Tetemeko la Ardhi la Ukubwa wa 8 laikumba Mexico, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha. Tahadhari ya Tsunami yatolewa

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
map.PNG


Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya ukubwa wa 8.0 kipimo cha tetemeko, limeikumba nchi ya Mexico kwenye pwani ya Kusini ya nchi hiyo katika bahari ya Pacific

Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa kinakaribia umbali wa kilometa 100 (62 miles) Kusini-Magharibi mwa mji wa Pijijiapan na lenye kina cha kilometa 35, Mtafiti wa Kijiolojia wa Marekani ameripoti.

Tahadhari ya Tsunami imetolewa kwa nchi za Mexico, Guatemala, EL Salvador, Costa Rica, Nicaragua, Panama and Honduras.

Tetemeko hilo la ardhi limesikika katika mji wa Mexico City, kusababisha majengo kutikisika na kupelekea watu kukimbilia mtaani.

UPDATES
Karibia watu 29 wamefariki dunia baada ya tetemeko hilo la ardhi kuipata Mexico ambalo ni kubwa kuipata kwa kipindi cha karne nzima.

Rais wa Mexico Enrique Peña Nieto amesema tetemeko hilo ni kubwa kwa nchi hiyo kulipata kwa kipindi cha miaka 100.

Tsunami imethibitishwa katika nchi ya Mexico, ambalo lilikuwa na mawimbi yenye urefu wa futi 3 (mita 1), hili limesemwa na National Weather Service's Pacific Tsunami Warning Center kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa titwa.

National Weather Service's Pacific Tsunami Warning Center kupia ukurasa huo huo wa titwa imesema kuwa tsunami ambayo inaweza kuwa na mawimbi yenye kubwa wa zaidi ya futi 10 (mita3) yana weza kuipata Mexico, wakati tsunami yenye mawimbi ya urefu wa futi 3 yanaweza kuzifikia hadi nchi za Ecuador, New Zealand and Vanuatu.
 
View attachment 583919

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya ukubwa wa 8.0 kipimo cha tetemeko, limeikumba nchi ya Mexico kwenye pwani ya Kusini ya nchi hiyo katika bahari ya Pacific

Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa kinakaribia umbali wa kilometa 100 (62 miles) Kusini-Magharibi mwa mji wa Pijijiapan na lenye kina cha kilometa 35, Mtafiti wa Kijiolojia wa Marekani ameripoti.

Tahadhari ya Tsunami imetolewa kwa nchi za Mexico, Guatemala, EL Salvador, Costa Rica, Nicaragua, Panama and Honduras.

Tetemeko hilo la ardhi limesikika katika mji wa Mexico City, kusababisha majengo kutikisika na kupelekea watu kukimbilia mtaani.
pole zao
 
Matetemeko, vimbunga, maporomoko ya udongo, mamilioni ya samaki kufa kwa kukosa oksijen huko kwenye mito, ukame, joto kali, n.k. n.k. Naam, ule mwisho u karibu enyi watu wa Mungu!
 
Majaribio ya Kinyuklia hudisturb tectonic plates za dunia, na athari zake huweza kutokea maelfu ya kilometa mbali na yalipojaribiwa!
 
Takribani watu 90 wameuwa kufuatia tetemeko la ardhi la uzito wa 8.1 katika vipimo vya richa nchini Mexico kwa mujibu wa maafisa.Msemaji wa serikali alisema kuwa watu 71 walikuwa wameuawa katika jimbo lililo kusini magharibi la Oaxaca.Mamia ya familia zimeripotiwa kushinda katika mitaa, zikihofia hatari za mitetemeko midogo.Wanajiolojia nchini Mexico wanasema kuwa mitetemeko midogo 721 imerekodiwa tangu tetemeo kubwa la Alhamisi.Tetemeko hilo lilikuwa la nguvu nyingi zaid kuwai kushuhudiwa nchini humo kwa karne moja.Siku ya Ijumaa, pwani ya mashariki mwa Mexico ilikumbwa na dhoruba inayojulikana kama Katia.Watu wawili walifariki kwenye maporoko ya udongo baada ya mvua kubwa. Pia Nguvu ya upepo mkali unaondamana na kimbunga, kimeanza kugonga visiwa kadhaa kusini mwa jimbo la Florida nchini Marekani, huku kimbunga kikiacha uharibifu mkubwa katika visiwa vilivyoko kwenye bahari ya Atlantic huko Caribbean, kuelekea Marekani.Kimbunga Irma, kinatarajiwa kugonga maeneo hayo, baadaye leo Jumapili.Viwango vya maji tayari vimeanza kuogezeka katika maeneo ya pwani ya Florida, eneo ambalo linatarajia kimbunga kikubwa kuwasili.Taharuki na hatma ya baadaye ya mji wa Tampa, ambao unakabiliana ana kwa ana na njia inakopitia kimbunga hicho, haijulikani.Zaidi ya watu milioni 6 huko Florida wanaondolewa majumbani mwao- robo tatu ya idadi nzima ya watu wa jimbo hilo.
097fd932efe0839a798d6220b04dcf4a.jpg
7b76afee10636f80e21585272ae17216.jpg
3e16c6e70954f0bea29584aadfa6644c.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama yatatokea mafuriko,kamwe hayawezi kuwa makubwa kushinda yale ya Nuhu!
Upinde wa mvua ndiyo alama ya agano kati yetu na Mungu juu ya kuiharibu dunia!
Tetemeko ni zao la sahani za mabara kugongana,kusagana au kuachana!
Zinapogongana,kuachana au kusagana mtikisiko wake ndiyo uleta tetemeko!
Ni majanga ya asili ila ni kumwomba Mungu madhara yasiwe makubwa!
 
nataman hilo tetemeko lingepita na pale magogon lifunike kila kiumbe kilichopo mule. harafu likate kona liingie mitaa ya lumumba likwangue kila kitu cha pale.
 
Back
Top Bottom