Tengeneza Urafiki na watu wanaofanya biashara unayoifanya au utakayotaka kuifanya "utafanikiwa"

Mjasiriamali communication skills kwake ni nguzo imara. Yaani ni mswahili mwenye hoja na ukikaa vibaya unaweza nunua vitu vingi kwake kuliko ulivyotegemea maana yeye anakutengeneza kwa maneno vilivyo. Hivyo kukaa na mtu yeyote na kuzungumza naye na kufikia muafaka ni jambo la kawaida maana ana uwezo mkubwa kisaikolojia.

Ngoja nikamtafute Member mmoja alishawahi niambia nimpe tofauti ya Mjasiriamali na Mfanyabiashara

Kwa nondo hii asipoelewa au ambulia chochote atakua ana "namna",Asante Mr. Purpose kwani jibu hili limempa mtu elimu kubwa.
 
Mkuu mtoa mada yupo sahihi.

Kwanza lazima ukubali na kuelewa kuna utofauti mkubwa kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara.

Mjasiriamali ni mtu mbunifu, mwenye uwezo mzuri wa kushawishi, mtu wa kujifunza kila kukicha, mtu anaye tafuta mbinu mpya kila siku ili kuongeza mafanikio katika kile anachifanya. Mjasiriamali ni mtu mjanja sana na kupitia ujanja na ubunifu alio nao anaweza kupata taarifa anayoitaka kutoka kwa mtu anayefanya kile anachokifanya either moja kwa moja kwa kumuuliza muhusika au kupitia njia nyingine.

Mjasiriamali ni jasusi wa kujitegemea.

Mjasiriamali ni mtu asiye na wivu wa kijinga kwa yule aliyemzidi au anayefanya vizuri zaidi yake, na mjasiriamali hupenda kukaa karibu na wale walio juu yake ili kujifunza kupitia wao. Mjasiriamali ni mtu mwenye mtazamo chanya na malengo dhabiti katika kazi yake.

Mjasiriamali ni mtu ambaye kichwa chake muda wote hakitawaliwili na faida ya biashara tu bali mbinu za kukua na kufanya zaidi katika biashara.

Mjasiriamali ni mfanya biashara bora zaidi.

Narudi kwa MFANYABIASHARA.

Huyu ni yule anayefanya biashara YOYOTE KWASABABU ANAYO PESA (MTAJI) WA KUFUNGULIA BIASHARA HIYO.

Mfanyabiashara ni mtu mzamiaji popote na haoni ajabu kuhamahama bila sababu na pia huwa anakosa mbinu za kufanya biashara yake ikue zaidi.

Mfanyabiashara anaamini ili apate faida kubwa lazima awe na MTAJI mkubwa, na mara nyingi mbinu kwake za biashara siyo kipao mbele sana.

Mfanyabiashara anahitaji elimu ya biashara ili kuwa mfanyabiashara bora au kufika level ya mjasiriamali.

Mfanyabiashara anawaza faida kila wakati na akikosa faida kwa muda fulani mfululizi lazima atafunga hiyo biashara na kuamia kwingine.

Kwa uchache nadhani unaweza pata picha. Na mfano mzuri wa mjasiriamali ni huyu CONTROLA.

Mjasiriamali communication skills kwake ni nguzo imara. Yaani ni mswahili mwenye hoja na ukikaa vibaya unaweza nunua vitu vingi kwake kuliko ulivyotegemea maana yeye anakutengeneza kwa maneno vilivyo. Hivyo kukaa na mtu yeyote na kuzungumza naye na kufikia muafaka ni jambo la kawaida maana ana uwezo mkubwa kisaikolojia.
Tofauti ni ipi hapo kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali?

Nakuomba kwa faida ya wengine utuwekee tofauti kati ya (1)machinga
(2)mjasiriamali

(4)mfanyabiashara

one one
Msonjo Khan
 
Kufanya biashara kila mtu anaweza ila shida inakuja kwenye kudumu katika biashara mtu anayofanya na si tu kudumu ila kufanikiwa katika biashara aliyodumu akiifanya.

Watu wengi ni wafanyabiashara ila ni wale watu shika hiki acha shika kile acha (mapepe) kuna mtu anafungua biashara ila hana target ya biashara anayoifanya baada ya mwaka au miaka awe sehemu flani,HANA kbisaaa, sasa mimi sielewagi huyu mtu anafanya hiyo biashara ili nini?!

Ok iko hivi, watu lengo kuu la kufanya biashara ni ili watu tupate PESA hilo ndio lengo,mengine yote yaje ila pesa ndio lengo la kila mtu anapofungua biashara yyte ile. Shida ni moja kwa wafanya biashara wengi hawataki kuwa wavumilivu na mwisho hupotea kwa miluzi ya biashara za wenzao."Miluzi mingi......"

Ninaposema uwe na marafiki wanaofanya biashara kama yako namaanisha nini?

Kama kweli wewe unaipenda hiyo biashara yako au unaipenda sana sana biashara unayoiwaza hapo kichwani mwako sasa hivi basi muda wako wakuhakikisha unafanikiwa ktk hiyo biashara unayoifanya au unayotaka kuifanya ni sasa.

Naomba nitoe mifano kidogo ili tuelewane:

Mfanyabiashara wa NGUO ZA MTUMBA wewe marafiki zako asilimia 81 wanatakiwa wawe wauza mitumba wenzako,

Kwanini?

Kwasababu kuwa na marafiki wanaofanya biashara yako itakusaidia sana sana sana kujua vitu gani vyakununua ukienda sokoni,nguo gani zinatoka sanaaa na nguo gani hazitoki sana urafiki wako na wenzako utakusaidia mambo mengi sana tofauti ukisema ukomae kuwaza mwenyewe nini ununue na nini usinunue.

Ukitaka kukomaa mwenyewe kuwa think tank of your own business bila kupata idea toka kwa wenzako wanaofanya biashara kama yako ujiandae kukumbana na hasara sana na kama kimtaji chako ndio cha "Mungu nisaidie" ujue huna round unapotea.

Mfanyabiashara wa VIFAA VYA SIMU wewe marafiki zako pia 81% wawe wauza vifaa vya simu wenzako,

Kwanini?

Kwasababu kujuana na wenzako kutakusaidia kujua hata ni machimbo gani yana vitu bei rahisi, biashara ili ufanikiwe faida ndio hukuinua toka ulipo kwenda hatua ya juu Kubali kataa hapo unaponunua vitu vyako vya dukani kwako,kuna sehemu huijui inauza vitu hvyo hvyo unavyonunuaga kwa bei ya chini kuliko hilo duka unaloenda..Je unajua hilo duka lipo wapi?

Watu tumetofautiana kuna tunaochukua mzigo China, Nairobi, Kariakoo, Congo,nk ok mimi nachukulia mzigo wangu Kariakoo nanunua earphones 1 piece kwa 700,wewe unachukua mzigo k.koo hiyo hiyo unachukua earphones hizo hizo kwa 1000,kuna mwingine nae anachukua mzigo k.koo anachukua earphones hizo hizo kwa 1200.

Hawa watu watatu wanachukua mzigo soko 1 bidhaa 1 lkn kila mtu ananunua kwa bei yake, Ndio wote wakienda kuuza wanapata Faida lakini hata siku 1 huwezi mlinganisha mnunua earphones kwa 700 na mnunua earphones kwa 1200 utegemee hawa watu maendeleo yao kibiashara yatakua saawa.

Wabongo tunaitana sana wachawi, tumeloga, kisa tu wewe umefanya biashara flani kwa muda mrefu haijakutoa ila kaja mwenzako kaifanya ndani ya mwaka imemtoa kimaisha unaanza muita mchawi, kaloga, nk wakati shida ni wewe mwenyewe.

Mtu ni mama ntilie badala awe na marafiki mama ntilie wenzake yeye marafiki zake ni waajiriwa wa BANK tena BOT na ni mfanyabiashara wa Nguo za watoto,mwingine ni muuza magari,mwingine ni mtu wa saloon kubwa sana inajulikana town,nk wakikutana hawa watu kila mtu atakua anasimulia faida na mfanikio ya biashara yake mwenye nguo atasimulia anavyopiga pesa, mwenye saloon atasimulia namna make up ina hela siku hizi, nk nk

Huyu mama ntilie yeye kwenye biashara yake ana karibia wiki nzima haelewi wateja wameenda wapi,kila siku anapika msosi unabaki, anapka mandazi hayatoki,kila chakula anapka kinabaki, sasa akiskia wenzake wanavyosifia mafanikio wanayoyapata kwenye biashara zao utamuona na yeye kimoyo moyo kimya kimya anapata "idea" ya kufungua saloon kama ya rafiki ake ili na yeye apige hela kama mwenzake.

