Tendwa kama Usajili umekushinda, Achia Ngazi!

Ila kweli Tanzania hii kuna watu wanajiamini na kujiona waungu watu, la Tendwa la kusema akipata hela ataenda kuhakiki wanachama wa CCJ mikoani, mi limenikera, najiuliza ni kweli hawana helaaaa? au ndo mizengwe tu ili chama hiki kinachoogopwa na CCM kisisajiliwe? Halafu ndugu yangu Tendwa kitu serious unaongea kwa nyodoooo, hivi nani anakupa kujiamini kihivyo? Hao CCM wanaokulinda ipo siku yao watatoka madarakani na wewe utakuwa kenge tu mtaani.

Kama anasema rais alitania kusema takrima haikwepeki, tutegemee nini?
 
Atageuka na kuwaambia alikuwa anatania kama Rais wake na kitochi cha mbege!


kwahiyo umma wa Watanzania ni kabila moja kubwa sana ambalo hawa jamaa ni watani zetu! Aiseeeeeeee we acha tu!:angry:

Kweli waweza tania unapohutubia taifa? yaani inakuwa kama uko kijiweni unapata gahawa!
 
kama hoja ndio zile alizozisema basi kwa kweli anastahili kujiuzulu...Amekiuka maadili ya kazi yake.
 
Tendwa aseme ni kiasi gani cha kuwapeleka maofisa wake mikoani wakahakiki ili bakuli litembee aone zitakavyochangwa kama umeme hizo fedha anazodai ofisi yake haina. CCM hao wanaogopa hata vivuli sasa! Kumbe CCJ inatisha!!!!
 
Kuna comment imetolewa na one of our learned friends....." tendwa is not the Registrar of Parties, he is the CCM Enforcer....I cannot believe this guy....atleast although tunajua kuwa wewe ni puppet wa Chama, show us that you are neutral....kweli sijui kama tutafika.....Asante Mzee Mwanakijiji kwa kutuelimisha..
 
Kama anasema rais alitania kusema takrima haikwepeki, tutegemee nini?

Huyu mzee hawezi kupumzika kwa amani hivi sixty haijafika akastaafu kwa mujibu wa sheria? Nashindwa kuchangia hoja maana naona uwezo wake umefika kikomo. All in all core activities za ofisi yake hazijui na hana budget yake! Hili ni tatizo.
 
Aliwapa usajili wa muda, wa kudumu hatashindwa. Alijibu kiofisi vizuri tu au mnataka aisajili CCJ kwa hati ya dharula?
 
madara ya viongozi Tanzania hayahojiwi.......

tendwa anaposema hana bajeti ya kwenda mikoani anamaanisha nini? kuwa CCJ ikimpatia fedha ataenda? au lazima bajeti hiyo itoke serikalini? na kama serikali itasema hatuna pesa mpaka mwaka mpya wa fedha, meaning vyama havitasajiliwa hadi wakati huo?
 
Angesema mtu Kiongozi mwingine wa kiasiasa ungemuuona Tendwa kaitisha wnahabari na anakemea JK kasema waziwazi kinyume cha Hukumu ya Mahakama kuu anasema alikuwa anatania.

Kiongozi gani wa nchi anaweza akatania jambo ambalo liliamuliwa na mahakama kuu? Kkama walivyozoea kujifanya wako juu ya Mahakama ndivyo wanajisahau wanajikuta wamejitumbukiza kwenye malumbano na wananchi Tendwa mchumia tumbo tuu hatufai kabisa kwenye nafasi hiyo
 
Fedha walizopewa bajeti iliyopita wamezifanyia nini?

Maana hakuna chama cha siasa kimesajiliwa currently,pesa za kufanya semina za sheria za uchguzi wametoa wapi...!

Kimsingi CCM inaogopa CCJ, thats y inatumia kila mbinu ku make sure that CCJ haishiriki uchaguzi mwaka huu,....

Me nimechoshwa na nchi hii na hivi sasa nahangika mahitaj yangu na na familia yangu tu...
 
Lakini fikiria kwa upande mwingine; labda anatusaidia kwa sababu anawafanya watu wafuatilie zaidi na kuwa na hamasa zaidi na CCJ; you know people always (or most of the times) root for the underdog..
 
Unatumaini? Mbona unaongea katika nafsi ya tatu kana kwamba hakika ("absolutely") wewe si mwanachama mwanzilishi/muasisi wa Sisi Je? Vipi tena?

Aaah na wewe uko mgumu sana kuelewa saa ingine. I really don't know how you got by in school?
 
Hii nchi ina hela ya kufanya kila jambo, hata la kipumbavu lakini sio la usajili wa chama kipya? Hii kali! Tena nimeisikia kwa mara ya kwanza. Laiti kama kila kitu kingesemwa hivyo tungekuwa mbali sana
 
Halafu bado una deni kule kwa Wabafokeng....ulisema unaenda kufanya utafiti....umeishia/ umefikia wapi?

Utafiti wa kisayansi haufanyiki kwa siku moja weye. Inabidi nifunge safari kwenda huko Bafokeng! Prisisheni ni muhimu sana, au?
 
hawa watu wamelewa madaraka mfano wake hakuna! Natumaini CCJ itatoa tamko leo kuwajibu hawa na kuwa fundisho kwao.

Sasa hivi naanza kupata sababu za kumtuma huyu bwana hapa chini kutabiri kuwa mwaka huu hakuna uchaguzi. Upepo hauwaendei vyema kabisa CCM, na sasa wanatafuta sababu za kudelay election
1. Kama CCJ ikienda mahakamani kudai haki, ambayo kwa vyovyote lazima ipatikani maana kila kitu kipo wazi basi watatoa amri pia kuiagiza mahakama itoe "Amri ya kusitisha uchaguzi mpaka pending litigations zitakapokuwa resolved" ili kukipatia haki CCJ

2. Kama siyo CCJ basi watatumia issue ya "Mgombea binafsi".

Unajua nimekuwa nikijiuliza kwa nini Serikali ya CCM inaogopa sana CCJ na kuwepo mgombea binafsi? - Huenda jibu likawa kuzuia wabunge wapiganaji wa CCM ambao wameisha kusanya nguvu za kampeni kuingia ama CCJ ama kugombea kama independent pindi kundi la CC litakapokaa na kuamua nani apewe ubunge na nani anyimwe kulingana na masilahi yao.


sheikh-yahyabc.jpg


Huenda huyu bwana alitumwa kutoa hoja kutuhadaa kisaikolojia
 
Nilimsikiliza kwa makini sana Mh.John Tendwa Msajili wa vyama vya siasa alipokuwa anatoa ufafanuzi kuhusu kuwapa au kutokuwapa usajili wa kudumu hawa ndugu zetu wa CCJ.

Tendwa anadai hana pesa ya kuhakiki majina ya wanachama wa CCJ nchi nzima. Swali letu hapa ni je Kama huna pesa hilo ni shauri la nani? kwa nini hilo liwe na shauri la chama? Kama huna pesa toa usajili hivyohivyo. Jambo lingine kwani Ofisi hii haina wawakilishi mikoani?

Tendwa acha mbwembwe toa usajili.
 
Back
Top Bottom