Tetesi: Tenda zote za Serikali na makampuni binafsi kuwa monitored na serikali, mawakala binafsi hawana nafasi tena

Atashindwa,
Awape tenda wasukuma kama anavyojifaragua kwamba na yeye ni msukuma kumbe ni mkimbizi tu ila hayo mambo atashindwa na alishashindwa kitambo sana

Kuna vitu msd hawana wala hawawezi to supply Kwa wakati,

Vifaa vya shule, maabara they know nothing kuhusu hiyo business

Jiwe awe wazi tu, nchi imemshinda akae pembeni
Kila likiisha jambo linakuja lingine,

Kwa habari zilizopo ni kwamba kunaandaliwa utaratibu maalumu wa kuwa na watu maalumu kwa ajili ya tenda mbali mbali kwa sekta zote, hospitali, shule, na makampuni mbalimbali ya nchini tender zote zitapitia kwa wakala wa serikali atakaye kuwa apointed

Nje ya tetesi kwa makampuni mengine ila
Kwa uhakika zaid kwenye shule zote za binafsi na serikali wameshapelekewa form za kujaza tokea mwaka jana ila haikuwa implemented,
Sasa kazi inaanza,

Hutaruhusiwa kununua Hata sindano mfano kama una dispensary yako, ni mpaka uigaze kupitia kwa wakala,

Ukitaka madaftari kwa ajili ya shule yako inabidi ununue kupitia kwa wakala,

Inamaana wale mawakala wa usambazaji wa vifaa vya maabara, shuleni, madawa, samani na vingine vyote ulaji wao ndo unafungwa hivo

ANGALIZO
MPANGO HUU WA SERIKALI UTAFELI TU MAANA NIA NI KUFANYA KUTUNISHA MFUKO WA HUYO ATAKAYEKUWA WAKALA,

PIA SERIKALI IACHE HASA KUCHUKIA MASHIRIKA BINAFSI,

HATUSHINDANI KWA KUCHEZEANA FAUL, ILA NI KWA KUBORESHA MAZINGIRA,

Britannica

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Mzee mbona anajipa kazi Nyingi za kufanya zisizo na tija ,Kama nchi imemshinda si aende zake ,kuna kila dalili dereva kasalenda .Mambo Yote anayofanya hafanikiwi ,hivi huwa hajiulizi tu ?Hivi ccm walituonaje watanzania mpaka kutuletea huyu Mzee .
 
Walipewa nafasi za juu katika biashara hii wakaleta kuua viwanda vyote, wakasambaza vitu hewa acha wanywe jeuri yao.
 
Serikali ya ovyo tu ndio inayoweza kudharau sekta binafsi..

Nikikumbuka jiwe alivyodanganya kuwa Hostel za UDSM zilijengwa kwa 10Bil na TBA halafu CAG kwenye ukaguzi akasema ni 54Bil ndio pesa iliotumika nacheka na kuona Ikulu kuna kichaa kabisa..

Yote ni kudanganya umma kwamba sekta binafsi ni wezi.
Na bado zimezingua upigaji upo sana,,sijui anapodanganya inamsaidia nn
 
Hili ni tatizo linguine. Kwanza walianza na MSD kuifanya ndo muingizaji na msambazaji pekee wa vifaa tiba, vitendanishi na dawa kwa hospitali za serikali. Kwa uamuzi huu serikali ililenga kukwepa ongezeko la bei za bidhaa na huduma kutoka makampuni ya watu binafsi ambao ni mawakala (representatives) wa makampuni ya uzalishaji (manufacturers). Kwahiyo MSD inaagiza moja kwa moja kutoka kwa manufacturers na kusambaza mahospitalini.

Utaratibu huu wa kuwakwepa wasambazaji kutoka sekta binafsi una changamoto nyingi na kwahiyo bado haujawa na ufanisi. Kwanza, tofauti na makampuni binafsi, MSD hawatembei kwa wateja (hospitali) na kujua mahitaji yao (yaani hawafanyi sales and marketing). Wanachofanya ni kuwauzia wateja bidhaa walizonazo. Ubaya wake ni kwamba wateja wanakosa bidhaa wanazozihitaji na wanazozipata zinakuwa hazina ubora unaotakiwa.

