Tetesi: Tenda zote za Serikali na makampuni binafsi kuwa monitored na serikali, mawakala binafsi hawana nafasi tena

Kila likiisha jambo linakuja lingine,

Kwa habari zilizopo ni kwamba kunaandaliwa utaratibu maalumu wa kuwa na watu maalumu kwa ajili ya tenda mbali mbali kwa sekta zote, hospitali, shule, na makampuni mbalimbali ya nchini tender zote zitapitia kwa wakala wa serikali atakaye kuwa apointed

Nje ya tetesi kwa makampuni mengine ila
Kwa uhakika zaid kwenye shule zote za binafsi na serikali wameshapelekewa form za kujaza tokea mwaka jana ila haikuwa implemented,
Sasa kazi inaanza, achia mpango wa watumishi kuwalazimishwa kutumia Posta na TTCL,

Hutaruhusiwa kununua Hata sindano mfano kama una dispensary yako, ni mpaka uigaze kupitia kwa wakala,

Ukitaka madaftari kwa ajili ya shule yako inabidi ununue kupitia kwa wakala,

Inamaana wale mawakala wa usambazaji wa vifaa vya maabara, shuleni, madawa, samani na vingine vyote ulaji wao ndo unafungwa hivo

ANGALIZO
MPANGO HUU WA SERIKALI UTAFELI TU MAANA NIA NI KUFANYA KUTUNISHA MFUKO WA HUYO ATAKAYEKUWA WAKALA,

PIA SERIKALI IACHE HASA KUCHUKIA MASHIRIKA BINAFSI,

HATUSHINDANI KWA KUCHEZEANA FAUL, ILA NI KWA KUBORESHA MAZINGIRA,

Britannica
Baada yakufanya hayo yote wanaoshauri watakuja gunduwa hali ni Tete Mali hazipatikani Kwa wakati na watu wanapanga folen kununua bidhaa kiukweli hatuna jinsi Ila Mungu ashuke atutetee wa Tz.
 
Itasaidia kukomesha wizi maana makampuni yalikuwa yanachukua tenda kwa gharama kubwa sana ukilinganisha na uhalisia, hongera sana JPM
Hili ni soko huru ,sasa turudi basi kwenye ujamaa.......imeletwa taneps imetosha
 
Tunakoelekea hii serikali itaanza hata kuuza Ice cream yenyewe na kupiga marufuku wananchi wengine kuziuza
Afadhali serikali. Bila serikali tusingekuwa na umeme wa mabwawa, wala Tanesco wala vyuo vikuu vya mwanzoni na vinginevyo,wala viwanda mbalimbali ambavyo japo vilikufa kwa uzembe wa uendeshaji tumeoneshwa njia. Muhimbili nani angewekeza hivyo? Hii ya gesi waliotupiga unaweza kuona umeme wake ulivyo ghali. Hakuna mtu binafsi angejenga bwawa la Rufiji la Mwl. JK Nyerere tunalotegemea litupatie umeme wa bei ya chini kama kidatu, kihansi na nyumba ya mungu. Nchi zote haya yanaendelea kujengwa na serikali kama three gorges ya china na lile la ethiopia linalozalisha umeme mpaka wanauza nchi za jirani. Watu binfsi ni biashara ndio namba moja. Haijali wewe una uwezo au la.
 
Back
Top Bottom