Terehe 14 Disemba, 2021, DPP atawasilisha Nolle kesi ya akina Mbowe?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Mawakili wa Serikali waliomba muda Zaidi kuandaa Maelezo yao ya maandishi kwani Mh. Jaji mwenyewe alikuwa tayari kutoa uamuzi wake kesho. Baadhi ya waliowasikia Wanasheria wa Serikali walivyotoka jana wanadai kuwa iwapo uamuzi utatoka kuonesha Mtuhumiwa Ling'wenya aliteswa basi Serikali itaendelea kuumbuka.

Kutokana na hali ilivyo na kwa dalili walizoziona kwenye kesi ndogo iliyokamilika kusikilizwa jana wameshauriana wawasilishe ombi la "Nolle" ili kesi isiendelee na watafute namna ingine ya kujisafisha.

Jana hiyo Mawakili wa Serikali walikuwa desparate sana wakiona kuwa wamepewa kesi ambayo imeanza kuwachafua katika jamii yetu. Walisikika wakimwomba Kiongozi wao Kidando aakutanishe kwa DPP kujadili hilo.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom