Tendwa kama Usajili umekushinda, Achia Ngazi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa kama Usajili umekushinda, Achia Ngazi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 18, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nina ushauri wa bure kwa Bw. Tendwa; abadili jina la ofisi yake kuwa la Mwendesha Semina za Kisiasa nchini kwani kama hana bajeti ya kufanya shughuli za ofisi zake yaani Usajili wa Vyama vya Siasa ambalo ni jukumu lake la kwanza na la msingi. Kama kweli hana fedha za kufanya kazi ya ofisi yake aifunge kwani utakuwaje msajili wa vyama vya siasa kama huna fedha za kusajili vya vya siasa?

  Lakini, hatuna budi kujiuliza lini aligundua kuwa hana hizo fedha? Maana Machi 1 alipowapa CCJ usajili wa muda alitegemea kuwa wangeshindwa kupata wanachama hadi miezi mitatu ipite na hivyo usajili wao ungejifuta automatically lakini ameshangazwa ndani ya siku 70 tu CCJ imepata wanachama zaidi elfu ishirini?

  Tangu mwanzo inaonekana Tendwa amechukizwa kabisa na ujio wa CCJ na kama nilivyoonesha pale pengine Marmo ambaye amekuwa mpinzani wa demokrasia nchini na anataka kutumia nafasi yake ofisi ya waziri Mkuu kukwamisha shughuli za CCJ. HIvi ni lazima CCJ isipate usajili wa kudumu licha ya kutimisha masharti yote.

  Sheria ya Vyama vya siasa ya 1992 inasema Msajili ni lazima akipe "KILA" chama cha siasa kilichotimiza masharti usajili wa kudumu. Labda kutokana na kutingwa ulikotingwa umesahau sheria inasemaje. Nimejitolea kukusaidia tu:
  (Ibara 8-5)

  Sheria haisemi ati msajili akikosa fedha za kufanya uhakiki basi asitoe usajili wa kudumu! Kwanza labda nimesoma haraka haraka sheria yenyewe (labda kwenye taratibu) haisemi moja kwa moja kwamba ni lazima Msajili atume watu mikoani kuthibitisha uwepo wa wanachama. Na zaidi ni upuuzi kudai kuwa kama akikuta mwanachama ambaye amekufa kwenye hiyo orodha basi atakifuta chama hicho. Nani kamuambia kuwa wanachama wakishajiandikisha wanatakiwa kusubiri wasife hadi wahakikiwe!? Ni kwa sababu hiyo, CCJ imeenda zaidi ya watu 200 tu. Atafute sababu nyingine ya kunyima usajili wa kudumu, lakini ziwe sababu zenye kuvuta akili basi!

  Tendwa wape CCJ usajili wa kudumu kama hutaki kwa sababu ya chuki ulizozionesha toka mwanzo achia ngazi umpishe Mtanzania mwingine kufanya kazi hii kwa uadilifu. Taifa haliwezi tena kuwavumilia watendaji wanaofikiri wao ndio zawadi ya Mungu kwa Taifa. Sababu alizozitoa za kwanini hawezi kufanya uhakiki zinaonesha kuwa Bw. Tendwa ameingia kwenye mkumbo wa viongozi walionogewa na madaraka na ambaye anataka aanze kuimbiwa imbiwa nyimbo za pongezi na kubembelezwa.

  Watu kama hawa ndio CCJ itahakikisha wanaondolewa kwenye utumishi wa umma mara moja kwani ni kikwazo cha utawala wa sheria na demokrasia. Kwanini mnataka kuwalazimisha Watanzania wajiunge na vyama ambavyo hawavitaki au kuviunga mkono kwa sababu ya woga wenu nyinyi? NI kitu gani kinawatisha kwa chama ambacho hakina majina makubwa (licha ya juhudi zenu za kutangaza vinginevyo)? Kwanini toka mwanzo mnatetemeshwa na wazo la CCJ kuweza kushiriki uchaguzi mkuu?

