Tendwa na Makame watofautiana JK kuhutubia usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa na Makame watofautiana JK kuhutubia usiku

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Facts1, Sep 21, 2010.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa, ametetea hatua ya mgombea wa kiti cha Urais kupitia tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete, kuhusu kufanya mikutano ya kampeni zaidi ya saa 12 jioni na kueleza kuwa kuanzia sasa wamekubaliana mwisho wa kampeni ni saa moja usiku.

  "Ni kweli kwamba muda wa mwisho wa kampeni huko nyumba ulikuwa ni saa 12 jioni, lakini muda huo ulikuwa na tofauti sana katika kumaliza mikutano katika baadhi ya maeneo kama ya Mkoa wa Kigoma na kule Ngara ambako saa 12 jioni, bado ni mapema sana,"alisema Tendwa.

  Tendwa alisema kwa msingi huo, si makosa sasa kwa mgombea wa CCM, (Kikwete) kuhutubia zaidi ya saa 12 kama ambavyo imetokea katika mikutano yake ya hivi karibuni mkoani Arusha na Manyara.

  Hata hivyo alipoulizwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (Nec) Jaji Lewis Makame alisema, tume haijapata taarifa hizo na kuwa bado wanaamini kuwa muda wa mwisho wa kampeni ni saa 12 jioni.

  "Ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako taarifa hizo, kwani kayasemea wapi hayo," alihoji Jaji Makame.

  Alisema Nec itafuatilia taarifa hizo na kwamba ikithibitisha, itatoa tamko lake.

  My take: Tanzania ni ya ajabu kweli sheria zinapindishwa kum-fit mtu na si mtu ku-fit sheria kwa hali hii hatufiki tunakotarajia.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  This is absolutely a big joke!
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  This is what I said early july. We need ''level field'' to have fair and free election.
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Tendwa bado anaangalia majira kwa kufuata Jua badala ya saa! Kwani ratiba katengeneza nani mpaka aulizwe Tendwa badala ya NEC? Jamani waandishi wa habari muwaulize wahusika katika jambo linalowahusu! Lakini JK akizidisha muda ajue ndivyo anavyodhoofisha afya yake 'kwa kasi zaidi, ari zaidi, nguvu zaidi'!
   
 5. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Sheria ni msumeno. Kama inasema saa 12 ni saa 12 hata kama jua bado lipo. Yaani Tendwa anataka kusema saa 12 Arusha sio saa 12 kwa vile bado jua linakuwa lipo Kigoma? What a joke!
   
 6. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Huu ni upumbavu, kwani wakati wanaamua kuwa mwisho wa kampeni iwe saa 12 jioni Kigoma na Ngara hazikuwepo? hawakuliona hilo? kwanini Jk avunje kwanza sheria ndiyo wewe tendwa ujustify makosa yake? kama hivyo ndivyo kwani Arusha na Manyara ni Kigoma na Ngara siku hizi? Tendwa Tendwa be careful, this time hatudanganyiki
   
 7. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Well sikujua kuwa Tanzania kuna two different time zones, lol. Mwaka huu kweli tutaona nani kasoma na kuelimika na nani kasoma tu. Tendwa-- stop it!! Unatia aibu, you better keep quite tu, lol Next time utasema kule Rukwa kwa kuwa kuku bado hawajaingia ndani basi wagombea waendelee kuhutubia kampeni, what a hek!!!
   
 8. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu Tendwa anatia aibu yaani hapo amejiidhihirishia kuwa yeye ni CCM damu, anashindwa kuzuia hisia zake. Wanajamii hebu geuzeni hili upande wapili ingekuwa ni mgombea yeyote wa chama cha upinzani amefanya hivyo amezidisha muda ungesikia kelele zake angeonga hadi mapovu yamtoke mdomoni.

  Ikiwa JK kafanya kosa aadhibiwe kufuatana na kosa kama muda ulipangwa ni Saa 12 jioni kwa Tanzania nzima basi ufuatwe hakuna cha kuangalia majira ya joto wala baridi, wakati wamekaa na kupanga muda walijua kuwa KIGOMA iko kwenye Longitude na Atitude nyingine ama hawakusoma jeografia????

  Jaji Lewis naomba ufanya kazi yako ipasavyo usiangalie sura wala rangi sheria iliwekwa kwa wote bila kubagua itikadi, usimsikilize huyo Tendwa kwani hajui alitendalo.

  NB: NAONA SASA KUNA HAJA YA KUTEUWA TUME HURU YA UCHAGUZI NA MSAJILI HURU WA VYAMA VYA UCHAGUZI MAANA HAWA WALIOPO HAWAFAI KWA MANUFAA YA NCHI
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kweli bado tuna safari ndefu!
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi nikiangalia photoz za Tendwa swali linajiunda ndani yangu kuhusu AKILI ZAKE inawezekana anaugua MNYONG'ONYO huyu. very unfit kichwani
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Well said huyu jamaa niwa ajabu kweli inaonekana bado yuko enzi za mawe majira yake yanategemea mwanga wa jua na sio saa itakuwaje siku hiyo kama kuna mawingu akiona giza tu atasema ni saa moja usiku hata kama saa inaonyesha saa 12, basi sheria isingetamka muda wa saa ingesema inategemea na mwanga wa sehemu husika
   
 12. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Sasa kaka JK alizidisha muda hadi saa 1 akiwa Ausha, akifika Ngara si atafikisha saa 3 usiku!
   
 13. M

  Mutu JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  This is unfair inaonekana sheria wametungiwa wapinzani,inabidi kuandamana,au wanasheria wa chadema kufuatilia hili
   
 14. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Tendwa anagalia sana. Mara Jk alikuwa anatania, leo majira hutofautiana
   
 15. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wadanganyika watu wa ajabu sana.

  Si Makame wala Twenda aliye-nukuu kufungu cha sheria au kanuni ili tu-rejee...
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo wao walipoulizwa swali, walitumia nini kama reference ya majibu yao?

  Why Tendwa had to go all the way kueleza kwamba saa 12 jioni jua linakuwa bado halijazama. Alipotaja saa 12 jioni jua linakuwa halijachwea alikuwa ana-refer nini? Kwanini hakutaja saa 1 jioni na akataja saa 12 jioni?

  Tatizo lenu watetezi wa madudu ya CCM, mkiona watu wanashuka na vifungu mnaanza kuhamisha magoli.
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  MHE JAJI TENDWA ANAPOZWA NA NYUMBA YA SERIKALI ALIYOMILIKISHWA KULE OYSTERBAY. MPAKA SASA NISHACHANGANYIKIWA NI NANI MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA MWAKA 2010, JE NI TUME YA UCHAGUZI (nec) AU NI MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA. HAYA NDIO MATAYARISHO YA WIZI WA KURA!!!!!!
   
 18. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa jibu la Tendwa, wakati wanaweka utaratibu kampeni ziishe saa 12 walifikiri Kigoma iko DRC?
   
 19. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Huyu Tendwa anatutia wengine kichefuchefu, hivi huo upara kumbe hauna kitu. Kwetu sisi watu wenye upara huwa tunaamini wana akili, lakini huyu ni tofauti kabisa. Duh, yaani mpaka saa hivi nina wasiwasi na usimamizi wa kura tutakazompa Dr wa ukweli.

  Hivi Kigoma ina majira tofauti na mikoa mingine? Aihamishie DRC basi kama vipi.

  Jamani, mi Kikwete akirudi madarakani kwa kuiba kura zetu, ntaingia msituni tu, hakuna lingine hapa.
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Labda Tanzania inahitaji time zones mbili.
   
Loading...