Teodoro Nguema Obiang Mangue: Mtoto wa Rais mwenye maisha ya kifahari kwa fedha za ubadhirifu

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
847
1,000
Huyu jamaa si ndiyo kuna wakati alikuwa yupo kwenye mahusiano na Eve (Eve Jihan Cooper) wa Ruff ryders?
Warembo wengi wakali duniani anavinjari nao. Kuna wakati huwa anakataliwa kuingia katika baadhi ya nchi makini duniani kutokana na ukubwa wa msafara wake na mabegi mengi mno ya pesa taslimu (hususan $, £ na €)!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
847
1,000
Hii hali inatuonyesha jinsi sisi waafrika tulivyo tofauti kabisa na wazungu maanake hapa mwafrika anawapora wananchi wenzake na kwenda kuficha uzunguni.

Ilhali wazungu nao wanampokonya na kuwarejeshea wananchi wenzake aliyowapora kisha tena utasikia wananchi hao hao waliopororwa wakiwalaumu tena wazungu kwa umaskini wao.

Ama kweli sisi waafrika tuna kila sababu ya kuwa kama tulivyo kwa sababu mchawi wetu ni sisi wenyewe.
Kweli kabisa!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 

baba-mwajuma

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
485
1,000
Huo ufilisi angefanyiwa na muafrika mwenzake tungemsema mfilisi anaroho mbaya....
We Huwajui Wafaransa Mkuu, kwenye Unafiki na ku pretend Wana A+,

Wapo Wazungu wazuri ambao hawana Time na Kunyonya Africa kama Nchi za Scandinavia kina Norway na Finland, wanatusaidia sana, ila Hao Kina Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji na nchi nyengine za magharibi wengi wanafiki tu.

Kama Ufaransa angekuwa anawajali kweli angeanza na TOTAL si kampuni ya Ufaransa hii? Maana kila siku ina scandal za wizi wa Mafuta huko Guinea.
 

mbalaka

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
2,116
2,000
Kuna clip moja inatembea, jamaa wa Barrick wanasema wanavyoinyonya Tanzania hata wenyewe wanaona aibu. Lakini vyote wamepewa ki halali na wanasiasa.
Huitaji kuunda Vikundi vya kijihadi kupora rasimali za Africa, we dili na wanasiasa tu.. Utachota unachotaka hadi aibu ikushike.
 

The imp

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
12,712
2,000
Tukikumbuka maisha ya kidhalimu ya Mobutu Seseseko na jinsi alivyoishia kubaya, ni dhahiri huyu Teodorin na babaye wataishia kubaya sana.

Baba yake ni dhalimu aliyepanda dhuluma kubwa dhidi ya watu wa Guinea ya Ikweta tangu 1979 alipompindua nduguye.

Hakika atavuna udhalimu maana apandacho mtu ndicho avunacho.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Babaye na teodorin alipata madaraka baada ya kumpindua baba take mdogo nae anaitwa obiang nguema.

Mahakama ya kijeshi eqoutorial guinea iliamua auliwe kwa kupigwa risasi.

Since then yuko madarakani Wala Hana mpango wa kutoka

Madiktea was afrika

Akina obiang nguema

Denis saso ngueso

Akina bongo ondimba

Kagame

Museveni

Kiir

Derby

IBK

Paulo biya

Ccm
 

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,615
2,000
View attachment 1873547 Kwa miaka mafanikio ya Teodoro "Teodorin" Nguema Obiang Mangue yaliwiana na mafanikio ya nchi yake Equatorial Guinea, kama ilivyopanda na kuboreka kama mzalishaji mkubwa wa mafuta katika Kusini mwa jangwa la Sahara
Mtoto wa Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo anafurahia maisha yake ya kifahari huko California na Ufaransa.

Maisha yake hayo mazuri ni tofauti kabisa na maisha ya wananchi wenzake wengi, ambao wanafaidika kwa kiasi kidogo na mapato yatokanayo na mafuta.

Mtindo wake wa maisha na matumizi yake yanatajwa kuhusishwa na ubadhirifu ambapo sasa Teodorin anakabiliwa na hatia ya makosa ya kiuhalifu nchini Ufaransa, vikwazo nchini Uingereza na rekodi mbaya ya rushwa nchini Marekani.

Lakini nchini kwake, Teodoro mwenye umri wa miaka 52 anaendelea kusalia kuwa makamu wa rais, akijiandaa kuchukua urais kumrithi baba yake mwenye umri wa miaka 79.

Vitendo vya ubadhirifu na ulafi​

Teodorin aliishi California mwaka 1991 alipojiunga na Chuo Kikuu cha Malibu.

