Tetemeko la ardhi latikisa Kumamoto Japan

Dah! Halafu itokee mpo sebuleni na wakwe mnatizama runinga na taarifa za kuhusu tetemeko hapo mahali ndio zinaonyesha. Anyway poleni wahanga.
 
Kuna nn hapo kila siku majanga kwenye huo mji wa kumamoto, poleni sana wana kumamoto.
 
Huu mji hauishi mabalaa, wakati ule ulikumbwa na tetemeko kubwa, Leo umepata kadhia ya mafuriko ya hatari. Wajaribu kubadili jina huenda watanusurika na haya mabalaa. Poleni sana wakaaazi wa huu mji.
 
Huu mji hauishi mabalaa, wakati ule ulikumbwa na tetemeko kubwa, Leo umepata kadhia ya mafuriko ya hatari. Wajaribu kubadili jina huenda watanusurika na haya mabalaa. Poleni sana wakaaazi wa huu mji.
Maana yajina ukilitafsiri kwakikwenu linaweza kuleta ukakasi ila kwakikwao usikute maana yake nipepo
 
Ndani ya Kumamoto kumetokea tena majanga 😕
Leo mchana wakati nasikiliza radio dochivelle nimesikia kumetokea tena mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko.
Waziri mkuu kasema watapelekwa wanajeshi 10,000 kutoa msaada
 
160414145331_japan_earthquake_624x485_afp.jpg

Tetemeko la ardhi latikisa Kumamoto Japan
Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa maeneo ya kumamoto Kusini mwa Japan na kusababisha uharibifu mkubwa.

Msemaji wa serikali ameiambia BBC kuwa tetemeko hilo lenye kipimo cha 6.4 katika vipimo vya Richter ilitikisa mji wa Kumamoto na kisiwa cha Kyushu.

Maeneo ya mashariki ya mji wa Kumamoto ndiyo yaliyokuwa kitovu cha tetemeko hilo.

Vituo vya kuzalisha umeme kwa nguvu za kinyuklia vya Sendai na Genkai vyote viko katika kisiwa cha Kyushu.

160414151246_japan_earthquake_512x288__nocredit.jpg

Msemaji wa serikali ameiambia BBC kuwa tetemeko hilo lenye kipimo cha 6.4 katika vipimo vya Richter ilitikisa mji wa Kumamoto na kisiwa cha Kyushu.
Majengo mengi yameporomoka katika mji wa Kumamoto na polisi wanashuku kuwa huenda watu kadhaa wamefukiwa na vifusi vya majengo yaliyopotromoka.

Afisa mmoja wa katika kitongoji cha Uki nje kidogo ya Kumamoto anasema kuwa hata jengo la baraza la mji umeathirika.

Msemaji wa serikali Yoshihide Suga amesema kuwa makundi ya waokoaji ndio yameaanza kutathmini madhara ya tetemeko hilo la ardhi na kisha kuishauri serikali.

Huduma za treni zilikatizwa kwa muda kama tahadhari tu.

160414151359_japan_earthquake_512x288__nocredit.jpg

Huduma za treni zilikatizwa kwa muda kama tahadhari tu.
Japan hukumbwa na matetemeko ya ardhi mara kadha lakini kutokana na sheria na kanuni kali za ujenzi madhara ya tetemeko huwa sio makubwa.

Tetemeko kubwa la ardhi lenye alama 9 kwenye vipimo vya Richter ilitikisa Japan Machi mwaka wa 2011 na kutibua kimbunga na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu 18,000.

Aidha vinu vya nyuklia vya kuzalisha umeme viliharibika katika tetemeko hilo.

Chanzo: BBC Swahili
Pole kwa wahanga.

NB Je za baridi hazijatikiswa 😂
 
Huu mji hauishi mabalaa, wakati ule ulikumbwa na tetemeko kubwa, Leo umepata kadhia ya mafuriko ya hatari. Wajaribu kubadili jina huenda watanusurika na haya mabalaa. Poleni sana wakaaazi wa huu mji.

Mbona usitaje jina tujue mji gani huo unaongea kuhusu.
 
Jina lake huo mji kulitaja mtihani.
Nilipokuwa sekondari, wakati tunasoma soma la kifaransa, kuna maneno ya kifaransa kama "timbre" ( inayotamkwa tombre). Sasa kuna dada mmoja alikuwa anaona noma kulisema hilo neno. Basi mwalimu akamwambia, "unapotumia lugha ya kigeni usifikirie maana ya maneno kwa lugha yako". Akaendelea kusema, "kama unaishi kwenye mji mmoja huko Japan halafu ndugu zako wanakuuliza unaishi mji gani utasitasita kuutaja? Utasema tuu, Kumamoto!
 
Jina lake huo mji kulitaja mtihani.

Hehehe!! Na kwao huko unawezakuta jina Morogoro lina maana balaa, sasa nenda huko uwaambie umetokea Morogoro uone wakiangaliana na kuangua kicheko.
Hizi lugha, hata zetu za asili kuna maneno yana utata ukiyatumia kwa baadhi ya makabila.
 
Back
Top Bottom