Tendo la kunywa maji wakati wa hotuba kina tija gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tendo la kunywa maji wakati wa hotuba kina tija gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Charles Ignatio, Jun 17, 2011.

 1. Charles Ignatio

  Charles Ignatio Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Mimi nashindwa kuelewa huu ni utamaduni gani ambao wanasiasa wamejiwekea, wa kunywa maji wakati wakitoa hotuba mbalimbali, mimi naweza kuwa nyuma na wala sina sayansi iliyopo lakini msingi wake siuelewi mfano mzuri ni Rais wa Nchi JK anapenda sana kunywa maji na kukatisha hotuba mara kwa mara, Je ni kwamba kuongea ni kazi nzito sana au? na kama kuongea kwa muda mrefu ndio kunawafanya watu hawa kunywa maji sana, hapa sitakubali kwani mbona watu wanaohubiri makanisani na majukwaani kwa muda mrefu kama Mzee wa upako hawanywi maji ovyo ovyo? Hilo pia halitoshi Mr. Budget Mkulo alionekana akikatisha sana hotuba yake, Kwa zaidi ya mara 5 na kuelekeza tension yake kwenye glasi ya maji, duu mpaka ilinishangaza, sasa wadau naomba mnipe ufafanunuzi wa siri iliyomo kwenye hiyo glasi ya maji, au yale huwa sio maji.?? Au yanaongeza konfidensi? Mbona walimu wanaofundisha zaidi ya madarasa matano hawaruhusiwi kunywa chochote wakati wanafundisha? au wanaadress kitu chochote
   
 2. Kinyasi

  Kinyasi Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Ni mikogo ya wanasi-hasa. Hakuna kingine zaidi ya hicho.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Inasaidia kupunguza nervousness. Lakini katika darasa letu la speech teacher alitufundisha kuwa kunywa maji kabla ya kuingia jukwaani.
  Sema something funny to introduce your topic na wakati wasikilizaji wanacheka unavuta pumzi na kujianda kumwaga sera. For me it worked wonders.
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mnaambiwa msome masomo ya sayansi mnajishaua.Hivi uliwahi sikia somo la biologia?
  Hewa ikipita kooni ngozi pale inakauka, hivyo kuathiri sauti.
  Maji ni ya kurudisha unyevu pale kooni, hili ni tatizo la kibinadamu hasa wazee.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hoja nyingine jaribu kumwuliza jirani yako akusaidie, we kila siku unakunywa maji hata ukikaa tu sembuse anayetumia nguvu na akili kukaukiwa koo unataka aendelee kudondoka jukwaani? Hujatembea na kuona wengine wanavyofanya yakhe? Damn
   
 6. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda hii, someni sayansi wajameni. Hata ya kusafishia macho kwa ku google kinachokutatiza inatosha. La sivyo kila kitu utaona mikogo...
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mbwembwe zao tu.....lakini walimu hatukatazwi kunywa maji wakati tunafundisha
   
 8. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hamna cha biologia wala shangazi yake sayansi kimu, inahitaji moyo kusema uongo mbele ya umma, hapo ni kutafuta kajikonfo tu kakudanganya wananchi
   
 9. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,658
  Likes Received: 5,249
  Trophy Points: 280
  Hawana uhakika na afya zao. Enzi za Ticha ulishawahi kuona "mauzauza" kama hayo?
   
 10. E

  Evergreen Senior Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kunywa Maji wakati mtu ana-address public kwa muda mrefu ni swala la kimaumbile/kisayansi lakini kunywa maji mara kwa mara wakati mtu akizungumza mbele za watu ina maanisha HOFU/WASIWASI!! Dont generalise mambo kwa kujidai umekwenda shule,ww umesoma Sayansi au Sayansi Kimu???!!!
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Mwanzilishi ni Jk, hii ilikuwa ni kumsaidia asingukeanguke kama ilivyo kwaida yake!
  Ni kweli maji ni muhimu lkn utaratibu huu umeanza siku hizi tu baada ya viongozi wetu kuwa na afya mbovu(hasa Jk)
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Watu wa aina hii ndio mnakimbilia kwa waganga wa kienyeji na "wataalam" pindi hata ukipata presha ili kuagua.
  Soma ndugu, soma sayansi!
   
