Terehe 14 Disemba, 2021, DPP atawasilisha Nolle kesi ya akina Mbowe?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
978
1,000
Mawakili wa Serikali waliomba muda Zaidi kuandaa Maelezo yao ya maandishi kwani Mh. Jaji mwenyewe alikuwa tayari kutoa uamuzi wake kesho. Baadhi ya waliowasikia Wanasheria wa Serikali walivyotoka jana wanadai kuwa iwapo uamuzi utatoka kuonesha Mtuhumiwa Ling'wenya aliteswa basi Serikali itaendelea kuumbuka.

Kutokana na hali ilivyo na kwa dalili walizoziona kwenye kesi ndogo iliyokamilika kusikilizwa jana wameshauriana wawasilishe ombi la "Nolle" ili kesi isiendelee na watafute namna ingine ya kujisafisha.

Jana hiyo Mawakili wa Serikali walikuwa desparate sana wakiona kuwa wamepewa kesi ambayo imeanza kuwachafua katika jamii yetu. Walisikika wakimwomba Kiongozi wao Kidando aakutanishe kwa DPP kujadili hilo.
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
17,246
2,000
Hawa makomandoo wa JWTZ wameteswa sana aisee, mateso makali kudhalilishaji wa ubinadamu wao, hata JWTZ wenzao wasifurahie kitendo hiki kabisa kabisa. Hii kesi ifutwe tu, maana inaleta simanzi kubwa miongoni mwa watanzania.
Inazidi kuibua chuki kati ya hizi taasisi na kati yao na wananchi pia. Sio afya kwa mustakabal wa taifa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom