Tetesi; Baada ya viwango vya ufaulu kushushwa Tanzania yaongoza duniani

Kifarutz

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
1,736
359
Wanajamvi,
Kuna tetesi kuwa baada ya viwango wa ufaulu kushushwa mpaka kufikia division five, sasa Tanzania inaongoza duniani kwa uhafifu wa viwango vya ufaulu. Jee taarifa hii ina ukweli kiasi gani?
 
Sio tetesi bali ni ukweli. Nakumbuka mara tu baada ya viwango vipya kutangazwa, magazeti na hata hapa jamvini kuliwekwa viwango vya ufaulu katika nchi mbalimbali, ambapo Tanzania ilionekana kuwa ya mwisho. 'Hongereni' wazee wa BRN!!!
 
Wanajamvi,
Kuna tetesi kuwa baada ya viwango wa ufaulu kushushwa mpaka kufikia division five, sasa Tanzania inaongoza duniani kwa uhafifu wa viwango vya ufaulu. Jee taarifa hii ina ukweli kiasi gani?
kuna uwezekano mkubwa kuwa ni ya kweli..
 
elimu ya tanzania bwana .. ni ya kumwachia mungu.....ndo anaejuaa nakumbuka enzi zile na nasoma kuna wazili alifuta degree accounts,akafuta somo la booking na commerce,agriculture halafu somo la chemistry na physics aliunganisha pamoja likaitwa pc...wale watu waliokuwa secondary miaka ya 2005 mtakumbuka kipindi hikoo na mlikuwa chuo kikuu mtakumbuka degree ya accounts ilivyofutwaa....
 
Sasa shule hazina waalimu, hakuna maabara, hakuna vitabu, hakuna maktaba, hao watoto mnategemea wafaulu vipi? acheni kulalamika kila kitu bana!!!!.......

kwakeli kushusha viwango ni suluhisho muhimu kufikia malengo ya BIG negative RESULTS NOW.

haya ndio mapinduzi tunayotaka katika secta ya elimu ambapo kila mtanzania atakua walau kafika kidato cha nne

najisikia furaha kusema KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI....
 
Wanajamvi,
Kuna tetesi kuwa baada ya viwango wa ufaulu kushushwa mpaka kufikia division five, sasa Tanzania inaongoza duniani kwa uhafifu wa viwango vya ufaulu. Jee taarifa hii ina ukweli kiasi gani?

Wala sishangai kwasababu Tanzania ni mojawapo ya nchi masiki kabisa duniani. Nchi za mwisho kabisa!
 
Hapa kuna confusion kidogo na binafsi sielewi nishike lipi. katibu mkuu aliita waandishi akatuambia ameanzisha div 5, waziri ndugu yetu mpendwa Mh. Philipo Mulugo akasema ilikuwa confusion yaani Prof Sifuni Mchome alikosea na hivyo Mulugo akamsahihisha kwamba div 5 haipo na div zero au round about ya msamvu ipo palepale, binafsi sijasikia maelezo zaidi mlioko jikoni tuambie round about ya msamvu ya ndugu Mulugo ipo au haipo?
pili, iwe zero au div 5 ukweli ni kwamba kwakuwa viwango vimeshushwa sana basi misamvu na mikono itapungua saaaana. kwakuwa naanzisha universal examination council basi msiwe na wasiwasi hizo div 2 zenu nitazigeuza msamvu. teh teh teh, kwi kwi kwi
 
elimu ya tanzania bwana .. ni ya kumwachia mungu.....ndo anaejuaa nakumbuka enzi zile na nasoma kuna wazili alifuta degree accounts,akafuta somo la booking na commerce,agriculture halafu somo la chemistry na physics aliunganisha pamoja likaitwa pc...wale watu waliokuwa secondary miaka ya 2005 mtakumbuka kipindi hikoo na mlikuwa chuo kikuu mtakumbuka degree ya accounts ilivyofutwaa....

booking ndio somo gani hilo?
 
!
!
kwani watanzania sie ni mahiri katika lipi la maana?

WATANZANIA ni MAHIRI katika KULALAMIKA na Tuache tulalamike hata Lowassa ashatamka; nchi ya walalamikaji,rais analalamika,PM analalamika,Spika analalamika,Ndugai analalamika,Mwigulu analalamika,Mbowe analalamika,Zitto,analalamika, Kitila analalamika, Shain analalamika, Seifu analalamika,Slaa analalamika,Ponda analalamika, Pengo analalamika,Kagasheki analalamika,Jangili analalamika, Diamond analalamika,Sugu analalamika,Lugola analalamika,wewe unalalamika,mimi nalalamika,mke wangu analalamika,watoto wanalalamika,mamkwe analalamika,Ufosaro analalamika,Mushi analalamika,Pr. Muhongo analalamika,Mengi analalamika, Jaydee analalamika,CLOUDS TV wanalalamika,Lowassa analalamika,Sitta analalamika,Membe analalamika,Mashekhe wanalalamika, Maaskofu wanalalamika,waumini wanalalamika, Mungu analalamika,Shetani analalamika.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom