Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,011
- 104,716
Jamani Utabiri sii lazima utumie bao, mtu yeyote anaweza kutabiri kisayansi na ikakubalika kutokana na statistical patterns.
Kwa hiyo alichofanya Tendwa ni kutazama Upinzani ulivyojipanga hadi sasa na kuzungumzia ushindani uliopo. Hata JK mwenyewe rais na mgombea anaweza kukiri kwamba safari hii kuna uwezekano mkubwa wa Upinzani kuzoa viti bungeni.
Kwa hiyo hata mtu anayetakiwa kuwa na kuonyesha neutrality kwa mujibu wa kazi yake ni sawa kutabiri?
Utajisikiaje referee wa mechi ya Simba na Yanga kabla ya mechi akisema anatabiri Yanga itafungwa 4-1 ? Wewe kama mpenzi wa Yanga utakuwa na imani na huyu referee ?
Unanikumbusha kuna hadithi moja ya Science Fiction ya Isaac Asimov (Franchise), in some futuristic (then, 1950's future being the 2008 election) United States society watu wameweza, kwa kutumia computer inayoitwa Multivac, kumpata mtu mmoja ambaye input yake ndiyo iko most representative of the whole population, sasa badala ya kila mtu kuhangaika kupiga kura, wanaona inatosha huyu mtu mmoja tu apige kura. Mtu huyu anaitwa Norman Muller.
Inaonekana Tendwa ana Multivac yake huko ofisini kwake, na kashajichagua yeye mwenyewe kuwa Norman Muller wetu, kesho na keshokutwa anaweza kutuambia tuahirishe uchaguzi kwani "patterns and statistics" zote anazo.
Chicago Tribune wenzake walitumia statistics hizo hizo kumtangaza gavana Dewey kumshinda Truman katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 1948, ending with the legendary picture of Truman celebrating sarcastically with a paper carrying the headline "Dewey defeats Truman".