Akanunua nyumba la kifahari la thamani ya dola $30m huko Malibu na vitu vyake vingine alivyokuwa navyo Marekani ni pamoja na gari la Ferrari na vitu vya thamani vya kumbukumbu ya mwanamuziki Michael Jackson.

Haya yalibainika mwaka 2014 alipoamriwa na mahakama nchini Marekani kusalimisha mali hizo baada ya kubainika zimetokana na matumizi yake ya fedha zinazonuka rushwa.

View attachment 1873545
Kufuatia ubadhirifu na ulafi usiokoma, Makamu wa Rais Nguema Obiang bila aibu aliipora serikali na kufunga biashara nchini mwake ili kusaidia maisha yake ya kifahari nje, wakati wananchi wake wengi tu wakiishi kwenye umasikini wa utupwa," alisema mwanasheria mkuu msaidizi wa serikali Jenerali Caldwell.

Fedha zilizotokana na kuuza mali za serikali zilipaswa kutumika kwa faida ya watu wa Guinea ya Ikweta ".

'Hakuna tena maisha ya kifahari'​

Mwaka 2016, waendesha mashtaka wa Switzerland walikamata magari yake 11 ya kifahari. Baadhi ya magari hayo; Bugatti, Lamborghinis, Ferraris, Bentleys na Rolls Royce - yaliuzwa kwenye mnada kwa $27m. Kiasi cha $23m kilipaswa kwenda kusaidia miradi ya maendeleo nchini Guinea ya Ikweta.

Baadae mwaka 2017, ilikuwa zamu ya Ufaransa kumbana Teodorin, alikutwa na hatia na mahakama ya ubadhifu wa fedha na kuamuru kukamatwa kwa mali zake nchini humo.

Licha ya kutokuwepo Mahakamani, alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu, faini ya dola milioni 35, na mali zake za kifahari Ufaransa zilikamatwa. Moja ya mali zake zilizokamatwa Paris ilikuwa na thamani ya zaidi ya dola $120m.

Kwa mujibu wa sheria za Ufaransa, utajiri wote huu uliokamatwa unapaswa kugawanywa kwa watu wa Guinea ya Ikweta.

Hukumu hiyo iliungwa mkono na mahakama ya juu ya rufaa nchini humo, iliyokataa rufaa yake ya kudai kwamba hana hatia na hoja zake kwamba mahakama ya Ufaransa haina haki ya kuamua kuhusu mali zake.

Kwa maamuzi haya Ufaransa sio tena mahala pa kufujia pesa zilizoibwa na viongozi wa juu kutoka nje na wasaidizi wao," alisema Patrick Lefas kutoka shirika la Transparency International France.

Wiki iliyopita, Uingereza iliongeza pigo lingine kwa Teodorin kwa kumuwekea vikwazo yeye na viongozi wengine kutoka Zimbabwe, Venezuela na Iraq.

Uingereza ilisema mali zake za kumbukumbu ya Michael Jackson ilikuwa ni pamoja na vikinga mkono au glove zenye thamani ya dola $275,000, glove hizo zilivaliwa na mwanamuzi huyo wakati wa uhai wake kwenye ziara ya tamasha lake lililoitwa 'Bad Tour' katika miaka ya 1980s.

Vikwazo hivyo vya Uingereza vinahusisha kukamata mali, kupiga marufu kupitisha fedha kwenye mabenki ya Uingereza na kusafiri kuingia nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Dominic Raab alisema vikwazo hivyo vipya vinawalenga watu hao 'waliojipatia fedha na mali kwa gharama wa wananchi".

Onyo kwa wengine​

Licha ya kukabiliana na mashitaka nje ya nchi, Teodorin anaendelea kusalia na nafasi yake kwenye siasa za Guinea ya Ikweta. Baba yake ni kiongozi aliyekaa madarakani muda mrefu zaidi Afrika na anaelezwa na mashirika ya haki za binadamu kama mmoja wa madikteta katili Afrika.

"Wakati Rais akiwa mtu muhimu, mtoto wake anafamika zaidi Afrika Magharibi na Afrika ya kati kutokana na kuvivutia sana vyombo vya habari vya kimataifa ", anasema mchambuzi wa Afrika, Paul Melly.

"Hatua zilizochukuliwa na mahakama katika baadhi ya nchi za Ulaya dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyofanywa na familia za marais wa Afrika ni ishara zinazoweza kuzikumba baadhi ya nchii kwa kupoteza uaminifu na kukosa fedha za maendeleo ," aliongeza.
"Lakini masuala haya wala hayazungumwi na kujadiliwa sana katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara ".
Mijitu kama hii kuanzia ma Raisi wastaafu,inabidi tuwakamate,tuwale Tigo harafu wao na familia zao,tuwafukuze nchini,waondoke na nguo walizovaa tu,pesa mali zote zinataifishwa kama mali ya umma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom