Tendwa: Iundwe katiba mpya kabla mambo kuharibika

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
MJADALA wa madai ya katiba mpya jana uliendelea kupamba moto wakati Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alipojitosa kwa kusema kuwa kkatiba mpya inatakiwa kabla mambo hayajaharibika na kupendekeza kuwepo kwa mkutano wa kitaifa wa kikatiba utakaojumuisha watu wa kada mbalimbali.

"Hata kama tuko katika taasisi za serikali, lazima tueleze ukweli. Mnaona wenyewe jinsi Bunge lilivyo na kigugumizi cha kuundwa kwa katiba mpya," alisema Tendwa.

Tendwa anakuwa kiongozi mwingine wa juu kuingia kwenye mjadala huo ambao ulifufuliwa baada ya Chadema kususia matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka huu na kuibuka na kilio cha katiba mpya, kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi na kuundwa kwa tume ya kuchunguza matokeo hayo ya uchaguzi wa rais.

Tayari mawaziri wawili wakuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Frederick Sumaye wameshaeleza umuhimu wa kuwa na katiba mpya ili kuondoa mapungufu mengi yaliyo kwenye katiba ya sasa iliyorekebishwa mwaka 1984.

Maoni ya watendaji hao wakuu wa zamani yanakwenda sambamba na orodha ndefu ya wanasheria nguli. Orodha hiyo inamjumuisha Jaji Mkuu Agustino Ramadhan, Jaji Robert Kisanga, Jaji Amir Manento, Jaji Mark Bomani, na mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Issa Shivji.

Jana Tendwa, ambaye pia ni mwanasheria, alisema kuwa katiba inatakiwa itokane na matakwa ya Watanzania wenyewe.

Mbali na kutoa angalizo hilo Tendwa alisema kuwa mchakato wa kuandaa katiba hiyo utokane na mkutano wa kikatiba ‘Constitutional Conference' ambao utajumuisha watu wa kada mbalimbali na kupanga jinsi ya kuandaa na kuandika katiba hiyo.

"Katiba ni kama moyo; hata sisi binadamu moyo ukiwa na tatizo ni lazima uende hospitali kwa ajili ya kupata tiba. Kwa hiyo hii katiba inayotumika sasa nayo ni lazima itazamwe upya," alisema Tendwa wakati akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) jana jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo uliowashirikisha viongozi na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa nchini ulikubaliana kuwa utatolewa muongozo utakaoeleza mapungufu ya katiba inayotumika sasa na aina ya katiba mpya inayotakiwa na Watanzania.

Pia walikubaliana kuitisha mkutano mkubwa utakaojumuisha asasi za kiraia, taasisi za dini, vyama vya wafanyakazi na wakulima pamoja na wananchi kwa ajili ya kujadili muongozo huo pamoja na kupeleka maazimio ya yaliyojadiliwa katika mkutano huo serikalini.

Tendwa, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa kuhusu suala zima la matatizo ya katiba ya sasa hasa inapofikia uchaguzi mkuu, alisema: "Kuna baadhi ya vyama nchini Kenya vilipinga sana suala la kuwa na katiba mpya... tusifikie wakati tukaona kuwa hakuna haja ya kuwa na katiba mpya... lazima tujadili kwanza ni katiba ya namna gani tunayoihitaji tena kwa kuwashirikisha wadau wote."

Tendwa alifafanua kuwa yuko tayari kuyafanyia kazi majumuisho yote ya mkutano huo huku akinukuu baadhi ya vifungu vilivyomo katika katiba hiyo ambavyo kwa namna moja au nyingine vimekuwa vikilalamikiwa kuwa havina maana yoyote.

"Katiba zetu kati ya 1961 na 1965 hazikuwa na haki za binadamu bali haki hizo ziliwekwa kama utangulizi, hatahivyo haki hizo ziliwekwa katika sheria namba 15 ya 1984 iliyorekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa mwaka 1977," alisema Tendwa.

Tendwa alitoa angalizo kwa kueleza kuwa historia inaonyesha kwamba chaguzi za Kenya na Uganda zilizingirwa na migogoro iliyoanzishwa na vyama vya siasa na matamshi ya waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa na kuongeza kuwa wakati mwingine ubaya wa chaguzi hizo ulisemekana kuwa ni katiba.

"Imeelezwa kuwa katiba za nchi hizi zimehusika katika kuzisimamia chaguzi hizi mbaya; hazionyeshi utawala bora na nyingi zina misingi ya tawala za chama kimoja," alisema Tendwa.

"Vile vile rais ana madaraka makubwa na mamlaka ya kuteua Tume ya Uchaguzi, tume ambayo husimamia mchakato wa uchaguzi mzima na hasa uhesabuji wa kura. Suala jingine ni rushwa katika uongozi wa kisiasa."

