Teophil Makunga umejidhalilisha mno kutumiwa na Nchimbi

Kama vile umenisoma mawazo.
Hii report imeandaliwa na watu wa TISS kisha kina Theo wakapewa tu waisaini.
Mawazo ya Theo hapa ni tofauti na michango ya waandishi wake kama kina Meena, Cherehani, Mabala n.k.

Sijui Theo utawaangalia vipi watu wako hawa kwa kukubali kwako kudhalilishwa kwa kiwango hiki.

Yaani nimeiosoma nikafikiri labda Theo ulitumwa dukani ndio wakaibadilisha, siamini kama umeshiriki humu.

Gazeti la Mwananchi, chini ya Theophil Makunga(sijui ni nduguye DC Novatus Makunga!), linaingia kwenye orodha yangu ya Magazeti yaliyo "Enemies of the people", pamoja na Uhuru, Mzalendo, Daily News, Sunday News, Habari leo, Rai, Al Nuur, na mengne ya mtazamo huo!
Mpumbavu huvunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe!
Sijui anajipendekeza ili afutiwe ile kesi ya uchochezi, aliyofunguliwa pamoja na Kibanda, baada ya makala ya Mwigamba Nov 2011?
 
theo kaaibisha kweli. Lakini pia ripoti hii imeonyesha ni jinsi gani ujinga bado upo miongoni mwa wasomi. Ripoti hii japo imeandikwa na wasomi, lakini wameshindwa kuficha ujinga wao ndani ya ripoti. Hata asiyesoma anauona ujinga uliopo ktk ripoti hii. Ni ujinga kweli kweli na tena ni ujinga haswa.

ndg hakuna utumwa mbaya duniani kama binadamu kuwa mtumwA wa nafsi yake.Theo ameamua kuwa mtumwa wa nafsi yake.anapoamua kutangaza bei yake hadharani.tunashukuru kwamba bei ya ndg Makunga na wenzake sasa tumeijua....wameamua kututangazia bila aibu kwamba bei yao.hawa ni watu wanaopaswa kulaaniwa vibaya...ndg zangu me nashindwa kupata neno sahihi la kuwaelezea watu hawa...siamini na haitatokea niamnini kwamba report hii imeandikwa na watu walowahi kwenda shule..ni report ya kupuuzi kuwahi kushuhudiwa ktk kizazi hiki na itabaki kuwa report ya kipuuzi hadi ukamilifu wa dahari
 
Jamani tusimlaumu sana, baada ya uchovu wa safari ndefu ya Canada mwenye INJI ataunda uDC usiyo na wilaya maalum kwa ajili yake, sasa angefanya nini? Niliposikia kwenye kamati kuna mhariri wa Mwananchi kwa mbali nilipata imani na naamini waliomteua walifanya makusudi kwa kudhani tutauamini uongo atakaousema. Shame upon him.
 
Huyu nae akikatwa hivyo vimikono vyake nafikiri ndio ata andika report nzuri kwa miguu!
Waandishi kama hawa ni kususia vigaazeti vyao tu!
 
nahisi harufu ya mpasuko wa wanahabari/vyombo vya habari kote nchini, sina tatizo sana na report coz ni kitu ambacho nilikitegemea na ingekuwa bora zaidi kama ingekabidhiwa kimyakimya na nchimbi nae akapiga danadana zake mambo yakaisha kuliko kuipa promo kwenye media, kubwa zaidi ni uwepo wa mtu kama T.Makunga kwenye ile kamati na mwisho wa siku na yeye akahusika kuandaa a useless report kama ile, labda tusubiri reaction ya waandishi/vyombo vya habari, but kwa kifupi wanachojaribu kufanya ni kujisafisha tu

Tundu lisu aliona mbali...wasiohona mbali wakampinga, nw this is the price.....big up Tundu lissu
 
Sisi watanzania jamani tunaudhi, ina maana kuna Mtu alitegemea tofauti na hii? Mlitakiwa mumshinikize kukataa kuwa sehemu ya kamati. Madam alikubali kuwa mwanakamati lazima awe sehemu ya hiyo ripoti. Lakini kwa nini tuhangaike kujadili hii ripoti wakati ripoti ya ukweli imetolewa na mct? Kujadili ripoti hii ni kuipa uhalali!
 
Na mimi sitanunua tena gazeti la mwananchi na citizen kutokana na maneno niliyosikia anaongea huyu makungu sijua amelishwa kungu, pumbafu yake, mshenzi sana,hana hata huruma kwa mwandishi mwenzake, shenzi kabisa.
Ripoti gani wanatuletea kama wanaogopa mahakama hiyo kamati ingevunjwa iachiwe mahakama imuachie huyo mtuhumiwa huru
 
Nilishangaa T. Makunga alipokubali kuwemo ktk kamati ya kihuni. Natabiri anguko la gazeti la Mwananchi kama huyu gamba atabakia mhariri wao mkuu!
 
...jamani huyo JAJI MSTAAFU aitwaye IHEMA ndo huyo aliyetajwa na Tundu Lisu kuwa alishindwa hata uwezo wa kuandika hukumu alipokuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Na huyu Teophilo MAKUNGA ndo huyo anayetuhumiwa kuwa ni gasho wa siku nyingi wa A. Kinana. Je hawa wadhaifu wawili mlitegemea kupata nini cha maana??
 
