Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,036
- 3,929
Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya ukubwa wa 8.0 kipimo cha tetemeko, limeikumba nchi ya Mexico kwenye pwani ya Kusini ya nchi hiyo katika bahari ya Pacific
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa kinakaribia umbali wa kilometa 100 (62 miles) Kusini-Magharibi mwa mji wa Pijijiapan na lenye kina cha kilometa 35, Mtafiti wa Kijiolojia wa Marekani ameripoti.
Tahadhari ya Tsunami imetolewa kwa nchi za Mexico, Guatemala, EL Salvador, Costa Rica, Nicaragua, Panama and Honduras.
Tetemeko hilo la ardhi limesikika katika mji wa Mexico City, kusababisha majengo kutikisika na kupelekea watu kukimbilia mtaani.
UPDATES
Karibia watu 29 wamefariki dunia baada ya tetemeko hilo la ardhi kuipata Mexico ambalo ni kubwa kuipata kwa kipindi cha karne nzima.
Rais wa Mexico Enrique Peña Nieto amesema tetemeko hilo ni kubwa kwa nchi hiyo kulipata kwa kipindi cha miaka 100.
Tsunami imethibitishwa katika nchi ya Mexico, ambalo lilikuwa na mawimbi yenye urefu wa futi 3 (mita 1), hili limesemwa na National Weather Service's Pacific Tsunami Warning Center kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa titwa.
National Weather Service's Pacific Tsunami Warning Center kupia ukurasa huo huo wa titwa imesema kuwa tsunami ambayo inaweza kuwa na mawimbi yenye kubwa wa zaidi ya futi 10 (mita3) yana weza kuipata Mexico, wakati tsunami yenye mawimbi ya urefu wa futi 3 yanaweza kuzifikia hadi nchi za Ecuador, New Zealand and Vanuatu.