Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,811
- 2,763
Tenga: Jezi mali ya mchezaji Taifa Stars
Habari Zinazoshabihiana
.... Jezi za 'Kikwete' zakabidhiwa TFF 04.01.2007 [Soma]
Athuman Idd atafune jongoo kwa meno - Tenga 19.01.2007 [Soma]
Tenga awapasha wachezaji Stars 13.09.2007 [Soma]
*Ampa tano Cannavaro kumvulia jezi Eto'o.
Na Erasto Stanslaus
RAIS wa Shiriksho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amempongeza beki wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Nadir Haroub 'Canavaro' kubadilishana jezi na mchezaji wa kimataifa wa Kameruni, Samuel Eto'o katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika 2010 uliofanyika mjini Younde, Kameruni.
Baada ya mchezo huo kumalizika 'Cannavaro' alifuatwa na Eto'o anayecheza klabu ya Barcelona ya Hispania akitaka wabadilishane jezi baada ya pambano hilo kumalizika ambapo Stars ilichapwa mabao 2-1 yaliyofungwa na mchezaji huyo.
Tukio hilo limeibua mjadala baada ya Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage akikaririwa na vyombo vya habari akisema 'Cannavaro' atakatwa sh. 20,000 kwa kitendo cha kubadilishana jezi na Eto'o.
Mchezaji mwingine iliyeingia katika mzozo huo ni Jerry Tegete ambaye alibadilishana jezi na mchezaji Jean Makoun wa Kameruni anayevaa 11. Tegete alivaa jezi nambari 10 katika mchezo huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Tenga alikata mzizi wa fitina na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na sakata hilo na alimpongeza beki huyo akisema amefanya kitendo cha kishujaa kutoa jezi ya Taifa bila kujali kama atadaiwa au la.
"Canavaro amefanya kitendo cha kishujaa kwani sasa tunakwenda na wakati kwani angekataa kutoa jezi kwa kuhofia kudaiwa ulimwengu usingetuelewa na kutoa jezi ni kuitangaza nchi," alisema Tenga.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa, alisema kuanzia sasa TFF imepitisha uamuzi kila mchezaji wa Stars ataondoka na jezi aliyovaa siku ya mchezo bila kujali alicheza uwanjani au la baada ya pambano kumalizika na itakuwa mali yake.
Tenga alisema kimsingi waliokuwa wakimdai 'Cannavaro' jezi hiyo walikuwa wakitimiza wajibu waliojipangia kati ya uongozi wa Stars na wachezaji lakini alionya kuwa walishindwa kuangalia mazingira halisi ya tukio husika.
Baadhi ya wadau wa mpira wa miguu wameuponda uongozi wa TFF kutokana na kitendo hicho hicho na walikuwa tayari kuwalipia gharama za jezi hizo 'Cannavaro' na Tegete.