Watz tukilalama kuwa hatuna waandishi mnapiga kelele, sasa oneni wenyewe. Huwa nasikiliza wanayosema wakubwa, nakosa mtu wa kuuliza maswali magumu kwani waandishi wote huwa wanaandaliwa vibahasha ili wasiulize maswali...sasa kazi kwa Makunga!

mi nadhani tatizo kubwa ni kuwepo kwa kesi mahakamani ambayo anayeshtakiwa ni polisi hivyo kama alivyosema nchimbi ukitoa ripoti kwamba polisi wameua moja kwa moja yule polisi yupo hatiani kabla ya kesi kwisha,kosa la ufundi walilofanya ni kwamba baada ya kesi kuanza kusikilizwa wale wajumbe akiwemo makunga wangejitoa katika ile kamati
 
Gazeti la Mwananchi, chini ya Theophil Makunga(sijui ni nduguye DC Novatus Makunga!), linaingia kwenye orodha yangu ya Magazeti yaliyo "Enemies of the people", pamoja na Uhuru, Mzalendo, Daily News, Sunday News, Habari leo, Rai, Al Nuur, na mengne ya mtazamo huo!
Mpumbavu huvunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe!
Sijui anajipendekeza ili afutiwe ile kesi ya uchochezi, aliyofunguliwa pamoja na Kibanda, baada ya makala ya Mwigamba Nov 2011?

tufanye utafiti kabla ya kulipuka tunaidhalilisha jf,theophil na novatus wala hawana undugu kabisa ni majina tu kama akina masawe,masanja,kweka,matonya nk
 
Maskini Gazeti la Mwananchi!
Ndo mwanzo wa kuporomoka, na soon litashushwa bei na kuwa 500 kama mengne!
Unahongwa hadi unaharibu hadhi ya ofisi inayokupa daily bread!
Wapi Tido Mhando?
Chukulia hatua mhariri wako huyu!

usije shangaa makunga akafutiwa kesi yake ya uchochezi!
 
Haya magazeti ya Citizen na Mwananchi yalijijengea heshima kubwa sana yalipoanzishwa. Watu wa pande zote walijenga imani nalo baada ya magazeti hayo kujipapambanua kwa vitendo kuwa yamekaa kiweledi zaidi. Wengi wetu tulifurahi kuwa TZ nayo imepata magazeti makini.

Kwa kweli wale waKenya, akina Sam Sholei, walifanya kazi kubwa sana kuyajenga haya magazeti. Hata mnapokuwa kwenye pres conference, akasimama mwandishi wa haya magazeti, mtu ulikuwa unajipanga vizuri kumjibu. Ilifikia mahali tukategemea kuwa hata wakiondoka hawa waKenya, haya magazeti yataendelea na ueledi wao.

Kumbe siyo hivyo.

Walipooondoka tu, haikupita hata mwezi. Lilianza kuboronga gazeti la Citizen. Tunaoona tukalalamika ili wajirekebishe - wakakataa. Mimi binafsi, nimeacha kabisa kulinunua hilo gazeti. Hata nikiwa nasubiri kwenye reception yenye gazeti hilo, huwa siligusi.

Hivi sasa, gazeti la Mwananchi linakuja kwa kasi kuungana na magazeti ya udaku. Juzi tu wametengeneza habari ya Sumaye kuongea na Chadema. Wakikosa udaku, wanashabikia habari za uongo za ugunduzi wa dawa ya Ukimwi. Na sasa ona anachofanya mhariri wao.
 
Makunga, unaamini kilichomo katika ripoti?

Waandishi, muone sasa msivyoaminika na kujidhalilisha. Muulizeni huyu mwenzenu, simameni leo, kwa ngvu moja, muikatae.

Ndio maana mnadharauliwa.
 
Nilishangaa T. Makunga alipokubali kuwemo ktk kamati ya kihuni. Natabiri anguko la gazeti la Mwananchi kama huyu gamba atabakia mhariri wao mkuu!

Serikali ya CCM wajanja sana Theophili Makunga anakesi mahakamani na Jaji Ihema walitimuliwa kwenye kamati ya kugawa vitalu kwa kashfa ya kamati kupokea rushwa sasa unganisha dots utapata majibu lazima kamati iandike kwa mujibu wa bosi.

Lazima tuwadai hawajamaa fedha zetu za posho bila kazi.
 
aaaa mi sishangai si ndio hili huwa linaandika mambo ya zito k mara nyingi kuliko gazete lingine....
 
mwandishi ukiwa na bei na wanasiasa wakiijua bei yako lazima wakudharau! ndicho alichofanya theophil ,“the man is so cheap!”

Huyu si kuna wakati alikuwa na kesi au si huyu ? Nisaidieni kuweka kumbukumbu sawa tafadhali
 
Baada ya kusoma ripoti ya kamati ya Kitchen Party ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi nimebadili msimamo wangu wa jinsi nilivyokuwa namkubali sana Mhariri huyu wa gazeti lenye heshima ya mgongo wa chupa la Mwananchi.

Pia mtazamo wangu dhidi ya gazeti hili kuwa ni objective umebadilika pia, Mwanahabari mwandamizi kama Makunga kushiriki kuandika ripoti nyepesi kama ile, yenye kila viashiria vya elimu ya Ngumbalu kwa walioshiriki kuiandika ni kujidhalilisha na kujivunjia heshima. Nchimbi kakutumia kujisafisha na kulisafisha jeshi lake lakini aliyepoteza credibility ni wewe.

Sijui tatizo ilikuwa ni posho ya ushiriki wa kazi za tume lakini hii report ni nyepesi mno, no wonder jaji Ihema alishindwa kuandika hukumu wakati jaji.

..





...





.
Mie nakwambia ukweli kutoka rohoni mwangu....

Mwananchi ni gazeti la kihuni mno na waandishi wake wengi ni wahuni tu...

Kuna siku ntawaambieni uhuni wa gazeti hilo......kwa ushahidi wa wazi kabisa maana ninao!!!


....



..
 
Back
Top Bottom