Tetesi Bulletin: Musiba agoma kuitikia wito wa Polisi kuhojiwa; Polisi wajiuma meno...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
1154519
Nimeamua kum-activate "Ka-Nzi" kwa ajili tu ya siku hizi mbili tatu. Taarifa ni kuwa:

a. Bw. Musiba ambaye alidai kuna njama za vigogo kutaka kummalizia amekataa kwenda kutoa taarifa zaidi Ikulu au hata kuhojiwa na POlisi. Ametumiwa barua ya kuitwa kwenye lakini ameiyeyushia. Kiufupi hakuna afisa wa polisi mwenye "ngazi" na uwezo wa "kumuita yeye" bila special "clearance" - angalia (B).

b. Kuna mtu kutoka Ikulu - kuanzia sasa uitwe "Mfumo Nje ya Mfumo" ambaye amepiga mkwara na kuwa Musiba hawezi kwenda kwenye ni "special assignment".

c. Lilipotakiwa kufungiwa gazeti la Tanzanite baada ya kuwataja vigogo na viongozi wastaafu mtu huyo wa "Mfumo Nje ya Mfumo" alipiga simu na kumpiga mkwara Abbas (wa MAELEZO) kuwa asithubutu kufanya kitu hicho kwa sababu ya (B).

d. Kinyume na wengi wanavyoamini set up ya Musiba ni kubwa sana na atakavyomalizwa hakuna atakayeamini. Yeye na wale wengine walioingizwa kwenye hizi 'special assignments" watakuja kushughulikiwa vibaya sana si mbali sana.

e. Mfumo huu wa "Nje ya Mfumo" umeiweka TISS katika hali ngumu sana ya kiutendaji kazi. Inapofikia "mbele ya mtu kuna mtu na nyuma ya mtu kuna mtu" basi ni vurugu mechi. Ka-Nzi kanasema hadi hivi sasa kina Musiba na wenzake wanaendelea kufanya wanachofanya bila ya shaka kabisa kwa kibali cha Ikulu na wanaposema Ikulu wanamaanisha "Rais Mwenyewe".

f. Hata hivyo kwa watu wanaomjua Rais Magufuli wanajua tu kuwa siku atakapokuja kuwaruka atawaruka mzima mzima... Hii itatokea pale ambapo kundi hilo litakapojaribu "kumshughulikia" kiongozi mmoja mstaafu mashuhuri wa chama tawala.

Hayo ndiyo yasemwayo na Ka-Nzi.

DEACTIVATE.

NB: Kwa tunaomuunga mkono Rais tunaangalia yanayoendelea kwa umakini mkubwa. Tunaelewa kinachoendelea na kwanini...
 
Back
Top Bottom