Tetemeko la ardhi huko CHINA.....

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Jul 27, 2007
451
9
nipo naangalia runinga ITV naona kuna TETEMEKO la ardhi huko china.
naamini kwa uwezo wake mola,watanzania wenzetu wote kwa ujumla wako salama.
najaribu kumtafuta mdau mmoja wa JF aliyeko huko china atupe news zaidi.
 
nipo naangalia runinga ITV naona kuna TETEMEKO la ardhi huko china.
naamini kwa uwezo wake mola,watanzania wenzetu wote kwa ujumla wako salama.
najaribu kumtafuta mdau mmoja wa JF aliyeko huko china atupe news zaidi.

Kwenye breaking news walisema hakuna alofariki lakini sasa hivi Al- jazeera wanasema karibu watu mia tano wamekufa.
 
naona msimu wsa majnga umeivamia dunia. Iliania Burma, ikaja Marekani sasa China. Tuombe Mungu haya yasifike kwenye hizi nchi zetu ambazo hata masuala madogo kama ya Mererani yanatutoa jasho
 
wachina sio wakweli katika taarifa zao,siku zote wao wanajifanya wasiri,yawezekana kweli kuna watu wamekufa ila station zao zote hapa zinasema hakuna aliyekufa na isitoshe hali ni shwari.Kumbukeni hata wakati wa winter kuna watu wengi sana walikuwa ila wao walikuwa wanaficha.mie hawa jamaa wananibore kinoma
 
tetemeko la ardhi kila siku china tu jamani ? pastor hagee (wa mccain) angesema kuna jambo !
 
xinhua wameripoti zaidi ya watu 10000 wamejeruhiwa katika county moja , sehemu iliyoathirika zaidi ni katika mji unaoitwa chengdu, uko china "interior" , ripoti zinasema asilimia 80 ya majengo ya mji yameharibiwa
 
Naona hapa JF idadi tayali imeanza kuongezeka ni kkijumlisha kwa haraka haraka tayari wamefikia 50,000 ,si unajuwa kwa China huenda ikawa wanashukuru wakati nyie mnasikitika.
 
Naona hapa JF idadi tayali imeanza kuongezeka ni kkijumlisha kwa haraka haraka tayari wamefikia 50,000 ,si unajuwa kwa China huenda ikawa wanashukuru wakati nyie mnasikitika.

Mwiba hii kauli yako siyo nzuri, kumbuka watu wamepoteza mama zao, watoto wao, wapendwa wao, baba zao, n.k. sasa hapo wana kitu gani cha kushukuru?. janga linapopiga hamna cha ujanja ndugu
 
nimeongea na mshikaji mtangazaji wa bbc yupo beijing anaitwa fadhil mpunji anasema watu 9000 almost wamekufa.
 
Ee Mola Tunusuru na Adhabu hii...wana JF tukumbuke mwisho wa UHAI...mafisadi hawaogopi siku hio..wanafikiri wataishi Milele...Mtu mmoja kumiliki Mali kiasi kikubwa sijui watumiaje...
 
mwaka 1933 tetemeko lenye ukubwa wa 7.5 lilitokea jimbo hilo hilo na kuua watu 9300,mwaka 1976 liliua watu 240000,mwaka 2003 lilitokea jimbo jingine na kuua watu 260 .Hili lilikuwa na ukubwa wa 6.8.figure kamili ya lililtokea leo bado haijajulikana.ila la leo lilikuwa na ukubwa wa 7.8.Sasa wataalamu tuelezeni hapo
 
Kuna WaTanzania wangapi huko CHENGDU?

Balozi wetu bwana RAMADHANI MAPURI ana react vipi kuhusu kujua hilo

mliopo China hebu tuleteeni latest
 
Kuna WaTanzania wangapi huko CHENGDU?

Balozi wetu bwana RAMADHANI MAPURI ana react vipi kuhusu kujua hilo

mliopo China hebu tuleteeni latest
Habari zenu
Latest kutoka ChengDu by kijana wa kitanzania ni kwamba hali si shwari,maeneo ya chuoni kwao tetemeko lime hit na kuua watatu ambao haijafahamika kuwa ni wanafunzi ama la,hakutoa taarifa ya kufa kwa foreigner yoyote,upatikanaji wa taarifa kwao ni mgumu kutokana na kutokuwepo kwa umeme pia mawasiliano ya simu yamerejea leo hii asubuhi.Jengo lao limeathirika ,wengi wao wamepoteza vitu vyao vya thamani ikiwemo laptop yake APPLE mpya imevunjika.

Anasema kuwa almost kila kitu kimefungwa;supermarkets,restaurants,makazi yote hivyo wamefunga shule na usiku wa jana kuamkia leo watu wote wamelala nje,hadi hivi leo wanafunzi wote wako uwanjani wakihofia dorms zao kubomoka,huduma za chakula na nyinginezo wanazipata toka local gorvenment free of charge.

Mimi niko central south of China na hilo tetemeko lime hit sana south west,jirani zetu,wakati tuko class jana tulilihisi kidogo pia kuna waTZ huko WuHan(jirani nasi)-mji ambao una waTZ wengi,walikuwa class 15th floor walilipata vizuri na ikabidi kipindi kisitishwe kwa muda,baadae mwalimu aliwapoza na kuendelea,hakuna maafa yaliyoripotiwa.

Hadi sasa walioripotiwa kufa katika tukio zima ni takribani watu elfu10,ubalozini wana contact details zetu ikiwa ni pamoja na e-mail adresses lakini mimi sijapata concern yoyote kutoka kwao ila naamini watakuwa wanafanya followup(tunawadhania kheir)
Tutapeana mambo yanavyojiri inshaallah.
 
figure niliyoipata sasa watu waliokufa ni 10300.pia waliojeruhiwa ni zaidi ya 1000.habari zanasema pia wakati wa tetemeko chemical plants zimelipuka mji mwingine na kusambaza tani 80 za sumu ya maji ya ammonia na watu 600 wamekufa na 2300 were buried by rubble
 
Back
Top Bottom