"Tengua kauli".... "Sitengui"

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,789
1,782
Hakimu mmoja ndugu yake alikuwa na kesi ya wizi wa kutumia nguvu. Akawa anahaha jinsi ya kumnusuru na kifugo.Baada ya majadiliano na mtuhumiwa akapata namna. Akasubiri siku ya kesi. Siku ilipowadia kesi ikasomwa: '**** unatuhumiwa kwa kumvamia **** nyumbani kwake na kupora *** baada ya kumtishia na kisu.Baada ya kesi kusomwa hakimu akamuuliza mtuhumiwa:
Hakimu: 'Una lolote la kusema?'
Mtuhumiwa: 'Kwanza wewe unayeniuliza sikutambui maana huna sifa za kuwa hakimu,ulipewa kazi hiyo kwa kuhonga na unatumia vyeti bandia. Kwa hiyo huna sifa ya kunihukumu'.
Hakimu: (baada ya kushusha pumzi)' Una hakika na hayo unayoongea?'
Mtuhumiwa: 'Nina hakika!'
Hakimu:' Unaweza ukatoa ushahidi wa maneno yako?'
Mtuhumiwa: 'Sina ushahidi'
Hakimu:'Basi kama huna uhakika na ulichoongea, tengua kauli yako mara moja tuendelee na kesi'
Mtuhumiwa:'Sitengui'
Hakimu: 'Nakuamuru tengua kauli yako'
Mtuhumiwa:' Nimesema sitengui'
Hakimu: 'Kwa hiyo kwa kuwa umeamua kunidhalilisha mimi na kuidhalilisha mahakama, natumia mamlaka niliyo nayo kukufukuza mahakani kwa hiyo huruhusiwi kuhudhuria vikao vya mahakama kwa muda wa mwaka moja. (hakimu akawaamuru askari wamtoe nje ya mahakama). Kilichofuata....ikawa mwisho wa kesi!
Baadaye hakimu na mtuhumiwa walikutana baa wakagongeana na kuendelea kunywa!!!
 
Back
Top Bottom