Tendwa hana mamlaka (kisheria) ya kufuta chama cha siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa hana mamlaka (kisheria) ya kufuta chama cha siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makene, Sep 28, 2012.

 1. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,477
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kutokana na ufafanuzi wa justice Mihayo, majukumu ya registrer ni kuandika vyama na ku'audit kasma wanazopewa.

  Hapewi mamlaka kisheria ya kuagiza vyama vya upinzani mambo ya kufanya, kama ilivyo kwa polisi hawana dhamana ya kuruhusu maandamano yafanyike au la.

  Vinginevyo wanaingilia uhuru wa demokrasia na kukwamisha kukua kwa demokrasia ya vyama vingi nchini.
   
 2. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wenyewe hawajui hilo, wanaropoka tu
   
 3. M

  Maseto JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 698
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa naangalia kipindi cha this week in perspective ambapo nimegundua kuwa msajiri wa vya siasa hana mamlaka kisheria kufuta vya siasa.

  Hii ni kwa mujibu wa Jaji Mihayo kuwa msajili anapewa majukumu mawili tu na sheria ambayo ni kusajiri vyama na kuvikagua juu ya matumizi ya ruzuku zinazotolewa na serikali.

  Ndg. Mihayo anasema kuwa msajili anapiga mkwara wa kufuta vyama kwa sababu ya kuziba ombwe la kutokuwa na shughuli ya kufanya.
   
 4. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,084
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  Kumbeee! Now we know, at least we can ask him why is he overlapping his position? Ndio kubaka demokrasia huko anakofanya..... I mean Arumeru East and recently that ataifuta CHADEMA.
   
 5. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 5,566
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Tendwa analijua hilo dhahiri!ila alifikiri watanzania wote bado ni mapimbi,baada ya kauli ile ya ukweli ilyojaa dharau kutoka kwa Mh Dr slaa tendwa aliingia mitini jumla,sikuwahi kumsikia tena,sasa hivi anajiuliza kama hawa ni watanzania wale aliokuwa anawaelewa au lah.
   
 6. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 5,566
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Watajulia wapi hao?huwa wanafunika vichwa vyao na wakiamka wanapiga adhana!kumbe ni saa tano za mchana!kwe kwe kweee
   
 7. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 827
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kayasema wapi haya jaji mihayo?
   
 8. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 3,920
  Likes Received: 1,532
  Trophy Points: 280
  Kayasema katika kipindi cha This Week in Perspective cha tbccm. Kilikuwa bonge la kipindi. Very Oobjective.

  Nadhani Simbeye atapigwa ban na tbc kuendesha hicho kipindi. Huyu jamaa ni very objective sidhani km anaweza kutumiwa na CCM. Binafsi hiki ndio kipindi pekee nachoangalia tbccm.

  Ila sioni kipindi hiki kikiendelea kwa muda mrefu ujao. Kama leo jaji Mihayo alikuwa very critical of watawala wa CCM na hofu ya kupoteza madaraka, jambo ambalo linaminya ukuaji wa demokrasia hapa nchini.
   
 9. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,965
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mseto km jaji mihayo kasema hivyo, vyema. ni kipengele kipi huyu kilaza tendwa alikuwa anatumia kuitisha cdm kuwa ataifuta? after all i dont remember when last, i watched tbc.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kwani kuna chama kilichoogopa mkwara wake? Huyu jamaa anajiandikia histiria mbaya kwenye kubaka demokrasia kutokana na ulimbukeni wa madaraka aliyozawadiwa.
   
 11. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,238
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Kwenye kipindi cha this week in perspective
   
 12. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 728
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tatizo la rules na guidelines za responsibilities mbali mbali za viongozi zina mambo ya vipengele. Unaweza kuta kuna kakipengele fulani kakipuuzi kabisa unaweza kabadilisha ama kukapindisha kuweza fanikisha azma hiyo.

  Wasema in social science 'yes' na 'no' yote ni majibu sahihi.
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24,925
  Likes Received: 1,982
  Trophy Points: 280
  Kipindi chenyewe ni cha kingereza!!
   
 14. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,514
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Asante sana Jaji Mihayo, umetoa Tuition ya bure kwa TENDWA, NAPE, WASSIRA, MWIGULU, NCHIMBI NA SOFIA SIMBA na yule engineer fake Manyanya.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 30,798
  Likes Received: 4,178
  Trophy Points: 280
  taratibu jamani; tendwa anayo mamlaka ya kukifuta chama cha siasa na ni mamlaka ya kisheria. Kitu ambacho hana (na sidhani kama angeweza kuwa nacho) ni kukifuta chama kiholela. Kwamba kachukia na walivyomjibu au hapendi siasa zao basi anakifuta; mamlaka hayo hana. Mamlaka ya kufuta chama yapo kwa mujibu wa sheria lakini kwa kanuni zilizowekwa. Tendwa anayo madaraka ya kukifuta chama cha siasa; lakini madaraka hayo yamewekewa uzio mkubwa kwa mabadiliko ya sheria ya mwaka 2009 ya yanamzuia Msajili kukifuta chama cha siasa kama uchaguzi mkuu utafanyika ndani ya miezi kumi na mbili. Ina maana hawezi kufuta chama cha siasa kama uchaguzi mkuu uko ndani ya miezi kumi na mbili. Na pia kuna masharti mengine.
   
 16. i

  iseesa JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUMBUKUMBU: Mwongozo wa spika!!!...Akasimama Mh. LUKUVI! Mwongozo wa Spika Mh Lukuvi! Akaitika Mh NDUGAI! .....Ndugu SPIKA Naomba Mheshimiwa MBUNGE afute Kauli yake kuwa Seikali inaBAKA Demokrasia. Kufuatana na Kamusi ya Kiswahili Mh Spika, Kubaka ni .........Akajibu Mh NDUGAI... Mh Mbuge futa neno KUBAKA .....Hivyo Bwwana Arushone angalia Mh LUKUVI asikusahihishe kwa kuwa hajui maana ya misemo na nahau za Kiswahili
   
 17. p

  politiki JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,325
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Msajili hana uwezo wa kufuta chama chochote anachoweza kukifanya ni kukifikisha chama usika mahakamani kwa kukosa sifa au kuvunja sheria za kuundwa/kusajiliwa kwake na inabidi aishawishi mahakama na ndiyo mahakama imkubalie kwa mujibu wa sheria kukifuta chama hicho kumbuka kwenye kesi ya TTP na PONA msajili alikwenda mahakamani kwanza na baada ya wahusika kushindwa kwa kushindwa kuitisha uchaguzi ndani ya vyama vyao mahakama ikarithia wakafutwa.
   
 18. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,665
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135

  Mkuu ukituwekea hizo kanuni tutakwenda sawa zaidi.
   
 19. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni kweli Mwanakijiji,tatizo watu wanaleta ushabiki kwenye ukweli,jamani tujaribu kuwa serious katika mambo ya msingi.i salute 4u my brother.
   
Loading...