisha kanuni na taratibu rasmi ndipo utaweza kuwalaumu
 
Back
Top Bottom