Tendwa aikubali CHADEMA. Asema 2015 ni patashika

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,243
Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini, John Tendwa amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kusimamisha mgombea wa Urais mwaka 2015 anayekubalika na Watanzania ili kukabiliana na changamoto za kisiasa zinazozidi kuongezeka hapanchini.

Kadhalika, Tendwa amesema kuanzia sasa ofisi yake itaanza kuvifanyia uchunguzi vyama vyote vya siasa ili kubaini vile ambavyo havifanyi kazi za kisiasa na kuviweka katika madaraja. Aliyasema hayo jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam alipozungumzana waandishi wa habari na kuongeza kuwa kwa sasa changamoto za kisiasa hapa nchini zimezidi kuwa kubwa.

Alisema CCM ili kiweze kuvuka katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ni lazima kisimamishe mgombea ambaye anakubalika na
wananchi wengi. Alitoa mfano kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezidi kuwa na nguvu Bara na Visiwani na kwamba hiyo ni changamoto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Alisema mwaka 2012 vyama vya siasa vilikabiliwa na changamoto nyingi na kwamba sasa ni wakati wa kujiangalia na kujiandaa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mkuu ujao. Alipendekeza kwamba vyama vinavyokuwa kisiasa na kufanikiwa kupata wabunge vinapaswa kupewa ruzuku ili kuviwezesha kufanya vizuri zaidi.

Akizungumzia siasa za Zanzibar, Tendwa alisema kwa sasa zimebadilika kutokana na muafaka uliofikiwa kati ya vyama vya CUF na CCM na hatimaye kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Kuhusu vyama vinavyoibuka katika uchaguzi na kufa baada ya uchaguzikumalizika, Tendwa alisema mwisho wao umefika na kwamba vitajifuta vyenyewe. Aliongeza kuwa ofisi yake itaviweka vyama katika daraja la 1-3 na vile vitakavyoangukia daraja la nne na sifuri havitakuwa vinaalikwa na kutambulika kama vyama vya siasa.

Aidha, Tendwa aliwaambia wanadishi wa habari kuwa kuanzia sasa mfumo wa chama kupata wadhamini ili kisajiliwe utabadilika na badala ya kupata wanachama 200 kila mkoa katika mikoa 10 sasa watatakiwa watu 1,000 kila mkoa.

CHANZO: NIPASHE
 
Ni mbinu za kimchezo na huwa zinatumika mara zote. Hata AC Milan leo wakicheza na Simba Sports Club coach wa AC Milan ataongea maneno yanayofanana na hayo kwa timu pinzani. Usihadaike.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Alisema CCM ili kiweze kuvuka katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ni lazima kisimamishe mgombea ambaye anakubalika na wananchi wengi. Alitoa mfano kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimezidi kuwa na nguvu Bara na Visiwani na kwamba hiyo ni changamoto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
CHANZO: NIPASHE

Huyu jamaa hovyo kabisa........yaani yeye kazi yake kuishauri CCM tu?
 
babalao 2 Hivi huyu mzee ni wa CCM? iweje anatoa ushauri wa kutaka CCM kishinde 2015? ndo maana CHADEMA hawamwamini tena!
 
Last edited by a moderator:
Ameshayapima maji akaona si yakuyapigia mbizi anang'ata na kupuliza mi mwenyewe simpatii picha tangu enzi za injii hii95
 
Huyu ndiye mlezi wa vyama au ni wa ccm pekee. Arumeru aliipigania ccm pamoja na wale wazee wa kimila ila alifel.
 
Tendwa anajua kuwa CCM walishindwa uchaguzi mkuu wa 2010...alijaribu sana kuichafua CHADEMA kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru kwa kutoa vitisho vya kua kwa kutumia wazee wa jadi mwisho wake Kamanda Lema ikabidi atulie...
 
bora CHADEMA iendelee kutomwamini tena huyu pwoyoyo make anazidi kujidhihiri kabisa yeye ni tarumbete ya mabwana zake CCM
 
Hawa Nipashe wamechakachua matamshi ya Tendwa, sio kama nilivyoyaona na kuyasikia jana ITV. Sijawahi kumsikia Tendwa akiongea sensible tangu nimfahamu kama msajili wa vyama vya siasa.

Pamoja na mambo mengine alivilaumu vyama vya siasa vilivyosababisha vifo vya watu katika mikutano yake (hapa alikuwa anailenga moja kwa moja CHADEMA). Akaongeza kuwa 2013 hatasita kukichukulia hatua chama cha siasa kitakachosababisha vifo vya watu katika mikutano yake. (Inaelekea Tendwa naye anayo CD ya Mwigulu Nchemba, maana inaelekea Tendwa anaamini CHADEMA ndiyo iliyomua marehemu Daudi Mwangosi).

Nipashe wamechakachua maneno ya Tendwa, la wadhamini alikataa hiyo idadi ya 1,000 kila mkoa kwasababu alisema kwamba hiyo 200 tu ni kasheshe kwa vyama vingi hivyo akasema atapendekeza idadi iwe 500 kwa kila mikoa 10 ya Tanzania. Sasa sijui hawa Nipashe kwanini wanamuwekea maneno Tendwa kinywani mwake.
 
Mara nyingi najisikia vibaya kujadili hoja marehemu za Msajili na Mlezi wa CCM
 
Tunashukuru Tendwa kwa ushauri wako tutasimamisha mgombea anayekubalika na CCM itaendelea kutawala.
 
Back
Top Bottom