Tendwa aionya CCM kuacha kutumia nyenzo za Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendwa aionya CCM kuacha kutumia nyenzo za Ikulu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 7, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tendwa aionya CCM kuacha kutumia nyenzo za Ikulu

  BARAZA la Ushauri wa Vyama vya Siasa nchini, limekishukia CCM na kukitaka kutotumia picha zilizopigwa Ikulu katika kampeni zake.Onyo hilo lilitolewa jana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.Tendwa, alisema hayo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano ulivyovishirikisha vyama Baraza la Ushauri wa Vyama vya Siasa nchini.

  “Picha za kampeni za CCM zinazoonyesha Ikulu zisitumike, ukitumia hizo picha halafu chini yake ukasema chagua chama fulani, hiyo itakuwa siyo demokrasia kwa sababu hata aliyepiga hizo picha ni mfanyakazi wa Ikulu,” alisema Tendwa.

  Kwa mujibu wa Tendwa, picha hizo pia zinawashawishi wananchi kuipigia kura chama hicho na kuwa vyama vingine haviwezi kuzipata kutokana na kutoweza kupiga picha katika eneo hilo.

  Mbali na kuitaka CCM iache kutumia picha zilizopigwa Ikulu, Tendwa alikita chama hicho pia kuacha kuvifanyia vurugu vyama vingine vya siasa.

  Alisema CCM inawatumia vijana wa UVCCM, kufanya vurugu katika kampeni za vyama vingine vya siasa ikiwamo kuchana mabango ya wagombea na kutoa bendera za vyama hivyo.

  Alikitaka chama hicho kuacha tabia hiyo mara moja.

  Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni za Urais za CCM, Abdulrahman Kinana alikanusha tuhuma hizo akisema hazikutolewa na Tendwa.

  “Mimi nina ‘tap’ (mkanda uliorekodiwa) yake, hajazungumzia hilo. Kwa sababu hiyo usiniulize kuhusu mambo ambayo hakuyazungumzia,” alisema Kinana.

  Kinana pia alisema ana uhakika kwamba, Tendwa hakusema kuwa vijana wa CCM wanawafanyia vurugu vyama vingine vya siasa.

  Hata hivyo alipotakiwa kufafanua kuhusu tuhuma za CCM kutumia rasilimali za serikali katika kufanikisha kampeni zake ajibu: “Siyo kweli."

  Alisema CCM inatumia rasilimali zake yenyewe kufanikisha kampeni hizo na sio rasilimali za umma.
  Baraza hilo limeonya pia juu ya kampeni chafu zinazoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa na likivitaka kuacha kufanya hivyo.

  “Baraza halijaridhika na utekelezaji wa kanuni za uchaguzi kwa hiyo limeitaka Tume na Msajili kutoa tamko pale kanuni hizi zinapovunjwa,” alisema Tendwa.

  Katika taarifa yake Tendwa pia aliitaka Taasisi ya Kuzuaia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kuwachunguza wagombea wanaojitoa baada ya kuanza kwa kampeni.

  “Baraza limehisi kuna harufu ya rushwa katika hili, ndiyo maana wakaitaka Takukuru iwachunguze hawa watu na pia limetaka itungwe sheria itakayo wabana hawa watu,” alisema Tendwa.

  Baraza hilo pia liliitaka Takukuru kuwachunguza wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambao wanavujisha siri za taarifa za rushwa wanazopewa na wananchi hali inayofanya zoezi la kuwakamata kushindikana.

  Baraza hilo pia limevitaka vyombo vya habari nchini kutokuwa wakereketwa wa vyama vya siasa ili kutenda haki kwa vyama vyote.
  “Lakini kwa vile vya serikali tunavitaka vitoe ‘fair play’ (haki sawa) kwa vyama vyote,” alisema Tendwa.

  Kwa mujibu wa Tendwa, Baraza hilo limetaka kutoa tamko ili ufanyike mdahalo wa wagombea urais katika vyombo vya habari kwa vile mdahalo wa sasa wa wabunge unafanyika kwa upendeleo.

  “Mimi kama msajili nina-encourage (ninaunga mkono) kuwepo na ‘dialog’ (mdahalo) ili kila mmoja apate nafasi ya kueleza sera zake, kwa sababu baraza linaona wagombea wenyewe wapo saba tu, kwa hiyo ni bora utaratibu ukawekwa hata wakifanya wanne siyo mbaya,” alisema Tendwa.

