Teophil Makunga umejidhalilisha mno kutumiwa na Nchimbi

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,396
7,968
Baada ya kusoma ripoti ya kamati ya Kitchen Party ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi nimebadili msimamo wangu wa jinsi nilivyokuwa namkubali sana Mhariri huyu wa gazeti lenye heshima ya mgongo wa chupa la Mwananchi.

Pia mtazamo wangu dhidi ya gazeti hili kuwa ni objective umebadilika pia, Mwanahabari mwandamizi kama Makunga kushiriki kuandika ripoti nyepesi kama ile, yenye kila viashiria vya elimu ya Ngumbalu kwa walioshiriki kuiandika ni kujidhalilisha na kujivunjia heshima. Nchimbi kakutumia kujisafisha na kulisafisha jeshi lake lakini aliyepoteza credibility ni wewe.

Sijui tatizo ilikuwa ni posho ya ushiriki wa kazi za tume lakini hii report ni nyepesi mno, no wonder jaji Ihema alishindwa kuandika hukumu wakati jaji.
 
Na mimi nimestushwa sn na ripoti hii.
Nguvu ya fedha na dola vimejionyesha LIVE kwenye hii ripoti.
 
Habari za mhariri huyo na gazeti la mwanainchi ni pesa mbele hata wewe ukiwa na pesa mpe atakuandika unavyotaka, sasa kwenye hiyo tume /kamati ulitegemea atafanya nini kama si kuwalamba miguu wakuu wenye inchi yao
 
theo kaaibisha kweli. Lakini pia ripoti hii imeonyesha ni jinsi gani ujinga bado upo miongoni mwa wasomi. Ripoti hii japo imeandikwa na wasomi, lakini wameshindwa kuficha ujinga wao ndani ya ripoti. Hata asiyesoma anauona ujinga uliopo ktk ripoti hii. Ni ujinga kweli kweli na tena ni ujinga haswa.
 
Ripoti imeonyesha sura halisi ya waandishi.

Niliposoma hitimisho ili nipate nguvu ya kusoma habari yote nilikosa hamu kabisa. Kama ni ukweli basi mengi yanahitajika kama ni nguvu ya madaraka na pesa basi poleni, mtawindwa kama swala na mkubali matokeompaka mjitoe kwenye hiyo minyororo
 
Maskini Gazeti la Mwananchi!
Ndo mwanzo wa kuporomoka, na soon litashushwa bei na kuwa 500 kama mengne!
Unahongwa hadi unaharibu hadhi ya ofisi inayokupa daily bread!
Wapi Tido Mhando?
Chukulia hatua mhariri wako huyu!
 
magamba hawana shukrani ngoja na yeye theophil wampige bomu ndio ataona madhara ya kununuliwa, ndio maana mimi gazeti la mwananchi huwa silisomi siku hizi ni kama uhuru na mzalendo.
 
Maskini Gazeti la Mwananchi!
Ndo mwanzo wa kuporomoka, na soon litashushwa bei na kuwa 500 kama mengne!
Unahongwa hadi unaharibu hadhi ya ofisi inayokupa daily bread!
Wapi Tido Mhando?
Chukulia hatua mhariri wako huyu!
Kama vile umenisoma mawazo.
Hii report imeandaliwa na watu wa TISS kisha kina Theo wakapewa tu waisaini.
Mawazo ya Theo hapa ni tofauti na michango ya waandishi wake kama kina Meena, Cherehani, Mabala n.k.

Sijui Theo utawaangalia vipi watu wako hawa kwa kukubali kwako kudhalilishwa kwa kiwango hiki.

Yaani nimeiosoma nikafikiri labda Theo ulitumwa dukani ndio wakaibadilisha, siamini kama umeshiriki humu.
 
Maskini Gazeti la Mwananchi!
Ndo mwanzo wa kuporomoka, na soon litashushwa bei na kuwa 500 kama mengne!
Unahongwa hadi unaharibu hadhi ya ofisi inayokupa daily bread!
Wapi Tido Mhando?
Chukulia hatua mhariri wako huyu!

Yaani mkuu, nia aibu sana sana, Looo! Afu ITV wamewavua nguo kabisaaa, kwani wakati wanasoma hiyo taarifa yao ya kupika kwamba polisi hawakuhusika, hapo hapo wakawa wanaonyesha ile picha walo mzingira na mmoja akimuonyesha mtutu ulo mmaliza, yaani hata mtoto mdogo wa darasa la nne aloona ameniuliza hivi mbona picha inaonyesha polisi wanaua halafu ripoti inadai hawakuhusika? ... ni aibu aibu na nadhani ni haki yao hata wakipta mtaani tuwazomee!
 
Mimi nilisoma ripoti ya MCT kwanza tena neno kwa neno. Baadaye kusikia ya Nchimbi imetoka nayo nikasema ngoja nijaribu. Binafsi nimeshindwa kuisoma ile ripoti ya Nchimbi. It's rubbish, total ****! Hata sijui imeandikwa na mtoto wa form ngapi? Kwa kweli nimekereka mno.
 
Kwani nyie hamkusoma Hitimisho? Hitimisho la ripoti ni Maoni aliyotoa Wilson Mukama. Sasa kuna Kamati hapo!
 
Ushauri kwa mmiliki wa gazeti la Mwananchi. Amuondoe huyu mtu ofisini haraka sana, vinginevyo hilo gazeti watasoma wenyewe.
 
Hiyo kamati imetumia pesa za walipa kodi kuficha ukweli amboa hata kipofu anauona. Halafu nyuso zao kavu hata aibu hawana. Wamedhalilisha taaluma zao kwa kiwango kikubwa mno.
 
nahisi harufu ya mpasuko wa wanahabari/vyombo vya habari kote nchini, sina tatizo sana na report coz ni kitu ambacho nilikitegemea na ingekuwa bora zaidi kama ingekabidhiwa kimyakimya na nchimbi nae akapiga danadana zake mambo yakaisha kuliko kuipa promo kwenye media, kubwa zaidi ni uwepo wa mtu kama T.Makunga kwenye ile kamati na mwisho wa siku na yeye akahusika kuandaa a useless report kama ile, labda tusubiri reaction ya waandishi/vyombo vya habari, but kwa kifupi wanachojaribu kufanya ni kujisafisha tu
 
Watz tukilalama kuwa hatuna waandishi mnapiga kelele, sasa oneni wenyewe. Huwa nasikiliza wanayosema wakubwa, nakosa mtu wa kuuliza maswali magumu kwani waandishi wote huwa wanaandaliwa vibahasha ili wasiulize maswali...sasa kazi kwa Makunga!
 
Back
Top Bottom