Tetemeko la ardhi mkoa wa Kagera haikusababisha na serikali pia haikua karibu na Uchaguzi! Hongera mkoa wa Morogoro, Uchaguzi upo karibu

mr yamoto

JF-Expert Member
Oct 2, 2016
923
1,393
Habari wana JamiiForums

Kwanza kabisa na nukuu

"Nilikuwa najaribu kuangalia kwa mfano nchi kama China kwenye mwaka 2014 watu 617 walipoteza maisha, mwaka 2013 walipoteza watu 193, Mwaka 2010 walipoteza watu 2,998 mwaka 2008 China ilipoteza watu 98,712," ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu".

Pia "Ukijaribu kuangalia Japan, nchi ambayo imeendelea na ina utaalamu wa hali ya juu sana, kwenye mwaka 2016 tarehe 14 mwezi wa nne ilipoteza watu 6, baada ya siku mbili tarehe 16 mwezi wa nne 2016 tetemeko likatokea tena na likaua watu 35 … mwaka 1923 liliua watu 142,800 na hiyo ni Japan".

Lakini ukijaribu kutafakari maneno ambayo aliyetoa rais magufuli wakati ule, napata mashaka kuwa kilikuwa si kipindi cha kukaribia na Uchaguzi. Hii ni tabia ya mwanasiasa

Labda pia ni nukuu kauli yake wakati ule "wananchi wajipange kurekebisha nyumba zao kwa kuwa Serikali haitaweza kujenga nyumba zote zilizobomoka"

Kuna maswali tunaweza kutafakari na tusipata majibu kama

Je Hizi hela huwa zinachotwa kwenye mfuko gani?

Kama jibu

Kuna Mfuko Maalum wa Kujihami na Majanga, Ofisi ya Rais. PM nI chair, Rais ni muidhinishaji wa kutolewa Fedha za mfuko.

Je ni lazima kila majanga yakitokea zinapaswa kutolewa?

Maana tabia za viongozi wa Tanzania kila wanapofika karibu na Uchaguzi wapo tayari kuwa wapole ili wakamilishe mahitaji yao.

Najua Kuna watu wanaweza kutafakari vibaya lakini tunapaswa tutambue hapa magufuli ni mwanasiasa tu.

Ndio maana kuna usemi unasema "mwanasiasa akikwambia usiku mwema toka nje uangalie kama kuna giza au la "

Hongera mkoa wa morogoro kwa kupata msaada, maana Uchaguzi upo karibu.

mr yamoto.
 
Kauli tamtam .... PM pia juzi kazungumzua mikopo elim ya juu
 
Back
Top Bottom