Testesi: Kisa cha serikali kushindwa kudhibiti mauaji ya Maalbino | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Testesi: Kisa cha serikali kushindwa kudhibiti mauaji ya Maalbino

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akili, Nov 13, 2008.

 1. a

  akili Member

  #1
  Nov 13, 2008
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  INASEMEKANA eti kuna wanasiasa na watumishi wa serikali ambao nao wameahidiwa na waganga hao hao kwamba ili wapate Uwaziri au ukuu wa mkoa au ukuu wa polisi wa mkoa au ubalozi au ukatibu mkuu wizarani ni muhimu kupeleka viungo vya maalbino.

  Katika hali kama hii soko kuwa kubwa na walinzi kuwa wateja, inakuwa ngumu kidogo kuona namna gani maalbino watanusurika.

  Labda pengine ianzishwe mgambo ya kuwalinda maalbino. Au maalibino wote waishi kwenye kambi moja karibu na Ikulu au kitu kama hicho.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Siku hizi waganga wamechenji madai,kwa hali ya vyero na utajiri basi ukipeleka sikio tu ,tena la mtu yeyote basi utafanyiwa na kupata mahitaji yako.Na kazi ya kukatana masikio imeshaanza katika mikoa ya ziwa.
  Hivyo kaeni mkifahamu kuwa sikio la mtu hivi sasa ni hotcake ndani yaTanzania.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Duh! Hapa itabidi tununue zile kofia za Rambo zinazoficha masikio.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hii kweli ni tetesi...
   
 5. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ha ha ha ha.

  Hii imenichekesha sana. Asante Jasusi kwa kutengeza siku yangu iliyokuwa imeanza kupooza.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280


  Wakuu hii ni kali. Sasa kila kiungo ni dili. Haya mambo yalianzia Mbeya miaka hiyo sasa naona yanasambaa kwa kasi. Mnakumbuka enzi za kuchunwa ngozi??

  Ila fahamu kwa hali hii baadhi ya binadamu wamegeuka shetani, wasio na huruma wala upendo wenye kuweka maslahi yao mbele. Huu ni ubinafsi.

  Yesu Kristu na ashuke kuuuchukua ulimwengu maana maasi na machukizo yanazidi kila kukicha. Muda si mrefu Sodoma na Gomora itakuja. The level of crime is at the highest degree now, guess what????Hata kuolewa na kuoa sasa hati hati maana hujui ni binti unakumbana na jamaa kumbe anakuoa ili apate kuwa karibu na wewe akupige dili? !!!! Si umesikia tena yale ya yule mume alikuwa katika harakati za kumnadi mkewe albino kwa 3.6 milioni??!!!

  Inatisha aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mambo yalianza zamani sana ,kama nakumbuka kulikuwa na mumiani ,hawa kama madrakula eti wakikunyonya damu na kwenda kuuza kusikojulikana,likaingia kashkashi la Mbeya uvunaji wa ngozi ya binadamu,likaingia parapanda la vichwa vya wenye vipara au upaa haujapita muda mrefu wakavamiwa maalbino na sasa wameona masikio pia yanasababisha ndoto kuwa kweli.
  Hivi hawa waganga kwa nini hawapigwi marufuku nasikia nchi za Falme za kiarabu wakikugundua unafanya mashuguli ya Uganga wanakuzoa kwa karandika na hakuna cha mahakama wakishapata uhakika kuwa unaendesha shuguli hizo basi utaishia jela na shuguli zako.
  Na hawa waganga wetu wanaokamatwa kuhusika na shuguli za kuwaua maalbino ,hivi wanawataja wateja waliokwisha wafanyia mauzauza hayo ya kuhusisha viungo vya albinoz ? Yaani angalau tungesikia kigogo mmoja amekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya albino miaka iliyopita !! Nashangaa na usalama wa Taifa vipi ?Ivi hawavuti kucha na kuwabana mabilinganya hawa waganga wanaowatia mbaroni ili kutaja dili zilizopita ?
   
 8. H

  Huduma Member

  #8
  Nov 14, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani unachosema ni kwamba wanasiasa na viongozi wa serikali wenyewe huwa wanakwenda kwa waganga hao hao ambao huwa wanawaagiza na wao walete viungo vya maalbino ili wapande cheo, watolewe kwenye listi ya mafisadai na waokoke na laana na juju la walalahoi au sio?
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Date::11/16/2008
  Zamu ya vigogo wa EPA kupanda mahakamani yakaribia
  *Wamo mawaziri,wafanyabiashara wazito zaidi

  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi

  BAADA ya Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP), kusema bado kuna upelelezi zaidi kwa baadhi ya majalada ya watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) iliyokuwa Benki Kuu (BoT), baadhi ya majina ya vigogo likiwemo la mmoja wa waliokuwa mawaziri wa wizara nyeti wa serikali iliyopita, yanatajwa kuwa katika orodha ya watu wanaoweza kufikishwa mahakamani wakati wowote.

  Kutajwa kwa majina ya vigogo hao (tunayo) pamoja na waziri huyo, ambaye pia alitumikia serikali iliyopo kabla ya baraza la mawaziri kuvunjwa Aprili, kumekuja wakati kukiwa na taarifa za uhakika kutoka duru huru za kiserikali kwamba, Rais Jakaya Kikwete, ameachia vyombo vya dola vifanye kazi zake kwa uhuru.

  Habari hizo za kuaminika kutoka serikalini zinasema uamuzi huo wa rais kuachia vyombo hivyo vifanye kazi zake kwa uhuru, umevipa nguvu za kuweza kuandaa baadhi ya taratibu za kushughulikia vigogo hao wa EPA na wengine wa ufisadi tofauti nchini.

  Alipoulizwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishina Robert Manumba, kuhusu kukamilika upelelezi kwa baadhi ya majalada aliyoagiza, DPP, alijibu: "Nafikiri si vizuri sana kuanza kuelezea kwa kina na hadharani kuhusu taratibu za upelelezi."

  Kamishina Manumba alisema upelelezi huo unafanywa na timu, hivyo si sahihi kuanza kuamka na kueleza mipango mbalimbali akasisitiza kwa kusema: "Nafikiri subiri tu, kila kitu kitafahamika na DPP ataweka wazi."

  DCI Manumba aliongeza kwamba iwapo upelelezi utaanza kuelezwa kwa uwazi ni dhahiri utavurugika na akazidi kusihi akisema:"Tusubiri, maana hii ni kazi ya timu."

  Wakati Kamishina Manumba akisema hilo, duru za kiserikali zilisema mmoja wa watu waliowahi kushika wadhifa wa katibu mkuu kwenye wizara moja na pia cheo katika ofisi ya waziri mkuu, anatajwa kuwa ni miongoni mwa watuhumiwa wa ufisadi ambao wanashughulikiwa kwa kujihusisha na kampuni ya Meremeta.

  "Kwa sasa, bwana mkubwa (Rais) ameachia vyombo vifanye kazi zake kwa uhuru; amesema hataki kuviingilia, ndiyo maana ndugu yetu (huyo waziri wa zamani) na wenzake anaweza kufikishwa mahakamani wakati wowote," kilisema chanzo hicho cha kuaminika na kuongeza.

  Kwa mujibu wa duru hizo, ndani ya orodha hiyo ya vigogo, wamo pia wafanyabiashara maarufu nchini ambao wanatajwa kwamba wanaweza kupanda kizimbani wakati wowote upelelezi ukikamilika na DPP akijiridhisha kwamba kuna ushahidi wa kesi.

  Duru hizo za habari za kiserikali zilifafanua zaidi kuwa tayari waziri huyo wa zamani amekwishajua mchakato unavyoendelea na kwamba katika siku za karibuni ameamua kuwa kimya.

  "Siku hizi amekuwa kimya... anajua kinachoendelea, labda apate msamaha wa bwana mkubwa (Rais) kabla ya kufikishwa mahakamani akienda kumuomba amsamehe, lakini hadi sasa ana wakati mgumu ndiyo maana yuko kimya," kilifafanua chanzo hicho.

  "Hivi sasa watu wana wasiwasi... kwa mfano, ndugu yetu (jina tunalo) naye anatajwa katika kashfa ya Meremeta kipindi akiwa katibu mkuu wizara..."

  "Bwana mkubwa hatabiriki, amechoka kuona anabebeshwa mizigo ambayo si yake. Sasa anataka kuonyesha wananchi kwamba yuko makini."

  Hadi sasa tuhuma zinazotajwa kuwa zinaweza kufikisha vigogo mahakamani kwa nyakati tofauti ni pamoja na wizi wa fedha za EPA, kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa Kampuni Richmond na sakata la Meremeta.

  Lakini wengi wanasubiri kuona vigogo wanaotajwa kuhusika kwenye kashfa ya EPA wakipandishwa kizimbani baada ya Jeetu Patel pekee kuonekana kuwa ndiye kigogo miongoni mwa watuhumiwa 20 ambao wameshafikishwa mahakamani hadi sasa.

  Ufisadi huo wa fedha za EPA ulibainika katika hesabu za BoT za mwaka 2005/06, baada ya Kampuni ya Deloitte&Touche ya Afrika Kusini kubaini ufisadi wa Sh40 bilioni zinazodaiwa kuchotwa na Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, lakini kampuni hiyo ya ukaguzi ikazuiwa kuendelea na kazi.

  Hata hivyo, mwaka jana serikali ilimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutafuta kampuni nyingine ya kimataifa, kufanya ukaguzi huo kubaini ukweli.

  Ofisi ya CAG iliteua Kampuni ya kimataifa ya Ernst&Young, ambayo ilibaini ufisadi wa zaidi ya sh 133 bilioni, ambazo zilichotwa na makampuni 22.

  Makampuni 13 yalijichotea Sh 90.3 bilioni, ni pamoja na Bencon International LTD of Tanzania, Vb & Associates LTD of Tanzania, Bina Resorts LTD of Tanzania, Venus Hotel LTD of Tanzania, Njake Hotel &Tours LTD, Maltan Mining LTD of Tanzania.