  Wapeni wananchi nafasi ya kuamua kwenye sanduku la kura na msitumie madaraka yenu kuwa kama baba na mama wa watanzania ati kuchagua ni chama kipi kinafaa kuwepo na kipi hakifai. Siyo jukumu la CCJ kuimarisha upinzani kama vile siyo jukumu la CCJ kuhakikisha wabunge wote wa CCM wanachaguliwa tena. CCJ itakuja na itikadi yake na sera zake na ni wananchi ndio wataamua hivyo.

  Toeni usajili wa kudumu mara moja ili CCJ ikamilishe uongozi wake wa kudumu wa taifa na kumalizia uandishi wa sera zake ambazo zitakuwa ni za kisasa na halisia zaidi zenye lengo la kurudisha serikali ya Watanzania mikononi mwa wananchi.

  Kama kweli hamna fedha, tangazeni ni kiasi gani kinahitaji kuwapeleka hao wahakiki wenu mikoa kumi na CCJ itawakopesha fedha kwa riba ili kukamilisha usajili huo wa kudumu.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kama sheria inasema "shall" msajili usjivutevute toa cheti haraka, suala la hela sio sababu iliyowekwa kwenye sheria, sheria ya vyama haisemi kama kama hana hela ni moja kati ya vitu vya kuzingatia wakati wa kutoa usajili. Usitake kupelekwa mahakamani bila sababu za msingi.

  Core objective ya ofisi yako ni kusajili vyama mambo ya sheria mpya achana nayo, kwanza haikuwekewa bajeti na bunge kwani imekuja baada ya kikao cha bajecti cha mwaka jana hivyo hela ulionayo ilipitishwa na bunge kwa ajili ya usajili kama ambavyo ofifi yako ilivyoanzishwa. Au unataka kutuambia kuwa bunge lilipitisha matumizi ya sheria mpya kabla ya kutunga sheria yenyewe?
   
 3. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ila kweli Tanzania hii kuna watu wanajiamini na kujiona waungu watu, la Tendwa la kusema akipata hela ataenda kuhakiki wanachama wa CCJ mikoani, mi limenikera, najiuliza ni kweli hawana helaaaa? au ndo mizengwe tu ili chama hiki kinachoogopwa na CCM kisisajiliwe? Halafu ndugu yangu Tendwa kitu serious unaongea kwa nyodoooo, hivi nani anakupa kujiamini kihivyo? Hao CCM wanaokulinda ipo siku yao watatoka madarakani na wewe utakuwa kenge tu mtaani.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Halafu aliniudhi kweli ati anawaambioa maimamu na maaskofu wahubiri kunywa majukwaa ya dini mambo ya sheria mpya. Akawa anazungumza kama Nabii Tito!
   
 5. E

  Edmund Senior Member

  #5
  May 18, 2010
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  M.M Mwanakijiji kumbe unamawzo kama yangu, jana kwenye taarifa ya habari ya usiku nilimsikia mwenyewe kwa masikio yangu Mr. Tendwa akidai eti fedha za kufanyia Uchunguzi, Uhakiki wa uhalali wa wanachama waliooredheshwa HAKUNA,

  MASWALI MUHIMU
  1. Ni nani anayepanga BAJETI ya Taasisi yake (tuachane na ile ya VITAFUNIO)
  2. Ni nani anayepanga Majukumu na Kazi za Taasisi hiyo
  3. Ni nani Mtekelezaji wa kazi hizo
  4. Elimu na Uzoefu wa huyu bwana ni upi?

  NIONAVYO MIMI
  Ile hali ya hawa tunaowaita viongozi wetu wa Nchi hii kutoa majibu ya Karaha, Kebehi, Zimamoto, Kipuuzi,Yanayotia hasira, Dharau na yanayoleta CHUKI itaisha lini.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hawa watu wamelewa madaraka mfano wake hakuna! Natumaini CCJ itatoa tamko leo kuwajibu hawa na kuwa fundisho kwao.
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Pesa amepeleka wapi?

