Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mitetemeko ya ardhi ilisikika pia Istanbul na Athens.
Kitovu cha tetemeko hilo la nguvu ya 6.3 kwenye vipimo vya Richter kilimuwa kilomita tano kusini mwa Lesbos, Idara ya utafiti wa Jiolojia ya Marekani imesema.
Nyumba kadha ziliharibiwa, Meya wa mji huo alisema.
Hakujatolewa taarifa zozote za majeruhi kufikia sasa. Uturuki na Ugiriki huwa kwenye eneo lenye nyufa na mitetemeko ya ardhi hutokea mara kwa mara.
"Tumeizoea mitetemeko sisi kama watu wa Izmir lakini hili lilikuwa tofauti. Nilidhani mwenyewe kwamba kwamba wakati huu tungefariki dunia", Didem Erus, daktari wa meno wa umri wa miaka 50 anayeishi mji wa Izmir Pwani ya Uturuki aliambia Reuters.