  Mengine ni Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment LTD, B.V Holdings LTD, Ndovu Soaps LTD, Navy Cut Tobacco (T) LTD, Changanyikeni Residential Complex LTD na Kagoda Agriculture LTD.

  Kwa upande wa makampuni tisa yaliyochota Sh 42.6 bilioni ni pamoja na G&T International LTD, Excellent Services LTD, Mibale Farm, Liquidity Service LTD, Clayton Marketing LTD, M/S Rashtas (T) LTD, Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloma and Brothers na KARNEL LtD.

  Kumbukumbu za makampuni mengine mawili ya Rashtas (T) na G&T International LTD, zikiwemo nyaraka za usajili hazikuonekana katika daftari la Msajili wa Majina ya Makampuni na Biashara (BRELA).

  Kufikia mwaka 1999 deni katika EPA lilifikia dola 623 milioni, ambazo kati ya hizo dola 325 milioni zilikuwa ni deni la msingi na dola 298 ni riba na kisha baadaye, deni likaongezeka hadi kufikia dola 677 milioni.

  Hata hivyo, chini ya Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme) wa mwaka 1994 kati ya serikali na Benki ya Dunia (WB), waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya fedha wanazodai, wapo waliokubali na wengine kukataa na kuongeza hadi mwaka 2004 taarifa zinaonyesha jumla ya dola 228 zililipwa chini ya mpango huo.

  EPA ni akaunti ya madeni ambayo ilitumika wakati wa Mfumo wa Ujamaa, ambayo akaunti yake ilikuwa katika iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) chini ya usimamizi wa BoT.

  Mwaka 1985, EPA ilihamishiwa moja kwa moja BoT, na ndipo mwaka juzi kulipoibuka utata wa tuhuma za ufisadi katika akaunti hiyo kwa mahesabu ya mwaka 2005/06, ambayo utata huo ulisababisha Ernst&Young kufanya ukaguzi kuanzia Septemba sita na kukabidhi ripoti yake kwa CAG mapema Desemba mwaka jana.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Duh! Sasa naona kuna ubambikaji wa hali ya juu wa jumbe bila kujali kichwa cha habari. Sasa hii habari ya Maalbino na ufisadi wa EPA wapi na wapi!!!!? :confused:
   
 11. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa bubu, si ni wewe ndo umeipost hii ya EPA hapa kwenye Maalbino? Kama si wewe basi either kulitokea tatizo la kiufundi au kuna mtu ameshajua password yako, na amelogin as Bubu then akawa anafanya anachotaka like this. Hata hivyo unaweza ukaidelete post hiyo ya EPA, na tatizo likija kujirudia, better you change password !!!
   
 12. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  si nasikia pale chimwag wenzetu walizika albino pale ile mgombea wao wa urais apite, na sasa wamamua kuwe chuo kikuu kuua soo?
   
 13. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #13
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Wauaji wa albino,hawakamatwi kwa sababu Polisi wanadhani kwamba hawa watu wauaji wanahitaji kuelimishwa,na siyo kupelekwa Mahakamani.
  Polisi hapa hawafanyi kazi kama Polisi Ulaya. Kule ikitokea serial killings,Polisi wanaulizwa kama wamekwishamakata mtuhumiwa yeyote. Kama bado,Mkuu wa Polisi anabadilishwa,anawekwa mwingine ambaye anaweza kuahidi kuleta matokeo

  Lakini tukumbuke kuhusu Ushirikina,na kusali chini ya mbuyu,wapo watu wengi ambao watakuambia kwamba walipata faida walipofanya mambo hayo. Kwa hiyo,siyo kazi yetu kuwaambia kwamba Uganga haupo Isipokuwa lazima uwepo ustaarabu,kama watu ambao tuanishi katika karne ya 21,
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kama Gordon Brown au CNN na BBC wakikemea kwa nguvu serikali ina uwezo mkubwa sana wa ku-deal na hilo tatizo. Ni uhakika wanaweza, tatizo ni kuwa halihusiani na maslahi ya wakubwa na kama linahusiana na maslahi ya wakubwa kama mchangiaji mmoja anavyosema, yaani nao wakipeleka sikio la Albino kwa mganga wanaweza kupewa uwaziri au ukuu, basi suluhu yake haitapatikana hata siku moja.
  Lakini tukumbuke kuwa watu wanapokuwa wamekata tamaa ya maisha, watafanya kila wanaloweza ili walau warudishe matumaini hata ikiwa ni kukimbilia kwenye ushirikina. Hicho ndicho wanachofanya hao wauaji wa Albino, na ajabu ni kuwa hata wakiua hao albino hakuna anayekuwa milionea, na sidhani kama JK anatoa uwaziri kwa misingi ya aina hiyo. Nadhani kwanza unatakiwa uwe mwanaCCM, mtandao, urafiki labda kidogo na uwezo na elimu yako.
   
Loading...