Tendwa alisema Tanzania kwa sasa ina miaka 49 tangu ipate uhuru, lakini akahoji katika kipindi hicho "watu wamebadilika kiasi gani? Haina ubishi kwamba demokrasia imekua katika kipindi hicho, lakini kwa misingi ipi?"

Msajili huyo aliweka bayana kuwa katiba ya sasa ya Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki bado ina misingi ya kikoloni.

Tendwa alikiri kwamba kumekuwepo na mabadiliko makubwa tangu uhuru akibainisha ujenzi wa shule, vyuo vikuu, mitandao ya afya na mifuko ya jamii, barabara na mawasiliano, kukua kwa kilimo na uzalishaji mazao bora.

Lakini akaongeza: "Hata hivyo mheshimiwa mwenyekiti, hatuwezi kujidanganya kwa hayo tuliyoyafikia na kwamba pengine tungepata maendeleo makubwa kama tungekuwa na katiba nzuri zaidi na yenye kuzingatia misingi ya kijiografia, jamii ya Watanzania, misingi bora na utashi wa kisiasa na rasilimali za nchi."

Msajili huyo aliisifu Kenya kuwa imeibuka na katiba yenye uasilia wa nchi hiyo baada ya mijadala kadhaa na hata mabadiliko ya tume au kamati ya rasimu ya katiba ya mara kwa mara.

Pia alisema katika nchi nyingine katiba zimeshutumiwa kwa kuwa na viraka vingi vinavyowekwa kila mwaka na ambavyo mara nyingi huungwa mkono na kupitishwa na chama chenye wabunge wengi ndani ya Bunge.

"Jambo kubwa linalolalamikiwa na , Mheshimiwa mwenyekiti, na wadau wengi ni mamlaka ya rais. "Niruhusu... niseme nukuu ya mwanafalsafa mmoja Sir William Blackstone ambaye kwa kuangalia mamlaka ya mfalme wa Uingereza mwaka 1765 alisema 'The King can do no wrong is a necessary and fundamental principle of the English Constitution(mfalme hawezi kufanya makosa ndio msingi mkuu wa katiba ya Uingereza)'. Ukibadili neno King na Rais... basi kwa hali hiyo utaona mantiki ya kilio cha wapinzani," alisema.

Awali makamu mwenyekiti wa TCD, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye pia ni mwenyekiti wa CUF, alisema kuwa katiba mpya inatakiwa itokane na mapendekezo ya wananchi, iwe ni misingi ya demokrasia, wananchi wawe na haki ya kuchagua na kuchaguliwa.

"Mbali na hilo rasilimali za nchi zinatakiwa kutumika kwa manufaa ya wananchi. Mpaka sasa katiba yetu tayari ina vikara 15 hivyo ni vyema ukaandaliwa mchakato mzito kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi suala hili la katiba," alisema Lipumba.

Katika mkutano huo Mkurugenzi wa utetezi na maboresho ya sheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alisema kuwa katiba ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 zinakinzana kwa kuwa makamu wa kwanza na wa pili wa rais wa Zanzibar hawatambuliki katika katiba ya mwaka 1977.
CHANZO: Gazeti la Mwananchi la leo
 
Fidelis Butahe na Vicky Kombe

MJADALA wa madai ya katiba mpya jana uliendelea kupamba moto wakati Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alipojitosa kwa kusema kuwa kkatiba mpya inatakiwa kabla mambo hayajaharibika na kupendekeza kuwepo kwa mkutano wa kitaifa wa kikatiba utakaojumuisha watu wa kada mbalimbali.

“Hata kama tuko katika taasisi za serikali, lazima tueleze ukweli. Mnaona wenyewe jinsi Bunge lilivyo na kigugumizi cha kuundwa kwa katiba mpya,” alisema Tendwa.

Tendwa anakuwa kiongozi mwingine wa juu kuingia kwenye mjadala huo ambao ulifufuliwa baada ya Chadema kususia matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka huu na kuibuka na kilio cha katiba mpya, kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi na kuundwa kwa tume ya kuchunguza matokeo hayo ya uchaguzi wa rais.

Tayari mawaziri wawili wakuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Frederick Sumaye wameshaeleza umuhimu wa kuwa na katiba mpya ili kuondoa mapungufu mengi yaliyo kwenye katiba ya sasa iliyorekebishwa mwaka 1984.

Maoni ya watendaji hao wakuu wa zamani yanakwenda sambamba na orodha ndefu ya wanasheria nguli. Orodha hiyo inamjumuisha Jaji Mkuu Agustino Ramadhan, Jaji Robert Kisanga, Jaji Amir Manento, Jaji Mark Bomani, na mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Issa Shivji.

Jana Tendwa, ambaye pia ni mwanasheria, alisema kuwa katiba inatakiwa itokane na matakwa ya Watanzania wenyewe.

Mbali na kutoa angalizo hilo Tendwa alisema kuwa mchakato wa kuandaa katiba hiyo utokane na mkutano wa kikatiba ‘Constitutional Conference’ ambao utajumuisha watu wa kada mbalimbali na kupanga jinsi ya kuandaa na kuandika katiba hiyo.

“Katiba ni kama moyo; hata sisi binadamu moyo ukiwa na tatizo ni lazima uende hospitali kwa ajili ya kupata tiba. Kwa hiyo hii katiba inayotumika sasa nayo ni lazima itazamwe upya,” alisema Tendwa wakati akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) jana jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo uliowashirikisha viongozi na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa nchini ulikubaliana kuwa utatolewa muongozo utakaoeleza mapungufu ya katiba inayotumika sasa na aina ya katiba mpya inayotakiwa na Watanzania.

Pia walikubaliana kuitisha mkutano mkubwa utakaojumuisha asasi za kiraia, taasisi za dini, vyama vya wafanyakazi na wakulima pamoja na wananchi kwa ajili ya kujadili muongozo huo pamoja na kupeleka maazimio ya yaliyojadiliwa katika mkutano huo serikalini.

Tendwa, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa kuhusu suala zima la matatizo ya katiba ya sasa hasa inapofikia uchaguzi mkuu, alisema: “Kuna baadhi ya vyama nchini Kenya vilipinga sana suala la kuwa na katiba mpya... tusifikie wakati tukaona kuwa hakuna haja ya kuwa na katiba mpya... lazima tujadili kwanza ni katiba ya namna gani tunayoihitaji tena kwa kuwashirikisha wadau wote.”

Tendwa alifafanua kuwa yuko tayari kuyafanyia kazi majumuisho yote ya mkutano huo huku akinukuu baadhi ya vifungu vilivyomo katika katiba hiyo ambavyo kwa namna moja au nyingine vimekuwa vikilalamikiwa kuwa havina maana yoyote.

“Katiba zetu kati ya 1961 na 1965 hazikuwa na haki za binadamu bali haki hizo ziliwekwa kama utangulizi, hatahivyo haki hizo ziliwekwa katika sheria namba 15 ya 1984 iliyorekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa mwaka 1977,” alisema Tendwa.

Tendwa alitoa angalizo kwa kueleza kuwa historia inaonyesha kwamba chaguzi za Kenya na Uganda zilizingirwa na migogoro iliyoanzishwa na vyama vya siasa na matamshi ya waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa na kuongeza kuwa wakati mwingine ubaya wa chaguzi hizo ulisemekana kuwa ni katiba.

“Imeelezwa kuwa katiba za nchi hizi zimehusika katika kuzisimamia chaguzi hizi mbaya; hazionyeshi utawala bora na nyingi zina misingi ya tawala za chama kimoja," alisema Tendwa.

"Vile vile rais ana madaraka makubwa na mamlaka ya kuteua Tume ya Uchaguzi, tume ambayo husimamia mchakato wa uchaguzi mzima na hasa uhesabuji wa kura. Suala jingine ni rushwa katika uongozi wa kisiasa."

Tendwa alisema Tanzania kwa sasa ina miaka 49 tangu ipate uhuru, lakini akahoji katika kipindi hicho "watu wamebadilika kiasi gani? Haina ubishi kwamba demokrasia imekua katika kipindi hicho, lakini kwa misingi ipi?"

Msajili huyo aliweka bayana kuwa katiba ya sasa ya Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki bado ina misingi ya kikoloni.

Tendwa alikiri kwamba kumekuwepo na mabadiliko makubwa tangu uhuru akibainisha ujenzi wa shule, vyuo vikuu, mitandao ya afya na mifuko ya jamii, barabara na mawasiliano, kukua kwa kilimo na uzalishaji mazao bora.

Lakini akaongeza: "Hata hivyo mheshimiwa mwenyekiti, hatuwezi kujidanganya kwa hayo tuliyoyafikia na kwamba pengine tungepata maendeleo makubwa kama tungekuwa na katiba nzuri zaidi na yenye kuzingatia misingi ya kijiografia, jamii ya Watanzania, misingi bora na utashi wa kisiasa na rasilimali za nchi."

Msajili huyo aliisifu Kenya kuwa imeibuka na katiba yenye uasilia wa nchi hiyo baada ya mijadala kadhaa na hata mabadiliko ya tume au kamati ya rasimu ya katiba ya mara kwa mara.

Pia alisema katika nchi nyingine katiba zimeshutumiwa kwa kuwa na viraka vingi vinavyowekwa kila mwaka na ambavyo mara nyingi huungwa mkono na kupitishwa na chama chenye wabunge wengi ndani ya Bunge.

