Tendwa: Sitashangaa siku wapinzani wakichukua nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa: Sitashangaa siku wapinzani wakichukua nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 25, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amesema hatashangaa siku moja vyama vya upinzani vikishinda uchaguzi na kushika madaraka.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma kuhusu maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, Tendwa alisema "kushika dola ndilo lengo la kila chama cha siasa".

  Alisema yeye akiwa mlezi wa vyama vya saisa nchini angefurahi kuona vyama hivyo vinakua na kutimiza lengo la kutwaa dola au nafasi za uongozi katika mamlaka mbalimbali za nchi.

  "Hili haliwezi kuwa ni jambo la kushangaza, sheria iko wazi kabisa kwamba lengo la kila chama cha siasa ni kushika dola au kuongoza mamlaka nyingine za kiserikali kwa mujibu wa sheria za nchi, na mimi nikiwa mlezi wa vyama vya siasa kama mlivyosema ningefurahi wapambane washinde ili wasifanye fujo,"alisema Tendwa.

  Kuhusu miaka 20 ya demokrasia ya vyama vingi nchini, Msajili huyo wa Vyama vya Siasa alisema maadhimisho hayo yataanza Julai 1, mwaka huu na kwamba yatatumika kufanya tathmini ya zama na matukio mbalimbali yaliyotokea katika kipindi hicho pia mchango wa vyama vingi katika demokrasia ya nchi.

  Tendwa alisema katika uzoefu wake akiwa msajili wa vyama vya siasa amebaini kuwapo kwa umuhimu wa sheria ya vyama kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuongeza tija ya uwapo wa ofisi yake na vyama hivyo kwa ujumla wake.

  Alisema katika mchakato wa uandishi wa Katiba Mpya, watapendekeza Msajili wa Vyama vya Siasa na naibu wake baada ya kuteuliwa waidhinishwe na mamlaka nyingine kama Bunge ili kuwapa nguvu ya kiutendaji na uwajibikaji.

  "Hili litaondoa lawama za mara anafanya hili au lile ili kumridhisha fulani kwani aliteuliwa na Fulani, kwahiyo sisi tunadhani mtu akiidhinishwa na chombo kingine basi anakuwa na uhuru wa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa ufanisi zaidi," alisema.

  Kuhusu vyama vya siasa, Tendwa alisema lazima uwapo utaratibu wa vyama visivyo na tija ‘kushuka daraja' kila baada ya uchaguzi kufanyika na kwamba hatua hiyo itavilazimisha vyama vyete kufanya shughuli za kisiasa.


  CHANZO: Tendwa: Sitashangaa siku wapinzani wakichukua nchi
   
 2. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Amesoma alama za nyakati, he is GT
   
 3. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mie nitashangaa wasiposhika dola. Pia nitashangaa wakishika dola.
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ipo siku hata JK atakubali kuwa nchi itaweza kwenda upinzani muda wowote atabakia Nape tu maana anaogopa hata kivuli chake!!Membe,Tendwa wanajua nini kinafuata!Tendwa ameonyesha kuwa baadhi maamuzi yake yanawabeba waliomteua hana jinsi!!anaomba katiba ione hilo!!
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  For what? Utashangaa? any reason? mpayukaji
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maana wapinzani wanaachia mianya ambayo ingewawezesha kuchukua nchi hata kupitia Tahrir.
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Vipi kuhusu wale washili wa Arumeru bado hawaja muua lema?
   
 8. T

  Tewe JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Ukiijua kweli itakuweka huru
   
 9. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,092
  Likes Received: 11,230
  Trophy Points: 280
  indirectilly anasema M4C itatinga magogoni 2015.
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hii habari ina mapungufu ya kiuchapishaji, au kihariri. Imeeleweka anyway
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni uhuru mr T
   
 12. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Msema kweli mpenzi wa Mungu.
   
 13. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Kasoma upepo nae sasa anajifanya mtabiri kama shekh yahya!ilo lipo peupe hata akiwasaidia vp magamba chadema imeshabeba nchi.
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu mzee bana ananifurahishaga sana...atakanusha tu hii kauli nyie subirini muone
   
 15. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwani c walishashinda kwa nguvu yake akageuza matokeo na kuipa ccm ushindi?
   
 16. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  JF
  kama Tendwa atashikilia uzi wake huu kuwa chama kisicho kuwa na wabunge & madiwani kishushwe daraja baada ya uchaguzi. kwa sasa ni vyama gani vingeshuka daraja ?????
   
 17. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Kwa wapenda demockrasia hili ni suala ambalo liko wazi ndiyo maana waanzisha vyama. Hata vile vyama ambavyo havijapata uwakilishi hata wa udiwani au ubunge bado vinaamini siku moja vitaongoza nchi.

  Kukaa na kuamini kuwa magamba hawatakaa wakatolewa madarakni ni siasa za njozi na ni kinyume na demockrasia. Lakini cha ziadi dalili za mabadiliko ya utawala zinaonekana wazi hata kama siyo leo kesho inawezekana. Tufunguke na tukubali mabadiliko katika fikra zetu.

  Tatizo kubwa kwa Tanzania watu wengine hawana pa kukimbilia pindi chama fulani kitakapoondolewa madarakani kwa kuwa akili na maisha yao wameweka kwenye siasa za chama kimoja, mfumo ambao umepitwa na wakati.
   
 18. Papaeliopaulos

  Papaeliopaulos Senior Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu aliyetangaza yale matokeo sio huyu. yule anaitwa Judge Lewis Makame (Mwenyekiti mstaafu wa tume ya uchaguzi)

  Hata hivyo heri yeye ameweza kusoma alama za nyakati
   
 19. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,576
  Likes Received: 4,690
  Trophy Points: 280
  Ngoja yule Mheshimiwa toka Gombe amsikie.
   
Loading...