 13. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Unachosema humu ni sahii kabisa, haya mambo ya kuletewa maji ya chupa kwenye vikao na kongamano hayakuwepo siku za nyuma yamekuja hibuka siku za hivi karibuni kwa shinikizo la wafanya biashara ya maji. Tukija kwa viongozi kuwa na glasi ya maji wanapo toa hotuba, naona hayo ni mambo ya mbwembwe tu na KUNATA, nisijuwe kwa Jakaya labda yeye ana a good reason ya kunywa maji, yeye hana hulka ya kupenda makuu au mambo ya KUNATA.
   
 14. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nahisi Wewe ni mwanachama wa Chadema,uwezo wa kufikiri ni mdogo uwezo wa kufanya maandamano unao
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi kuna mtu huku jamvini leo 2011 hajui wala hataki kujuwa umuhimu wa kunywa maji wakati unatoa speech ndefu? Mkullo ametoa speech ya budget kwa zaidi ya saa 2! Kunywa maji kama mtu anatoa speech ndefu is a human-thing. Angalia wanasiasa wa nchi zingine wakati zingine.Maybe tufundishane nini umuhimu wa maji mwilini!!!!
   
 16. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Inatokana na mazoea ya kula sana kitimoto.
   
 17. k

  kazuramimba Senior Member

  #17
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wewe unaonekana ulikuwa kilaza darasani yaani zuzu kabisa na sijui mode ameruhusuje stupid thread kama hii manake inajaza ubao tu.Kama hujui umuhimu wa maji acha kunywa uone! Kilaza wa vilaza wewe.Ndo nyie mnao bania thread za maana sikose nafasi! acha ushabiki usiokuwa na maana.
   
 18. p

  plawala JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwmaba maji yanahitajika wakati wa hotuba ndefu haina mjadala,hoja ni kwamba kuna dalili za kwamba matumizi yanazidi kiwango kinachotegemewa,kukimbilia glasi mara kwa mara kunaweza kuwa na sab nyigine kama kupunguza wasiwasi, afya mgogoro,uzee nk
  halafu tofauti ipo kat ya mtu na mtu,wengine wanaweza kuongea hata masaa 3 bila ya kugusa maji
   
 19. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  watu wanajifanya kubobea biologia,sijui ya std2 au3? Ni wapi elimu ya biolojia inasema ukiwa unaendelea na zoezi unywe maji? Kwanza unapishana na biolojia kwa kuwa ktk zoezi lolote ikiwemo kula,kuongea au michezo hupaswi kunywa. Mara nyingi wanaoamua kutafuna pipi laini,kunywa maji mbele za watu au kulamba midomo,hufanya ivo kulainisha kinywa au midomo. Na wataalam wa magonjwa mbalimbali wanajua kwa nini midomo ukauka,upauka au kukauka koo kwa mtu asiyefanya kazi ngumu, au mtu anayetumia madawa makali yakiwemo madawa ya kulevya. Katika ili simshauri rais wangu afanye tabia iyo wataalam watamregard visivyo. Kwa kuwa binadamu anashauriwa kunywa takriban litre 1.5 mpaka3 ,mh anaweza kunywa hata litre nzima kabla ya kuja ukumbini na akanywa hata litre nzima baada ya hotuba. Mwl nyerere aliweza,mkapa akaweza,itakuaje mrithi asiweze?
   
 20. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Maji ni Uhai, sidhani kama ni jambo baya kunywa maji wakati ukihutubia.
  Besides, wanaokereka mtu akinywa maji mara kwa mara ndiyo watakaokereka zaidi iwapo mtu huo ataanguka eti kisa ameishiwa maji mwilini ....
   
Loading...