Biashara hasa ya bidhaa za kisayansi ni very dynamic na inahitaji intelijensia ya hali ya juu kujua nini kinahitajika sokoni. MSD hawana intelijensia ya kibiashara kitu ambacho kinawafanya wasijue waingize bidhaa gani na kwa wakati gani. Mathalani, msimu huu wa masika wasambazaji wa kampuni binafsi tayari walishatambua kulikuwa na mahitaji ya kaseti za kupima homa ya dengue na sio malaria wakati MSD hawakuja hilo na kwa hiyo hawakuwa na kaseti za homa hiyo kwenye bohari lao bali za malaria. Matokeo yake kaseti hizo zikawa hadimu na bei yake ikawa juu Zaidi kuliko kawaida na zilipatikana kwa makampuni ya watu binafsi tu kwa bei ya sh. 300,000 hadi 350,000 na bei ya kipimo chenyewe huko mahospitalini ikawa hatari tupu (elfu 40-70).

Ukweli ni kwamba bei ya kaseti na huduma ya kipimo cha homa ya dengue haina tofauti na homa ya malaria ambayo kwa kawaida hugharimu sh. 3000-5000. Lakini bila kuzingatia kuwa dengue ni homa ya mpito, MSD nao baadae kabisa wakaanza kuingiza kontena za kaseti za dengue ambazo bila shaka zitaishia ku-expire. Cha ajabu ni kwamba ingawa bei ya kipimo hicho toka MSD ilipungua ukilinganisha na ile kutoka kwa wasambazaji binafsi, bado haikuweza kupungua kufikia bei ya kawaida ya sh. 3000-5000 wakati MSD kama wa serikali huingiza bidhaa kwa njia za mkato.

Changamoto nyingine ni kwamba baadhi ya vifaa tiba havihitaji kusambazwa tu kwa wateja, bali kuna huduma (after sale services) zinatakiwa ziendelee kutolewa na manufacturers. Kawaida ni kwamba, manufacturers hutoa huduma hii kupitia mawakala wao waliopo katika nchi husika ambao huwapa mafunzo maalumu ya kuweza kutoa huduma hiyo. Ukweli ni kwamba after sale-services ni “closed system” kwa maana si kila wakala anaweza kutoa huduma hiyo kwa vifaa tiba kutoka manufacturer mungine. Bali manufacturers wengi hawako tayari kufungamana na wakala mwenye mafungamano na washindani wao.

Kwahiyo MSD kama wakala hawataweza kufungamana na competing manufacturers kwa wakati mmoja kama vile BD, Thermo Scientific, Carestream, Philips, SonoScape, Fazzini, Uzumcu, Roche Diagnostics, Sysmex,Abbott, Human Diagnostics, FujiFilm, Liofilchem, Oxoid, Fiochett, Snibe, Eppendorf, Cephaid, Mindrey, Erba, Stago, Applied Biosystems, Himedia, Instrumentation Laboratory, Sharlau, Merk Millipore, Sigma Aldrich, Life Technologies, Omega, Qiagen, Promega, Bio-Rad, Tekkim Kimya, Zeiss, Optika, Olympus n.k. Kiufupi ni kwamba utaratibu wa biashara unaopendekezwa na serikali hautokuwa na tija bali ni kuharibu soko huria na utasababisha kuadimika kwa bidhaa shindani.
 
Inasiktisha sana...

Hapo kutakua na msongamono mkubwa sana wa ununuzi vifaa...

Unatoa order leo, unaipta baada ya miaka2 na pesa ishaliwa...

Mifumo ya serikali ipo slow sana...


Cc: mahondaw
 
Hap Sijaelewa ,ko inamaana kutakuwa hakuna manunuzi kupitia suppliers wa Gpsa?suppliers Msd?
 
Hapa ndio wale wanaoshabikia vyama vya upinzani kufa wajue hatari itakayowakabili pindi hilo likitimia.

Sasa hivi kuna kodi nyingi zinaendeshwa kimya kimya kibabe na hakuna ruhusa ya kuongea wala chombo chochote cha habari kuripoti.

Uchumi umeyumba vibaya sana na waliotaka sifa hawana ujanja, namna pekee ni ni kupora hela za wananchi kwa kodi za kitapeli.

Haya yanayoendelea yatakaa wazi tu pindi mishahara itakapooacha kulipwa. Yajayo yanasikitisha.
Hapo kwenye mishahara athubutu, ndio atajua hata kunguru huwa anauma akizidiwa.
 
Kwa hii jiwe ataangukia pua tu,
Kwenye kupima ardhi tu wanachemsha, wanaweka kampuni binafsi, huyu jamaa ni kama mchawi/mwanga
 
Back
Top Bottom