  Hii ni idara ya serikali, na kila idara ya serikali hupeleka bageti ya pesa za matumizi hazina ili kupewa fungu la fedha, kumbuka ni muda mrefu hakuna chama chochote cha kisiasa kilishaomba usajili wa chama, hivyo anapaswa kutueleza fungu hili la pesa za uhakiki amezipeleka wapi?

  Semina hupewa fungu lake, mafuta yana fungu lake.

  Tendwa tunataka utupe takwimu sahihi za pesa mlizo omba hazina, mlizotumia ni kiasi gani na bakaa ni kiasi gani.

  Taarifa zako ni nyepesi sana, kwani hujatumia senti tano ya bageti yako katika pesa ulizoomba na kupewa na hazina za kuhakiki vyama, kwani hakuna chama chochote cha kisiasa mwaka huu kilishaomba uhakiki isipokuwa CCJ.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  May 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Atageuka na kuwaambia alikuwa anatania kama Rais wake na kitochi cha mbege!
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Wafanye wafanyavyo ukweli ni kwamba wananchi wameshachoka na uongozi lala wa CCM - kitendo cha mweshimiwa huyu ni cha aibu sana na wala hakilingani na hadhi yake - eti hatuna pesa za kuhakiki majina mikoani - sasa mnafanya nini hapo ofisini kama hauna bajeti? pesa zilizopo ni za posho ya vikao na vitafunio?

  Mambo mengine yanachukiza kweli kweli - wape usajiri wa kudumu waende kwa wananchi wakaombe ridhaa ya kuongoza wakishinda sawa we unabana kitu gani Tendwa?
   
 10. d

  damn JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tendwa anatii maagizo na amri za mkubwa wake aliyemweka pale----the Presidency. Hiyo ofisi na tume ya uchaguzi inatakiwa kusimamiwa na viongozi wa dini. Hapo wengine ndiyo tunaweza kuwa na imani kidogo na serikali.
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Watoe tamko kali na kumpa siku saba akishindwa kusajili chama wampeleke mahakamani haraka sana. Msajili wa kwanza aliwabania DP wakapeleka mahakamani mahakama ya Rufaa ikasema msajili hana haki ya kukataa kusajili chama.
   
 12. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  jana alikuwa nanongea kwa nyodo ile mbaya

  nikajua moja kwa moja kuwa ccj hatupati usajiliwa kudumu.
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  jana alikuwa nanongea kwa nyodo ile mbaya

  nikajua moja kwa moja kuwa ccj hatupati usajiliwa kudumu.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu Msajili wa vyama nchini anaajiliwa na nani?
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa mawazo yangu sijui kama CCJ itasajiriwa mana hapa makada wote wa CCM akiwemo chiligati alisema CCJ haiwezi kusajiliwa mana Tendwa BOSs wake ni Presadaa JK.

  Ushauri wa bure: NGUVU YA UMMA NDO ITUMIKE KUSHINDIKIZA CCJ ISAJILIWE otherwise hapa Tendwa atapiga kiswahili mpaka mwisho
   
 16. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Huenda umeshau kuwa huyu ni Nabii Tendwa kwani alitabiri kuwa ccj haiwezi kukamilisha usaili kabla ya uchaguzi na pia ccj ni "ghost", mwenye uwezo wa kuona ya mbeleni kiasi hiki sio nabii kweli?

  Hapa pamoja na kufikiria kwenda mahakamani lakini shinikizo la nguvu linatakiwa ikiwa ni pamoja na maandamano ya kidai haki hiyo inayotaka kupokonywa kiyemela kwa manufaa ya ccm. Lazima iwepo mipango thabiti ya kupunguza madaraka ya rais yanayomfanya kuwa kama mungu na kujizungshia yale ayapendayo. Hili wala sio shikizo la ccm, ila ni la JK
   
 17. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  hiyo kwenye red mi umenigusa mkuu kwani hiyo seksheni haiitaji watu wasio waaminifu inatakiwa imani ya ukweli toka moyoni ili uatendee watu haki mi kwa mtazamo wa kawaida naona hiyo ofisi ni sawa tu na tawi la sisiem.
   
