Tendwa:Tumechoka sasa una mamlaka kemea waongo hawa dhidi ya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa:Tumechoka sasa una mamlaka kemea waongo hawa dhidi ya Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, May 23, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  NA SOLOMON MWANSELE, MBEYA

  WAUMINI wa dini ya Kiislamu mkoani hapa, wametahadharishwa kuhusu mwenendo wa Chadema, kuwa kinahamasisha kuibuka vurugu nchini na kuwa chama hicho ni hatari, kwani kimedhamiria kuiingiza nchi katika machafuko. Imeelezwa kuwa dhamira ya Chadema kama chama chenye mrengo wa dini fulani, ilijionyesha dhahiri wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, ambapo dini hiyo ilitumika kukifanyia kampeni.
  Tahadhari hiyo ilitolewa na Sheikh Hassan Katanga kwenye hotuba ya sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Forest jijini hapa.

  “Si vyema waumini wa dini ya Kiislamu kukiunga mkono Chadema… chama hiki ni hatari na hakina dhamira nzuri na nchi yetu,” alisema Sheikh Katanga .
  Aliongeza kuwa kwa mwenendo halisi wa Chadema ulivyo, inaonyesha wazi kuwa kinataka kuweka utawala wa dini hiyo (jina linahifadhiwa), kwani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, kampeni zilikuwa zinafanywa na viongozi wengi wa dini husika.
  Kwa mujibu wa Katanga, waumini wa dini ya kiislamu wanapaswa kutokiunga mkono kutokana na kujipambanua kuwa kipo kwa ajili ya kuupiga vita Uislamu na kwamba hata maandamano ya chama hicho kwa nchi nzima hayana dhamira njema.
  Aliongeza kuwa maandamano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, yana lengo la kuwachochea wananchi ili kujiingiza katika vurugu.
  Sheikh Katanga alisema mikutano ya hadhara na maandamano ya Chadema, kimsingi hayana mantiki, kwa wakati huu ambao uchaguzi mkuu umemalizika na wananchi wamewachagua viongozi wanaoona wanafaa kuwaongoza.
  Alisema kuwa nchi ikiingia katika machafuko hakuna atakayesalimika, awe mwanachama wa Chadema ama vyama vingine vya siasa, na mbaya zaidi kinamama na watoto ndio watakaoathirika zaidi.
  Hivi karibuni Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema na mwenzake wa UDP, John Cheyo walitoa tahadhari kuhusu mwenendo wa Chadema na baadaye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira alisema serikali ina ukomo wa kuvumilia mambo mbalimbali, hivyo isije kulaumiwa itakapoanza kuchukua hatua.
  Wassira alisema kauli za Chadema kutaka kutumia nguvu ya umma kuiondoa madarakani serikali iliyopo, haikubaliki na ni kinyume cha Katiba.
  Naye Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, naye amesema ofisi yake haitasita kukifutia usajili Chadema, iwapo kitaendelea na mwenendo wake, wa kuhamasisha vurugu nchini.
  Aidha, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, kimesema tangu viongozi wa Chadema uanze ziara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, umekuwa ukitoa kauli za kuupotosha umma na zenye kuchochea uasi na machafuko
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Huyo Shekh ametoa lini hii habari mkuu?
   
 3. K

  Kiwembe Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana jipya ndo maana 2nasema kama chadema ni chama cha wachaga bac ccm ni chama cha waislam
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  nenda kwenye web ya uhuru publication utaikuta kama leading story...
   
 5. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mbona ni outdated news hii?
   
 6. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  hii lazima itakuwa ni article ya magazeti aina ya uhuru, jambo leo au mtanzania
   
 7. K

  Kiwembe Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida yao mbona wao hawana habari zenye kuleta sense kwa mainterellectual
   
 8. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  Kama Sheikh ameishia darasa la pili, unategemea ataongea vitu vyenye logic kweli.
   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  habari ni kwamba CCM ni cha Waislam, CDM ni cha Wacchaga /wakristo
   
 10. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  huyo sheikh anajua hata kuandika?
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani kama hii habari imetolewa zamani kuna sababu gani ya mtu kuiweka hapa JF leo kama huyu mtu hana mawazo sawa na huyo Sheikh?.. why today iwekwe ktk magazeti na hapa JF!..Kuna maandamano gani ya Chadema yanazungumzia kurudi Mbeya? Jamani mwee, na ili iweje kama huu sio Udini tunaokemea kila siku na wanaoufanya ni nyie wapenzi wa Chadema..I mean sielewi kabisa wanaChadema mnapokuja na vitu kama hivi huwa mnalenga kutuma ujumbe gani?
   
 12. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa kama Rais wa nchi ambaye ni mwislam anaamini hivyo na anakili kwa kusema hayohayo itakuwaje kwa viongozi wake wa dini. Naona hili usimtwishe Tendwa ila mwachie mzee wa kaya mwenyewe.

  Mzee wa kaya alilianzisha na alimalize mwenyewe. Tofasuti na hapo linammaliza yeye maana atasimama mahakamani ili kujibu tuhuma hizi baada ya utawala wake.
   
 13. A

  ADVOCATE NEWBOL Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nashangaa, na ninaamini na watu wengine wote ambao si wajinga wanashangaa, kuwa serikali inaachia (kwa sababu za kijinga kuwa CHADEMA wakipandikizwa kuwa ni wadini basi CCM watapeta) chuki kupandikizwa katika jamii. Ujinga tu. Baadaye tutakapochinjama, wajinga wanaotuongoza watasema ni CHADEMA hao wakati ni wao wanaoacha ujinga uhubiriwe. Kama kuna chama cha kidini, jinai hiyo na basi kifungwe. Wajinga hawa wanajua kuwa hakuna chama kama hicho, ila ni mbinu za kisiasa. Upuuuuuuuuuuuuuuuzi mtupu.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kumbuka Mbowe alipokuwa Tunduru alisoma barua iliyosambazwa na mashushushu kuwa Chadema ni Chama za kidini, na alionyesha hadharani barua hiyo, ambayo ilisambazwa mikoa ya kusini yalikofanyika maandamano ya Chadema. Aliyosema huyo shehe ndiyo yaliyojilia.
   
 15. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sijui ni habari hii imetolewa lini kwa uhakika, LAKINI si muda mrefu kama unavyosema kwani gazeti ya AN-NUUR la wiki ilopita limetoa hitimisho la mkutano wa waislam wanaosoma vyuo vya elimu ya juu mkoani mbeya na tamko lao. Mkutano huo kama sijakosea umeisha alhamisi au weekend. kwa hivyo huyo shekh kahutubia baada ya huo mkutano.
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Education is key.
   
 17. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Elimu ya mesheikh inatia wasiwasi!!! i think most of them are not critical thinkers but all in all "A DRAWN MAN CAN CATCH A STRAW"
   
 18. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu,
  Huyo Sheikh alitoa hayo Ijumaa ipi? Mwaka gani? Leo ni jumatatu, ina maana vyombo vingine vya habari vimeshindwa kupata maelezo ya huyo sheikh kama yalitokea wiki jana?
  Inawezekana haya yakawa maoni yako.


  Hii santuri mbona ni moja wapo ya zilipendwa na haikununulika?
   
Loading...