Anasahau shida si kufungua saloon shda ni mbinu za kupata faida kuptia hiyo saloon, yeye badala awaze anafanyaje ili mama ntilie yake iinuke isimame juuu anawaza kuanza biashara nyingine.

Yote hii n kwasababu ya miluzi mingi (kuwa na marafiki wasio deal na biashara unayoifanya) huyu mama ntilie angali angejua kuna mama ntilie ananunua mchele kwa buku mchele anaonunua yeye 1700, laiti angejua kuna mtu wa machinjioni analetaga nyama kwa oda Kilo 1 anakuuzia 4500 badala ya 6000 buchani sidhani kama huyu mama ntilie angekosa faida kwenye biashara yake.

Shida n kwamba watu wana marafiki wasiofaa katika biashara zao,unapokua na marafiki wanaofanya biashara yako watakusaidia vitu vingi hasa upatikanaji wa bidhaa unayouza,bei hata na ubora wa bidhaa husika.

Hivi hujawahi ona kuna duka k.koo ukienda ukiulizia kitu flani akikwambia HAMNA my dear utazunguka k.koo nzima na hutopata? ushawahi kwenda nairobi ukakuta duka flani ukamuuliza una bidhaa flani akakujibu hiyo HAIPO na kweli hata uzunguke nairobi nzima hutopata hiyo bidhaa, unahisi inakuaje anajua hicho kitu hakipo?

Anakwambia kwa kujiamini kbisa Huwezi pata hicho kitu,na kweli hupati Si kwamba yeye n mchawi ila n kwamba ana connection na marafiki wanaofanya biashara kama yake.

Marafiki wenye mawazo ya biashara tofauti na biashara tunazofanya si wazuri kwa afya ya biashara yako,hatunyimwi kuwa na marafiki ila hapa naongelea urafiki wa kibiashara ule ambao mkikutana mnapga story za faida ya Lotion Faida za Perfume za kupima,nk

Siongelei urafiki ule wa shost flani na flani ule wa kupga umbea na stori zenu za kimaisha hapana huo urafiki wa hivyo unaweza kuwa na rafiki yyte yule ila linapokuja swala la biashara unatakiwa uchuje marafiki.

Jua ni yupi wa kua nae rafiki yupi wa "mambo,poa" sio upo umekaa mwakani unataka kuanza biashara ya kuuza Mtindi na Maziwa fresh,halafu kampani yako n marafiki wauza Rasta,wauza body spray,wauza viatu,wauza,saa,nk itafika mwakani utafungua hiyo biashara yako ya maziwa fresh na mtindi ila nakuhakikishia HUTOBOI, kwanini? huna mbinu,huna idea ya wapi maziwa yanaptkana kwa wingi na bei rahisi,huna vitu vingi sana kuhusu biashara utakayokuja ianza.

Anza sasa hivi kubadilisha marafiki,kuna watu wengi nawajua leo hii wameacha biashara zao kwasababu ya hili ninaloandika hapa na wamehamia kufanya biashara walizokua wakifanya marafiki zao, nawajua na nawaona ambavyo wanapoteza muda maana najua hawana round wataacha hizo biashara tena watahamia biashara zingine.

Mtafute mfanyabiashara aliefanikiwa muulize ameshafanya biashara ngapi hadi kafika hapo alipo,Ukiona kaanza kukwambia sjui nilishonaga viatu,nikauza juice,nikauza mtumba,nikapga debe, nk Mpe X huyo anakudanganyaaaaaaaaa...

Mfanyabiashara mkweli atakwambia nilianzaga na kuuza chips nikayumba yumba ila nikakomaaa na leo hii nina biashara zingine nafanya ila Chipsi ndio msingi wa kila kitu (umeona utofauti) si kwamba hafanyi biashara zingine "hapana" anafanya kuptia maendeleo aliyoyapata kuptia kuuza Chipsi.

Hao ndio wafanyabiashara waliofanikiwa husimama na biashara moja Hufanikiwa kwenye biashara 1 atayumba ataanguka akiinuka tena atarudia ile ile biashara aliyokua akiifanya Hayumbishwi na idea na mawazo ya watu wengine.