 18. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Tendwa anataka kutuambia kuwa kama vingejitokeza vyama kama vitano hivi vinavyohitaji usajili wa kudumu kati ya bajeti ya 2009/10, na ambavyo vyote vimetimiza masharti ya kusajiliwa kisheria asingevisajili? Kwani gharama ya kuhakiki chama kimoja ni kiasi gani?

  Je, ina maana kwamba Tendwa hakuomba fungu la kufanikisha kazi yake (kusajili vyama vya siasa) kwa kuwa alishapewa maelekezo kuwa hakuna chama chochote kimpya ambacho kingeruhusiwa kusajiliwa?

  Maswali ni mengi kuliko majibu! Tendwa kazi yako hasa ni nini? Ukiweza kulijibu vema hilo, jibu na hili tena, wewe nawe ni msemaji wa rais?
   
 19. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi naisubiri hiyo siku wafadhili watakapoikatia Tanzania misaada kwa kuua DEMOKRASIA si mnaona wenyewe:

  Ilianza Rais''' eti hata msiponipigia kura kuna watanzania wengi watanipa!.......

  Ikafata daftari la kudumu la wapiga kura eti waliojiandikisha ni zaidi ya 21 milioni!!!!!!!!!!!

  Sasa Amekuja Tendwa....Eti hakuna pesa za kuhakiki wanachama wa CCJ Mikoani....

  HIVI WADAU NIULIZE ''' HAMUONI MPAKA HAPO KUWA KURA ZISHAIBWA!!!!!!!!!!!!!!!!

  Mimi nafikiri hata Masanduku ya kura kuna ambayo tayari yamehifadhiwa pahali yakiwa na kura ndani.....
  Jamani Mungu atunusuri sioni mema mbeleni ILA KWA KUOMBA NA KUFUNGA.......OH! .....MUNGU tuhurumie wanao Tanzania kabla haijaja ile siku mbaya.

  Siku ambapo:

  > Tutatauta kazi wala hatutaziona maana zitakuwa zimeshachukuliwa na wanajumuiya wa afrika mashariki kutoka nchi nyingi

  > Tutakuwa tukiongozwa na viongozi mafisadi tu kuanzia raisi mpaka mtendaji kata....

  > Siku ambayo nyumba ya mlala hoi itachimbuliwa na greda kupisha Fisadi anayetaka kujenda nyumba ya mia moja.

  > Siku ambayo shule zote za English Medium zitakuwa zimepigwa marufuku na kuamriwa kuwa za kata.

  > Siku ambayo Watoto wetu wote watakuwa wanasoma shule za kata huku wale wa vigogo na mafisadi wakisoma Ulaya na Amerika.

  > Siku ambayo ajira bila kingereza hazitakuwepo hata kama ni kazi ya kufagia barabara na wakati huo huo ukitilia maanani kuwa shule za Medium zitakuwa zimefungiwa na kubaki za kata ambazo zote kuanzia nasari hadi kidato cha sita zitafundisha kwa kiswahili.

  > Siku ambayo taasisi zetu zote za juu zitakuwa zimelazimishwa kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia..

  Naomba siku hiyo isije wakati wa Baridi maana Makoti na masweta yatakuwa yanauzwa kwa $ 500 wakati mwananchi wa chini atakua bado anaishi chini ya dola $1 kwa siku baada ya Ombi la TUCTA kuzuiwa
   
 20. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mtu akikushauri jambo la kipumbavu na ukalikubali atakudharau..Kama kweli ameshauriwa hivyo na Muungwana basi atakuwa anazeeka vibaya..

  Unajua huyu mzee nadhani atakuwa na matatizo ya akili,unakumbuka mwanzoni alisema CCJ ni Hoax..


  Mkuu FMES tunakuhitaji..sijakusikia wiki mbili hivi..salama Mkulu
   
Loading...