Tendwa: CCM inaporomoka na upinzani unakuwa kwa asilimia 40

Wanasheria watusaidie kuhusu chama kununua shahada, je inawezekana kutengua matokeo kama ushahidi utakuwepo?
 
Anazuga tu huyo, kwani hajui chama kinachonunua kadi za wapigajura kila uchaguzi unapowadia, mnakumbuka kuna jamaa alikamatwa na kadi polisi wakasema si kosa mtu kukamatwa na kadi?
 
Tendwa utapona kweli au wakribia ku staafu au unatuzuga kwamba huko nao jamaa wanunua shahada ? Polisi walisema si kosa mkakaa kimya leo baada ya kila kitu kuwa wazi ndiyo mnakurupuka ? Kweli Tanzania ina maajabu .

Ndo tz yetu hii. Majangili yamejipenyeza na sasa yanashika nchi. Msajaili wa vyama kwa sasa anapotezea tu, hana ubavu wowote! Ye mwenyewe ana mtii aliyempa kibarua! katiba mpya ndo suluhisho la yote!
 
Ndege njanja hunaswa kwenye tundu bovu. Idadi ya waliochoshwa na uchakachuaji na ujambazi wa kisiasa inazidi kuongezeka, hadi 215 njia itakuwa nyeupe na taratibu za wapiga kura kufanyia marekebisho.
 



Wakati Tendwa akitaja sababu hizo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo, Protace Magayene, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kubuni mbinu mbadala ya kuhakikisha wananchi wanajitokeza kupiga kura. Wapigakura walioandikishwa katika Jimbo la Igunga ni 171,019 na waliojitokeza kupiga kura mwaka huu ni 53,672 sawa na asilimia 31.3, kukiwapo ongezeko la asilimia 2.7 ikilinganishwa na idadi ya waliopiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ambao walikuwa 49,013 sawa na asilimia 28.6 ya 171,077 waliokuwa wamejiandikisha.

Source: IPPMedia

Moja ya mbinu hizo ni hii hapa...
https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/179163-tanzania-inahitaji-compulsory-voting-for-2015-and-beyond.html
 
Ameyataja machache tu. Ccm ilipeleka green guide waliokuwa wananyanyasa wananchi waliokuwa na mwelekeo wa upinzani. Polisi waliokuwa wanakamata watu hovyo bila makosa, kuwaacha watuhumiwa na kufunga washtaki, kuwatisha watu kwamba wameletwa mungiki na makomandoo kuwafanyia fujo! Kimsingi hata hao waliojitokeza ni wengi!
 
Kadhalika alitaja sababu za watu wachache kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora, ikilinganishwa na idadi ya walioandikishwa, kuwa ni pamoja na ujambazi wa kisiasauliofanywa na baadhi ya wanasiasa kununua shahada za wapigakura.

Hii ni aibu kubwa chama cha kisiasa kufahamika kushinda uchaguzi kwa njia haramu za uambazi wa kununua shahada za wapiga kura kwa siri. Njia hii imeanza kuungwa mkono na baadhi ya watendaji wakuu kama akina Tendwa baada ya kuchoshwa na ubakaji wa demokrasia nchini.
 
Ndege njanja hunaswa kwenye tundu bovu. Idadi ya waliochoshwa na uchakachuaji na ujambazi wa kisiasa inazidi kuongezeka, hadi 215 njia itakuwa nyeupe na taratibu za wapiga kura kufanyia marekebisho.

mkuu mbona 215 ishapita zamani sana? Pia nji maana yake nini?
 
Tz bila ccm inawezekana vijana tuchukue hatua kukabiliana na hili janga linalosababishwa na magamba
 
Back
Top Bottom