  Pamoja na mambo mengine, baraza hilo lilimtaka msajili kutoa tamko kuwa hakuna chama kidogo na kikubwa kwa kuwa vyote ni vyama vilivyopata usajili kwa mujibu wa sheria.
  Kutokana na agizo hilo Tendwa alifafanua kuwa hakuna chama kidogo wala cha msimu na kwamba, chama chochote kitakachotimiza masharti kitasajiliwa bila kikwazo.

  Hata hivyo alisema kuwa, yuko mbioni kurekebisha kanuni ambayo itamruhusu kupandisha ada ya usajili wa vyama vya siasa kutoka Sh25,000 kwa usajili wa muda mpaka Sh500,000 na usajili wa kudumu ukitoka Sh50,000 mpaka Sh1,000,000.

  Chanzo: Mwanachi
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Duh -- mambo hayo! Halafu watajigamba wanashinda kwa halali na kwa kishindo!!! Hivi CCM huwa haina kabisa ustaarabu wa kufanya kampeni zake kama chama cha siasa na siyo kama serikali?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwa nini wasichukuliwe hatua? Ingekuwa chama cha upinzani saa hizi tayari kimefutwa.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tendwa anajikosha kwa madudu ya kutupa pingamizi
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na picha za mabango haya siyo zile Mwanahalisi liliandika kuchapishwa kwa gharama ya serikali -- dili iliyoratibiwa na akina Salva? sasa hawa Takukuru wako wapi kuchunguza hilo? Mimi naona Chadema wasichoke kuweka msururu wa mapingamizi dhidi ya CCM hata kama yanashindwa -- ili mradi wananchi wajue tu CCM inavyofanya rafu. Na kama Tendwa anazungumzia kwamba pingamizi lile la Chadema limeleta chuki miongoni mwa wananchi, hili la mabango jee? Yaani wananchi wamependezwa nalo?
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yeah -- anajikosha kwa Chadema baada ya kuwaminya katika uamuzi wake wa kumtumikia bwana!!
   
 7. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  CCM ina uchu wa madaraka (wa kuhodhi madaraka) ndio maana wapo tayari kumwaga damu ili wabaki madarakani. Kama kutatokea mapigano kati yetu, yatakuwa yametokana na uchu wa CCM kuhodhi madaraka. Na tukumbuke mauaji ya Pemba. CCM wameshamwaga damu ya Watanzania huko nyuma. They will do anything to hold on to power.
   
 8. P

  Pax JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Jana wengi wetu, wenye vyama na wasio na vyama tumeshuhudia Tendwa akijiwekea historia yake binafsi pamoja na kudhalilisha fani ya sheria kwamara nyingine tena. Amejidhalilisha kwa kukosa umakini na uadilifu usiokuwa na mvuto wa itikadi za vyama. Amekubali kuwapigia magoti wasaliti wa amani na uwajibikaji uliotukuka. Tendwa amekosa uadilifu, na najua nafsi yake inamsuta katika jambo hili. Ameingia kwenye mtego pasipo kujua. Hoja ya msingi ni moja tu, sheria imevunjwa ama sio?

  Natumai angeanza kwa kutusomea kifungu cha sheria kilichovunjwa kinasemaje, halafu tuangalie aliyoyafanya Kikwete yanakwenda kinyume na sheria hiyo au hapana? Haihitaji hata siku tano kuamua jambo kama hili. Tendwa kaamua kuwadhalilisha wanasheria wa Tanzania kwa makusudi kabisa kwa ajili ya maslahi binafsi. Haiingii akilini mishahara ipandishwe kwenye jukwaa la kampeni halafu mtu aseme haikuwana nia ya kushawishi wapiga kura. Ni ulimbukeni uliovuka mipaka kuamini vinginevyo, na hata aliyetoa hiyo amri kuongeza mishahara nafsi yake inamsuta maana anafahamu fika lengo ni kushawishi apate kura. Ni laana na dhambi kubwa kutunga sheria na kuipitisha kwa mbwembwe huku ukijua hutaitimiza, alimtungia nani hiyo sheria? Nafananisha sheria hii na mtu aliamua kuchimba makaburi akijua watazikwa wengine kumbe yeye anakuwa wa mwanzo kuzikwa humo.