"Ndege wafanano huruka pamoja" tafuta ndege unaofanana nao mruke pamoja,hao marafiki zako wengine waongo wanakupoteza unauza zako genge wanakwambia hupat faida kama wao wanauza Mkaaa,kumbe wenzako mkaaa ni geresha tu Mchana ikifika usiku wana Madanga 100 kidogo,ili akuonyeshe anapata hela zake kupitia mkaaa ni lazima asifie sana mkaaa una faida,sasa na wewe kwa kuwa mapepe kisa unaona biashara yako haiendi unaacha unaingia kuuza mkaaa kisa tu "mtaji unao"...Biashara si mtaji Pesa tu Guys biashara inahtaji vitu vingi sana ili isife. isianguke.

Leo naomba niishie hapa ila kwa wale wabishi komaeni na ubishi wenu kwa wale mnaoona Kuna chakuchukua chukueni,na wale mnaodumisha neno la Mungu "upendo wa ndugu na udumu" basi tuendelee kuwa na marafiki woteeee "akili kumkichwa" tusiitane wachawi please Biashara ikikushinda Funga kajipange upya acha nyooshea wenzio vidole.

That's my bro CONTROLA 💥
Nakuelewaga sana wewe..... akili kubwa
 
Nimekupata mkuu. Sema kuna watu masnitch we Acha.

Jamaa anajuana na mwwnye frem. Ananidalalia fremu just because anajuana na mmiliki. C unajua mjini kila kima ni dalali.
Mi najiuliza nn cha kufungua namaliza kujiuliza nampigia jamaa nakuja twende tukalipe kwa mwenye fremu. Jamaa ananiambia wahi watu wengi wanaitaka fremu.Najiandaa nikalipe mara paap meseji. "frem ishachukuliwa, mwenyewe anasema" Duh nkasema baasi sio rizki.

Siku zikapita. Mara paap kwenye ile fremu naona matangazo biashara xxx opening soon. Mimi hapo hapo kama meter kadhaa labda 150m hivi nna duka langu lingine nauza bidhaa hiyo hiyo xxx.
Nikasema yalaaaaa nshapata mshindani. Nikasema poa kila mtu na rizki yake.
Siku zikapita maraaaa ...surpriiiiiseee... kumbe Yule dalali fake kanizunguka kachukua hiyo fremu on top of that kafungua biashara km yangu vile vile yaani. Kwanza alinidanganya ilishachukuliwa kumbe ni yeye bhana.

Akawa kila nikipita anainama chini kama kondoo ila mi nkamuambia wife don't worry tukomalie ubora km siku zote coz we are established more than him yeye wa juzi tu.

Nadhani mnaelewa hapa... tatizo c kufungua biashara km yangu ...this is very acceptable kua na competitor. But the nature nliompata huyu competitor raised my eyebrows.

Halaf akaanza kuja kuulizia apate ujuzi kwangu kupitia muuzaji wangu. Baasi nikatoa biti Kali kwa muuzaji wangu sitaki kukuona unampa Siri za Aina yoyote. aende mbele uko akatafte info kwa wengine.

Mr CONTROLA unataka nishirikiane na huyu paka.????!!!! Not in this case jamaangu sio kwa u snitch huu. Km angekua tu mtu mwingine Sawa. Ndio maana nimeikubali mada yako very educative but sio kwa mtu km huyu.
 
Uzi uliopita ulisema acha kutoa siri ya biashara Kwa wafanya biashara wa bidhaa kama yako leo hii Unasema Kua namafiki na watu wanaofanya biashara kama yako hili wakupe mupeane siri za biashara Mi nakupa (X) sijaelewa hapo unamahanisha nini biashara ni ushindani kujishusha kwa mfanya biashara kama yako ni Kujindaa Kudondoka Uwezi pata ukweli kwa mtu anayefanya kitu kama unachofanya wewe.
Unajua ukweli wa mambo
 
Mzee controla location ya kuuzia vifuniko vya asali ni mbagala. Wauza vyupi ni wengi mno...nimeanza kwenye goli la barabarani nimewekeza capital ya 1.3m...ningeshukuru kupewa ujanja zaidi
kokudo huyu mwanafunzi sio wako kweli!

Naamini una mmudu hebu msaidie kuna siku hakuwepo darasani...

Mr.Clever utamshukur huyo mtu maana akija hatokunyima siri za kambi...
 
Mzee controla location ya kuuzia vifuniko vya asali ni mbagala. Wauza vyupi ni wengi mno...nimeanza kwenye goli la barabarani nimewekeza capital ya 1.3m...ningeshukuru kupewa ujanja zaidi
Mkuu unataka ujanja wa kuongeza thaman au namna ya kujitangaza?

Kwa natural ya hapo unahitaji mambo hayo mawili ni muhimu
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom