Tendwa: CCM inaporomoka na upinzani unakuwa kwa asilimia 40

Pawaga

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
1,330
966
Haya yamezungumzwa na mh Tendwa kuwa upinzani unakuwa kwa kasi ya 40 asilimia na magamba yanaporoka. Kuna watu humu jamvini wakiambiwa huwa wanabisha sana nadhani sasa wataelewa maana hata hao wakubwa wao wanalijua hilo.

Source: Nipashe

tendwa1(38).jpg


Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa




Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amesema matokeo ya uchaguzi mdogo wa Igunga ambao mgombea wa CCM alishinda kwa mara nyingine yametoa picha kuwa upinzani unazidi kukua na CCM inashuka.....

Akitoa tathimini ya uchaguzi huo, ambao ushindani mkubwa ulishuhudiwa miongoni mwa vyama vitatu wakati wa kampeni, CCM, Chadema na CUF, Tendwa, alisema alikwisha kusema tangu baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kuwa upinzani umekua kwa asilimia 40 ikilinganisha na ushindi wa kishindo wa CCM wa mwaka 2005. "Matokeo ya uchaguzi wa Igunga yanaonyesha kuwa upinzani unazidi kukua na CCM inashuka," alisema Tendwa alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari. Alisema hali hiyo inatokana na ushindani mkubwa wa kisiasa uliopo hivi sasa nchini kati ya vyama vya upinzani na CCM.


Kadhalika alitaja sababu za watu wachache kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora, ikilinganishwa na idadi ya walioandikishwa, kuwa ni pamoja na
ujambazi wa kisiasa uliofanywa na baadhi ya wanasiasa kununua shahada za wapigakura.


Wakati Tendwa akitaja sababu hizo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo, Protace Magayene, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kubuni mbinu mbadala ya kuhakikisha wananchi wanajitokeza kupiga kura. Wapigakura walioandikishwa katika Jimbo la Igunga ni 171,019 na waliojitokeza kupiga kura mwaka huu ni 53,672 sawa na asilimia 31.3, kukiwapo ongezeko la asilimia 2.7 ikilinganishwa na idadi ya waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ambao walikuwa 49,013 sawa na asilimia 28.6 ya 171,077 waliokuwa wamejiandikisha.


Hata hivyo, Tendwa, alisema:"Uchaguzi ulikuwa wa amani na utulivu. Kura zilipigwa kwa amani, hakukuwa na msukosuko, ingawa kulikuwa na kasoro za kiutendaji. Kasoro hizo zimewaathiri watu wa Igunga kutokupiga kura. Aliongeza: "Athari hizo si kubwa, lakini athari ni athari. Idadi ya waliojitokeza kupiga kura Igunga inasikitisha … Nasubiri ripoti, lakini nimeambiwa kulikuwa na kununua kwa kadi za kupiga kura na baadhi ya wanasiasa. Huu ni ujambazi wa kisiasa."


Alisema sababu nyingine iliyochangia watu wachache kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo, ni kauli na vitendo vya vitisho vilivyotolewa na baadhi ya wanasiasa wakati wa kampeni. Tendwa alisema vitisho hivyo viliwafanya wananchi wa Igunga, ambao wengi wao wanaishi vijijini kuogopa kwenda kupiga kura, badala yake kuamua kwenda kutafuta mahitaji yao muhimu, kama vile maji..............

........Hata hivyo, alisema kila chama cha siasa, kikiwamo chama tawala (CCM), kinawajibika kubadilika na kuzingatia utawala bora, uongozi mzuri na uvumilivu wa kisiasa kwa vile hakiko peke yake katika medani za siasa.

Source: IPPMedia
 
Wewe unafikiri kuna mtu halioni hilo? Hawataki kukubali ukweli tu, wanatafuta vijisababu vya kujipa moyo! Achana nao; tutumie nguvu, muda na akili zetu kuzidi kuimarisha upinzani ni si kujibizana nao!
 
Wewe unafikiri kuna mtu halioni hilo? Hawataki kukubali ukweli tu, wanatafuta vijisababu vya kujipa moyo! Achana nao; tutumie nguvu, muda na akili zetu kuzidi kuimarisha upinzani ni si kujibizana nao!
Tendwa amemua kuwafurahisha tu magwandwa lakini haimanishi anachokisema
 
Ndio sababu wakaja na hii strategy (ambayo inawashinda!) ya kuvua magamba!
 
haya yamezungumzwa na mh tendwa kuwa upinzani unakuwa kwa kasi ya 40 asilimia na magamba yanaporoka. Kuna watu humu jamvini wakiambiwa huwa wanabisha sana nadhani sasa wataelewa maana hata hao wakubwa wao wanalijua hilo. Source: Nipashe
mchana wanakataa ila usiku wanakiri kwenye mashuka waliyojifunika
 
Hata asingesema Tendwa, ukweli tayari unaonekana. Magamba wanategemea vijijini tu (less informated areas). Igunga mashahidi
 
Haya yamezungumzwa na mh Tendwa kuwa upinzani unakuwa kwa kasi ya 40 asilimia na magamba yanaporoka. Kuna watu humu jamvini wakiambiwa huwa wanabisha sana nadhani sasa wataelewa maana hata hao wakubwa wao wanalijua hilo. Source: Nipashe

Kweli Mwenye macho haambiwi tazama nguzo pekee waliyobaki nayo CCM ni wajumbe wa nyumba kumi na hili swali mjumbe wako nani? kwenye vyombo vya kidola na nyaraka za serikali litakoma lini
 
ndio analitambua hilo leo. mtu hahitaji Phd kuelewa kuwa chama cha magamba kimepoteza mvuto kwa watanganyika
 
CCM inakufa rasmi 2015,sasa inaporomoka sana,si mmeona igunga??? imepoteza kura karibia 9000 ndani ya mwaka mmoja tu,ukifuata sequence+series utajua tu whats next,mpaka 2015 watakuwa na kura 8,000 tu katika kura 75000.

Hizo ni Hesabu,kwa tasmini inaonekana kila mwaka ccm inapoteza wapiga kura 9000 na kila mwaka wapiga kura wanaongezeka 5000,kwahiyo mpaka 2015 kwa igunga(sample space) itakuwa na wapiga kura 75,000,kwahito mpaka 2015 ccm itakuwa imepoteza wapiga kura 36,000 katika mtaji wao wa kura 26000,kwahiyo jibu ushapata hapo igunga ni CDM 2015 na asilimia 40% ya viti bungeni(wabunge zidi ya 145),
 
Kitu kimoja kizuri sana ambacho kitaiendeleza Tanzania ni kuwa na upinzani wa kweli, hiyo ni faraja na neema kwa kila Mtanzania, lakini si upinzani kama wa CHADEMA, upinzani wa kuongelea watu badala ya sera.

Kwa kuwa Tanzania bado ni mwanjo mwanjo katika siasa za vyama vingi, kila mtu anawaona magamba kwa sasa wamaana sana kwa kuwa wanachokiona ni wao kwa mara ya kwanza ndio hicho cha kuongelea watu, Watanzania ni kama vipofu tilioona punda. Lakini, kizuri ni kuwa watu wameshaanza kujuwa siasa maji taka ni nini na siasa za maendeleo ni nini, siasa maji taka ni turufu ya ya garasa, turufu ya mali ni siasa za kuleta maendeleo kwa vitendo. Hakuna mpaka sasa chama pinzani kilichoonesha haswa namna yakutatuwa matatizo yanayomkabili Mtanzania kila siku, wapinzani kila kukicha, Rostam, Kingunge, Makamba, Januari, Februari. Ni nini hii?

Tunataka kusikia upinzani umeingia ubia na kampuni la kufuwa umeme wa bei poa, kama alivyojaribu Mrema. Tunataka kuona upinzani unajenga shule bora za kuigwa japo moja kila mkoa kwa kuanzia, tunataka kuona upizani unaanzisha viwanda vya mfano, ambavyo watasema haya ndio mnayakosa kwa kuichaguwa CCM.

Leo upinzani umekazana Rostam, Rostam, Rostam, Rostam. Huyo Rostam amekuwa mkubwa kuliko upinzani wote, anatisha kwa kutukuzwa na upinzani, kama mnajuwa ana madhambi mbona hatuwaoni mkampeleka mahakamani? au mnaogopa atawaadhiri kama alivyomwadhiri Mtikila?

Hakuna wa kusifiwa kwa kuuboresha upinzani katika Tanzania kama Kikwete, yeye ndio alioahidi kuikuza demokrasi na kweli anafanya hivyo, kwa wengine hatuoni ajabu, ila tunachostaajabu tunapoona upinzani umepewa fursa kubwa sana katika awamu hii lakini hawazitumii ipasavyo, wao wamebaki na ngonjera za Rostam.
 
Haya yamezungumzwa na mh Tendwa kuwa upinzani unakuwa kwa kasi ya 40 asilimia na magamba yanaporoka. Kuna watu humu jamvini wakiambiwa huwa wanabisha sana nadhani sasa wataelewa maana hata hao wakubwa wao wanalijua hilo. Source: Nipashe
Mzee tendwa hebu kuwa muwazi - badala ya upinzani just say "CDM inakuwa kwa kasi ya 40%"
 
FF hivi halmashauri zilizo chini ya upinzani unazionaje kiufanisi?
 
Tendwa amemua kuwafurahisha tu magwandwa lakini haimanishi anachokisema

Nyie ndio wanafiki mnaokiua chama chenu,haya kati yako wewe na Tendwa nani anaijua CCM?we umekuja juzi tu na hujui lolote kuhusu CCM acha kushabikia kitu usichokijua wewe.
 
Back
Top Bottom