  Nchi yetu imekosa dira, imekosa muelekeo, imelewa. Viongozi wamelewa madaraka. Wanasheria wamejaa maslahi binafsi, wanashindwa kuheshimu haki. Fikra zao zimemezwa na wanasiasa bila wao kufahamu, wamechoka, wamefilisika mawazo na uadilifu.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, BARIKI WAPENDA MABADILIKO WOTE WANAOIPIGANIA NCHI YETU KATIKA KWELI, WATETEA AMANI NA UADILIFU UWALINDE DAIMA.
   
 9. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Wewe Pax ulitaka aamue kinyume kukufurahisha wewe. Do not be.....ly!!
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kumbuka 16 June 2010, Fikiria Jana na tungoje 31 Oktoba 2010. Wahusika wakuu katika tarehe zote hizo ni wanasheria.

  Tutegemee nini 31 Oktoba???????
   
 11. M

  MAHDI New Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari waungwana wa jamii topic yangu hi hii
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ninaamini sasa JUSTICE is UNJUST
   
 13. P

  Pax JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Sijasema mahali popote kuwa nilitaka anifurahishe mimi, na wala sijasema amfurahishe mtu yeyote, nimesema atueleze na kutufafanualia kifungu hicho cha sheria kinasema nini maana ndio fani yake halafu atuambie ni kwa namna gani jambo alilofanya Kikwete limekivunja ama halijavunja hicho kifungu cha hiyo sheria. Hakuna nililosema zaidi ya hapo, sasa hapa ......ly! uliyosema nitakuwa mimi au ni wewe? Umepewa akili na fikra za kufikiri lakini unakimbilia kuongelea mambo bila kuangalia kwa undani nini maana yake. Ni watu ka ninyi msiotaka kufikiri ndio mnarudisha nyuma maendeleo ya hii nchi tunayoipenda. Ushauri wa bure, soma, tafakari halafu andika. Umasikini wa kufikiri ni mbaya kuliko aina yoyote ya umasikini hata kama umejaa hela za ufisadi. Ni kansa inayomaliza Taifa hili, ni kansa iliyowakamata wengi, ni kansa inayomaliza heshima ya wanasheria maana hawajielewi hata wako wapi. Ni kansa inayomfanya mru atoe majibu mepesi hata kama yanahusu jambo linalohitaji umakini wa hali ya juu. Ni kansa inayomfanya mtu aseme " amelitupilia mbali pingamizi" bila kueleza kwa kigezo na misingi ipi.
   
 14. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  katenda haki au kabana kwa jambo lipi? maana ofisi yake inashughulika na masuala mengi!
   
 15. P

  Pax JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Majibu yapi unayoyajua wewe? hajajibu swali, atueleze sheria imevunjwaje au ni kwa namna gani sheria haijavunjwa?
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hata aende magogoni the fact ni kuwa yeye ni kilaza
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  SHERIA sio TAALUMA. Mnaohangaika na hao wanaojiita WANASHERIA mnapoteza muda wenu tu. Hivi mlitarajia "hukumu" gani zaidi ya hiyo alioitoa kisha akaona AIBU hata kuisoma? Ndio maana mtu anaweza akaua, akaiba, akazini na bado akashinda kesi!
   
 18. P

  Pax JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kajidhalilisha na wanasheria wote kawadhalilisha. Awaombe radhi
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Uko sawa kabisa Pax, Uamuzi uwe wazi na sababu za kufikia uamuzi zitolewe hadharani. Kama hivi vitu havipo basi kisheria hakuna uamuzi kabisa, uamuzi unatolewa na anayeamua na kamwe hautolewi na kuelezwa na mhusika katika suala hilo.

  Tunakwenda wapi nchi hii???????
   
 20. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mimi natamani sasa nisikie Tendwa atasema nini baada ya CCM kupitia katibu wake mkuu kukaidi agizo la Baraza la Vyama kupitia Tendwa kuwa CCM wasitumie mabango ya mgombea wao yanayoonesha Ikulu maana hayo ni ya serikali sio ya CCM. Makamba alisema wataendelea kuyatumia, Tendwa atasema nini juu ya hili?
   
Loading...