"Jambo kubwa linalolalamikiwa na , Mheshimiwa mwenyekiti, na wadau wengi ni mamlaka ya rais. "Niruhusu... niseme nukuu ya mwanafalsafa mmoja Sir William Blackstone ambaye kwa kuangalia mamlaka ya mfalme wa Uingereza mwaka 1765 alisema 'The King can do no wrong is a necessary and fundamental principle of the English Constitution(mfalme hawezi kufanya makosa ndio msingi mkuu wa katiba ya Uingereza)'. Ukibadili neno King na Rais... basi kwa hali hiyo utaona mantiki ya kilio cha wapinzani," alisema.

Awali makamu mwenyekiti wa TCD, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye pia ni mwenyekiti wa CUF, alisema kuwa katiba mpya inatakiwa itokane na mapendekezo ya wananchi, iwe ni misingi ya demokrasia, wananchi wawe na haki ya kuchagua na kuchaguliwa.

“Mbali na hilo rasilimali za nchi zinatakiwa kutumika kwa manufaa ya wananchi. Mpaka sasa katiba yetu tayari ina vikara 15 hivyo ni vyema ukaandaliwa mchakato mzito kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi suala hili la katiba,” alisema Lipumba.

source?
 
Ila Tendwa hafai kuwa kiongozi wa Constitutional Conference, awe mjumbe tu. anaweza kuwa kasuku wa viongozi wasiotaka katiba mpya, na wakamtumia kuivuruga kwa kufanya mabadiliko ya kisanii tu, na kutofanya mabadiliko yanayohitajika. Maana kauli yake ya ..."niko tayari kufanyia kazi majumuisho yote ya mkutano huo (wa katiba)..." inaonyesha kama anataka kuteka (hijacking) mjadala huo, hadidu za rejea na kikubwa zaidi majumuisho yake.

Kiongzi au Mwenyekiti anafaa awe mtu kama Prof Issa Shivji.
 
njaa tu zinamsumbua mzee huyu, anataka atimuliwe kabla hajastaafu/hajafia katika hicho cheo?
 
Tendwa: Iundwe katiba mpya kabla mambo kuharibika Wednesday, 15 December 2010 07:41

Fidelis Butahe na Vicky Kombe
MJADALA wa madai ya katiba mpya jana uliendelea kupamba moto wakati Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alipojitosa kwa kusema kuwa kkatiba mpya inatakiwa kabla mambo hayajaharibika na kupendekeza kuwepo kwa mkutano wa kitaifa wa kikatiba utakaojumuisha watu wa kada mbalimbali.
“Hata kama tuko katika taasisi za serikali, lazima tueleze ukweli. Mnaona wenyewe jinsi Bunge lilivyo na kigugumizi cha kuundwa kwa katiba mpya,” alisema Tendwa.

Tendwa: Iundwe katiba mpya kabla mambo kuharibika

Ahsante Mungu uliyemwonyesha Sauli njia sahihi,na baadaye akauona nuru yako na akakoma kuwatesa watu wako, hatimaye akawa mtume Paulo! Tendwa huenda akawa Paulo katika hili, baada ya kumuongezea mgombea mmoja muda wa kampeni kutoka saa 12 jioni mpaka saa 1, na kushabikia kampeni za nyumba kwa nyumba za usiku!
 
Hili la katiba mpya hawawezi kulikwepa. Sasa hivi ni kuweka msisitizo wa hali ya juu ili ipatikane kabla ya uchaguzi wa 2015. Tendwa kasoma alama za nyakati.
 
List of fame and shame inaongezeka.

Huyu mzee angesaidia sana katika kuweka a level playing ground kama angekuwa na ujasiri.

Angewapa CCM muda wa miezi 6 ili kuondoa neno Mapinduzi na kuweka lengine katika jina la chama chao kama wasingetimiza sharti hilo akakifuta. Hatutaki vyama vya mapinduzi tz sasa ni wakati wa demokrasia sia DOMOkrasi.

Pili, angezuia Ruzuku kwa CCM at least kwa miaka 3 ili vyama vyengine vipate kuwafikia wananchi vijijini.

Tatu, angesimamia kwa haraka kupatikana sheria inayoruhusu vyama kuungana.
 
Haya ndiyo maneno. kilichobaki ni kauli rasmi ccm

Bado wanajadiliana kwanza kuhusu tamko ambalo watalitoa kuhusiana na hili la katiba mpya. Kama ujuavyo ndani ya CCM kuna kambi chungu nzima, hivyo bado hawajakubaliana watoe tamko lipi na pia kuna wale ambao wanataka wakae kimya tu kama vile hawajazisikia kelele za kutaka katiba mpya.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom